Gharama ya kununua nyumba za NHC

Kinachofanya hizi nyumba ziwe na bei hizi ni nini?

Huwezi kuniambia bei ya apartment Dar inakuwa sawa na - au hata kuzidi- bei ya apartment kama hiyo, yenye services na amenities zaidi, kwenye miji mikubwa mingi kwa mfano ya Marekani. Hasa ukizingatia Purchasing Power Parity na access to credit ilivyo tofauti.

Hizi apartment zinanunuliwa? Na nani? Uchumi wetu umekua kuruhusu bei hizi kuwa competitive? Au ni kwa vile ziko chache sana na wanategemea wachache "wenye nazo"?
 
Waungwana mimi naomba mtu atumie lugha ya hesabu, akokotoe, bei ya kununua nyumba ya kima cha chini ni shilingi ngapi pamoja na riba? Je utaratibu wa kulipa ukoje yaani kama unapunguza deni inatakiwa kwa mwezi utoe kiasi cha shilingi ngapi? na hadi unamaliza deni utakuwa umelipa shilingi ngapi? Na hii kauli kwamba hupewi hati ya kiwanja mpaka umalize deni ni kweli? Na kama ukifariki kabla ya kumaliza deni inakuwaje?
 
Inahitaji wendawazimu kwa mtanzania kununua nyumba ya vyumba vitatu isiyo hata na eneo la kulima mchicha kwa mkopo wa shilingi milioni 300!
Ndio maana nchi yetu ina madeni makubwa na hizo pesa tulizokopa hatujafanyia la maana kulingana na thamani ya hiyo mikopo.
 
Kinachofanya hizi nyumba ziwe na bei hizi ni nini?

Huwezi kuniambia bei ya apartment Dar inakuwa sawa na - au hata kuzidi- bei ya apartment kama hiyo, yenye services na amenities zaidi, kwenye miji mikubwa mingi kwa mfano ya Marekani. Hasa ukizingatia Purchasing Power Parity na access to credit ilivyo tofauti.

Hizi apartment zinanunuliwa? Na nani? Uchumi wetu umekua kuruhusu bei hizi kuwa competitive? Au ni kwa vile ziko chache sana na wanategemea wachache "wenye nazo"?

Mkuu nimejaribu kufuatilia miradi mingi ya NHC lakini kwa kweli huwezi kuona ni jinsi gani mwananchi wa kawaida anaweza kumudu kununua nyumba hizi. Labda tuambiwe malengo ya kuanzishwa kwa shirika hili yamebadilika? Maana hata ukiangalia hizo low-costing houses zao bei bado ziko juu sana. Je beneficiaries wa NHC wamebadilika?
 
Hii ni nchi ya kibepari mshikaji. Maskini wanatakiwa pembezoni mwa mji na kwenye nyumba za matofali ya kuchoma.
 
Tunasubiri za waswahili huku Mpiji Magohe labda bei zitashuka hizo za Upanga ni za Wahindi

Mkuu kuna mradi unakuja wa Kibada. I hope hawa jamaa watatuuzia nyumba kwa bei affordable kwa wengi. Maana so far nyumba zinazouzwa ni kama vile zimewalenga wenye uwezo mkubwa zaidi ambao huenda wengi wao wana nyumba zao wenyewe tayari.
 
Hii ni nchi ya kibepari mshikaji. Maskini wanatakiwa pembezoni mwa mji na kwenye nyumba za matofali ya kuchoma.

Mkuu mwalimu alipoanzisha NHC hakutaka iwe hivi. NHC ililenga kuwasaidia walalahoi. Matajiri wanamudu kujenga nyumba zao tena nzuri tu kuliko walala hoi ambao huishia kujenga kuta nne za 'banda' na 'kuchafua' muonekano wa miji yetu.
 
NHC si ya watanzania, ni ya wahindi, wapemba, waarabu, wasomali, n,k na mafisadi wa kitanzania wenye hela haramu!! Mtu mwadilifu kazini hawezi kununua hizi nyumba!! Badala ya kuwauzia wazawa ambao wanaenda kazini kila siku ili wawe karibu na ofisi wanawauzia wahindi wafanya biashara.
 
Mkuu kweli kwa mishahara yetu hii sidhani kuna mwananchi mfanyakazi wa kawaida na wa kati anaweza ku-qualify hata hiyo mortgage financing toka kwenye mabenki. Maana vigezo pia ni kipato chako ili kujua kiasi ambacho wanaweza kukupatia kununua nyumba. Naona focus ya shirika sasa inahamia kuwasaidia matajiri (ambao wengi wana uwezo wa kujijengea nyumba zao) na kuwaacha solemba walalahoi.
 
....milioni 320? Wana wazimu hawa, mil 320 najenga nyumba kadhaa napangisha, na nikiamua kupachika tofali napachika nyumba za kutosha napangisha mjini...
 
jamani mahela yote hayo dah sa hizi ndio za mtanzania wa kawaida kweli au ni matajiri kwa income gani eh kweli mwenye nacho anaongezewa haya wenye hela zao
 
Mkuu kuna mradi unakuja wa Kibada. I hope hawa jamaa watatuuzia nyumba kwa bei affordable kwa wengi. Maana so far nyumba zinazouzwa ni kama vile zimewalenga wenye uwezo mkubwa zaidi ambao huenda wengi wao wana nyumba zao wenyewe tayari.
Thubutu,
Huo mradi wanasema ni wa nyumba za watu wa kipato cha chini lakini nakuhakikishia subiri majina ya waliopata yatakapotoka ndio utajua.
Hawa jamaa wa NHC ni wezi waliojihalalishia wizi wao kama wale wa temeke manispaa ambao kila kukicha wanachukua hela za fomu 20,000 za viwanja kwa ajiliya kugawa viwanja 300 kwa tu, tena kwa wakubwa.Hii nchi ina wezi halali wengi sana aisee
 
Kimfumo Tanzania tunachochea ufisadi. Huwezi kutarajia mtu anunue nyumba kutoka serikalini kwa milioni 320 wakati mtu mshahara wake kwa mwezi mzima milioni haifiki huko serikalini bila ya kumruhusu mtu huyo kujiingiza kwenye ufisadi

Ni aibu kwa shirika la serikali kuja na bei hizi
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi anatakiwa kuchunguza kinachoendelea ndani ya NHC ambako kunadaiwa kuwepo ombwe la uongozi licha ya sifa nyingi alipewa ndugu Mchechu alipoteuliwa kuongoza shirika hili. Inaonyesha Bodi ya Wakurugenzi ni dhaifu sana na baadhi ya watumishi ktk menejimenti hawana uchungu wowote na shirika,wao ni kujilipa posho kubwa kubwa na safari zisizo na tija!
 
Mkuu nimejaribu kufuatilia miradi mingi ya NHC lakini kwa kweli huwezi kuona ni jinsi gani mwananchi wa kawaida anaweza kumudu kununua nyumba hizi. Labda tuambiwe malengo ya kuanzishwa kwa shirika hili yamebadilika? Maana hata ukiangalia hizo low-costing houses zao bei bado ziko juu sana. Je beneficiaries wa NHC wamebadilika?

Kwa mara nyingine tena Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo 24 Oktoba, 2012 limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Mindu, jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huu ulianza rasmi mwezi Novemba mwaka 2011, na unatarajiwa kukamilika rasmi Aprili 2013 na mteja kuweza kukabidhiwa nyumba yake mwezi Mei 2013,

Kila nyumba itauzwa kwa bei ya TZS 272,050,673.08 bila kodi ya ongezeko la thamani (VAT ) na TZS 321,019,794.24 ikiwa na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
Wanabodi
kama kuna mtu au watu wanafanya uhuni ni huyu mkurungernzi wa NHC na watu wake.
1. Anaweka VaT makusudi ili tuone kwamba ni VAT, ila hiyo ni % hivyo ukiweke bei juu lazima itapanda, na bei ikiwa chini itapungua.
2. Anachukua mkopo kwa wanunuzi, bila kuwapa lipa, ona anauza Oktoba na kisha anakupa nyumba May 2013, maana yake anakaa na asilimia 80 yako kwa miezi zaidi ya minane ( kama itakamilika on time vinginevo kwa mwaka) fikiria kama mtabidi watu 60 @ akalipa 80% ya 272 m, mtakuwa mtoa mkopo wa Tsh 217.7 x 60= 13,062/m (billion 13) hazina liba kwa nusu mwaka, huu ni mkopo free100%
3. Unapo kuwa na NHC, kwa ukubwa wa mradi tunategemea gharama za ujenzi zipungue, ila NHC zinaongezeka.
4. Wastani wa mshahara Tanzania, ukiondoa (biases inaopatikana kwenye mabenki na contract za international organization) unakadiriwa ni Tsh1,500,000pm.

Mchanganuo wa jumla, kwa urahisi sana, 321, 019,700 / miezi 360= (sawa na miaka30) makato ya mwezi 891,721.50. kumbuka wastani wa mshahra kisha toa statury deduction kodi 30% na kisha ILO (sheria ya kazi) wanataka ubaki na 1/3 ya mshahara. Hivyo basi 1,500,000- 450,000(tax) - 500,000 (1/3 Labor law) baki 650,000/ kumbuka rejesho ni 900,000 ambayo ni principal amount bila riba, legal fee, loan fee, n.k

Ndugu hizo ni hesabu za harakaharaka tu, kwenye keyboard. Swali watu wangapi wana mshahara huo au juu ya huo? je watu hao walio bakiziwa 500,000 kwa mwezi wataenda kazini, watakula, watavaa, watalipa umeme na maji, matibabu na ada za watoto, kisha wajiwekee hakiba kwa tahadhari?
Mwisho, Mkurugenzi anatumia ujana na ujanja tu, kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu, nashangaa hata wanaompa mkopo huo, kabla hata nyumba hazijaisha, na ndo wanamfanya aone mahitaji makubwa na watu wanahela, kumbe wanaweza kuwa wasomali, wahabeshi, waarabu, wahindi wararushwa, wazee wa mujuni,n.k
lpo siku tutajua ukweli NHC ipo kwa faid ya nani.
Wakatabahu
 
Kwa mfano nyumba za mradi wa Mindu ni apartments. Hivyo unauziwa apartment moja kwa shs. 321,019,794.24!!! Hivi bei za apartments kwa wenzetu zikoje? Si ilitakiwa apartments ndio ziwe nyumba za bei chee?!! Maana kwa wenzetu matajiri ndio unasikia mtu anamiliki nyumba iliyojengwa kwenye eneo la eka 50, yenye vyumba 10 vya kulala, mabafu 8, swimming pool 3, viwanja vya tennis, basketball, sebule 3 n.k n.k ila kwa wasaka nyoka, apartments ndio mkombozi.
 
Jamani bei ya apartment inaangalia na sehemu yenyewe pale. Mindu ni karibu na kariakoo,Posta.
Kingine angalia mtaa ulivyo pembeni ya hiyo kuna Canal residency ambayo kwa mwaka ni 48mil tena unalipa installment mbili tu. Richmond towers iko mbele ya Canal hizi pamoja na swiss tower ni za muhindi mmoja anamiliki Cassino Posta hizo bei napo ni mbaya nyumba yauzwa $200000
 
Back
Top Bottom