Gharama ya kumhamisha mtumishi kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kituo kingine

IlangiKwetu

Member
Oct 9, 2014
85
33
Heshima mbele wadau,

Naomba kujua gharama ama stahiki ambazo anapaswa mwajiri kumpa mtumishi anapompa uhamisho kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kituo kingine cha kazi. Mfano kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam.

Kwa kuzingatia cheo cha mtumishi huyo (Senior/Junior level)

Ikiwa pia gharama ya kusafirisha mizigo ya mtumishi huyo.

Nawatakia Chrismass/Noel njema.
 
Atalipwa kama ifuatavyo:-
1.Pesa ya kusafirisha mizigo tani 10, kila tani ni Tsh 1,500/km

Tani 10*Tsh 1,500*idadi ya kilomita

2.Pesa ya kujikimu ya siku 14,yeye na mkewe. Kwa senior officer ni Tsh (120,000 *14)*2

3.Pesa ya kujikimu ya siku 14 kwa watoto.. (60,000*14)*idadi ya watoto

4.On transit allowance.. Kila baada ya masaa 8 ya safari Tsh 60,000

5.Night allowance.. Tsh 120,000*idadi ya nights

6.Disturbance allowance.. Hapa atapewa mshahara wa mwezi mmoja

7.Fedha za kufunga na kufungua mzigo.. Tsh 500,000*2

8.Fedha ya teksi.. Tsh 200,000*2
 
Back
Top Bottom