Gharama ya demokrasia ya kimagharibi.

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,299
2,000
Nimekaa nikafikiria,hivi katika nchi maskini kama Tanzania,na baadhi ya nchi kama malawi,demokrasia ina faida gani.
Kwangu mimi haingii akilini kutumia pesa na rasilimali nyingi za nchi kugharamia vitu ambavyo havina faida ya moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida,Hebu fikiria kila chama cha siasa hapa nchini kinalipwa mamilioni ya pesa kila mwezi kama ruzuku,tuna wabunge kama 360,na kila mbunge analipwa posho,mshahara,na anapewa fedha kibao kupitia mfuko wa jimbo,miezi kadhaa iliyopita Iliundwa tume ya Raisi kukusanya maoni kuhusu katiba,wajumbe wake walikuwa wanapokea posho ya laki tano kwa siku 500,000TSH,kwa siku zote walizofanya kazi.walipangishiwa nyumba,wakapewa magari ya bei mbaya kufanyia kazi zao.

Hayo tisa,kumi bunge la katiba liliundwa karibu na wajumbe 600,kila mmoja alikuwa anapata TSH 300000.KWA SIKU.hebu fikiria kwa siku 70 walizo kaa hapa dodoma,ni fedha kiasi gani imetumika,its alot!.

Sasa hv viongozi wa CCM,na UKAWA wanazunguka nchi nzima kueneza siasa,hiyo mizunguko yao inafaida gani kwa MTZ wa kawaida,mizunguko hiyo inaleta vp huduma bora za matibabu,ajira kwa wasomi wetu,viwanda nk.Mi naona ni upotezaji wa rasilimali za nchi bure.

Kwanini tusisitishe haya mambo ya demokrasia,(SUSPEND THE CONSTITUTION) ili tujierekeze kwenye mambo ya msingi kwa nchi hii,kuna tetesi kwamba nchi ipo hoi ki fedha,na kuna hati hati kwamba mikopo kwa ajiri ya wanaojiunga na elimu ya juu ikawa kidogo.

JWTZ mpo wapi,kwanini msifanye kama THAILAND,jeshi lao limeona wanasiasa wanaweka usiku tu,wanabishana kila leo,mambo ya msingi kwa uchumi wa nchi hayaendi,wakaamua kuchukua nchi,nyie mnasubiri nini,au na nyie mmeisha chafuka na UFISADI,

Inakera sana,kijana kutwa nzima unasaga rami kutafuta ajira upati,walioajiriwa vipato ni vidogo kiasi kwamba uwezi kuweka hata akiba kwa ajiri ya baadae,wakati huohuo unaa mbiwa kuna mbunge anafunga ndoa ya kifahari ya 9600000TH,BONGO ! Kazi ipo,ni masiara wakuu

Jumapili njema,karibuni zabibu za dodoma.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom