Gharama ya awali ya Katiba mbovu na NEC isiyo huru.... Bilioni 2! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gharama ya awali ya Katiba mbovu na NEC isiyo huru.... Bilioni 2!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bill, Dec 17, 2010.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,237
  Trophy Points: 280
  Imeelezwa kuwa gharama za kuendesha kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi ni Tshs Bilioni 2 kwa uchache na hizi gharama zinalipwa na waTZ waliodhulumiwa haki zao na watawala walioamua kujitangazia watu waliowataka.

  Gharama hizi ni matokeo ya Katiba yetu mbovu, NEC isiyo huru, wasimamizi wa kura kwenye majimbo wasio huru.

  Tumeanza kwa kulipa Pesa Bilioni 2 ikiwa ni gharama ya Katiba mbovu na NEC isiyo huru, kinachofuata waTZ watalipa DAMU YAO ikiwa ni matokeo ya watawala wetu kung'ang'ania katiba hii mbovu na NEC isiyo huru.

  MABADILIKO YA KATIBA NI LAZIMA ILI KUEPUKA UMWAGAJI WA DAMU YA WATZ
  Source - Tanzania Daima

  Bilioni 2/- kutumika kesi za uchaguzi


  na Irene Mark


  [​IMG]
  ZAIDI ya sh bilioni 2.2 zitatumika kwa ajili ya kusikiliza kesi 43 za uchaguzi, kupinga matokeo ya ubunge katika vituo 11 vya Mahakama Kuu hapa nchini.
  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Jaji Kiongozi Fakhih Jundu, alisema fedha hizo zinatakiwa kuifikia Mahakama kabla ya Februari mwakani wakati shughuli za mhimili huo zitakapoanza.
  Alisema, kesi zilizofunguliwa hadi Desemba 10 mwaka huu zinalazimika kusikilizwa na kumalizika katika kipindi cha miaka miwili ambapo Mahakama Kuu itasikiliza kesi kwa mwaka mmoja na kutoa nafasi ya mwaka mwingine kwa ajili ya watakaokata rufaa kupinga hukumu zitakazotolewa.
  Jaji Kiongozi huyo alibainisha kwamba kutokana na idadi ya Majaji waliopo, kila kesi inakadiriwa kusikilizwa ndani ya siku zisizopungua 45 huku ikikadiriwa kuwa na wastani wa mashahidi 15 kwa kila kesi.
  "Inakisiwa kuwa kila kesi itasikilizwa kwa muda wa siku zisizopungua 45 vile vile wastani wa mashahidi 15 wanakadiriwa kuwepo kwenye kila kesi na ili haki iweze kutendeka, jaji hatasikiliza kesi katika kituo chake cha kazi hivyo tutalazimika kuwasafirisha majaji kutoka kituo kimoja kwenda kingine," alisema Jaji Kiongozi Jundu.
  Katika ufafanuzi wa gharama za uendeshaji wa kesi hizo, Jaji huyo alisema kiasi cha sh 52,644,000 zitatumika kwa kila kesi hivyo kiasi cha sh 2,263,692,000 zitatumika kugharamia uendeshaji wa kesi zote 43 zinazopinga matokeo ya ubunge.
  "…Hizi ni fedha nyingi na lazima serikali izitoe, tumeshaiandikia hazina itutafutie fedha hizi. Mahakama haina pesa, huu ni mzigo wa serikali lazima ibebe mzigo huu.
  "Nasema lazima serikali izitoe kwa sababu ni matakwa ya demokrasia… na hizi ni gharama za demokrasia ni vizuri wote tufahamu hivyo," alisisitiza Jaji Kiongozi Jundu na kuongeza kwamba hiki ni kipindi cha likizo ya Mahakama hadi Februari mwakani tutakapoanza kazi.
  Kadhalika, Jaji huyo alitoa rai kwa walalamikaji kujiandaa vema huku akiitaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni mdau mkubwa kujiweka sawa ili kuziwezesha kesi hizi kufanyika bila vikwazo.
  "Isije ikawa mtu kafungua kesi akiwa hajajiandaa ndiyo maana kwa kuzingatia gharama hizi ipo sheria inayomtaka mlalamikaji anayepinga matokeo kupeleka mahakamani kiasi cha sh milioni tano.
  "Hizi ni kesi nzito lazima kujipanga mtu asiende kwa kujaribu kwa sababu mwisho wake matokeo yatakua mabaya kwa aliyefungua kesi itambidi kulipa faini… nawashauri kama mtu ameshindwa asubiri kipindi kijacho," alisisitiza Jaji huyo.
  Aidha, alibainisha kuwa usikilizwaji wa kesi hizi utaathiri mwendelezo wa kesi nyingine kama za mauaji na nyinginezo hali inayoweza kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi wengine. Jaji Jundu aliitaja mikoa inayoongoza kwa wingi wa kesi hizo na idadi yake kwenye mabano kuwa ni Tabora (9), Dar es Salaam na Mwanza (7), Mtwara (5), Mbeya (4), Moshi (3), Dodoma, Iringa na Arusha (2) wakati Bukoba na Sumbawanga (1).
   
 2. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ktiba mpya ni muhimu sana,wmkuu leo nasikia anatoa tamko la serikali sijui tusubiri maana huyu mzee naye keshapitwa na wakati tangu enzi za mwl yupo tu
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Na kwa nini gharama hiyo iwe kubwa wakati watu wanatafuta haki yao? Utawala bora uko wapi?
   
 4. k

  kayumba JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii ni sheria ya kikoloni mamboleo? Ebu fikiria mtanzania wa kawaida huko kijijini amejitokeza kugombea ubunge alafu uchaguzi ukatawaliwa na mizengwe (kutoka kwa wasimamizi na dola) na rushwa alafu akashindwa. Je ataweza kupata milion 5 kwa ajili ya kufungua kesi? Nimeshangaa huyo Jaji kuona ni kitu cha kawaida. Kuna watu watashindwa kudai haki yao kwa vile tu ni maskini. Amakweli aliyeshiba hamjui mwenye njaaaaaaaaaaaaaa!

   
 5. n

  niweze JF-Expert Member

  #5
  Dec 19, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya Kura Wameiba Sasa Wanaendesha Kesi na Gharama Hizo za Mabilioni Kuwalipa Wajadili Ulaji wa Hela. Well Hii Ndio Demokrasia Unapo Wapa CCM Watukanyage Kama Maji Machafu. CCM ni Professional kwa Wizi...
  Katiba Ikowapi Tuwaondoe Hawa Wezi?
   
 6. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kikwete anaipeleka nchi hii kuzimu
   
 7. n

  nyantella JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Hivi nyie Chadema mnapotukana Judges, usalama wa taifa, polisi, jeshi almost taasisi zote nyeti mkipata uongozi wa nchi mtaanzisha kila kitu? yaani hizo taasisi zote do you real thaink is possible? jaribuni ku-think outside the box and there is no way you can have watu woote waka wa supprt! wake up!
   
Loading...