tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,817
- 18,241
Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kupepesa macho. Tangu kampuni za simu za mkononi zivumbue njia mpya ya kununua umeme wa LUKU bure kupitia mpesa, tigo pesa, airtel money, etc, ununuzi wa umeme umekuwa rahisi sana. Ununuzi wa umeme unaweza kufanyika muda wowote, iwe usiku au mchana au wakati hali ya hewa inapokuwa mbaya, kwa mfano, wakati wa mvua. Mtu kulala giza wakati una salio kwenye mpesa, tigo pesa au airtel money, ni kujitakia mwenyewe.
Baada ya serikali ya awamu ya tano kugundua kwamba wananchi wanafaidi bure huduma hii ya kununua umeme, ambayo kimsingi serikali haichangii chochote, serikali tukufu ya awamu ya tano, wameamua kuwakamua wananchi bila shuruti na bila sababu zozote za msingi. Mwanzoni huduma hii ilikuwa ikipatikana bure kabisa lakini sasa wananchi wanyonge watahitajika kukamuliwa 1.1% ya gharama za kununua umeme. Hii ni mbali na 18% VAT, 3% REA na 1% EWURA tunazokamuliwa kila kukicha.
Serikali hii inayojinasibu kuwajali wanyonge imeamua, kwa makusudi kabisa, kuwaongezea wanyonge mzigo wa gharama za maisha kwa kuwakamua zaidi fedha kidogo walizobaki nazo mifukoni mwao. Sijawahi kuona serikali yenye roho mbaya kwa wananchi wanyonge kama serikali hii ya awamu ya 5.
Kwa wale ambao hamfahamu mzigo wa 1.1% ya gharama za kununua umeme, itabidi twende taratibu mpaka muelewe. Kwa mfano, mwananchi anayemiliki kiwanda kidogo kama saluni, hutumia umeme usiopungua Tsh 100,000 kwa siku. Hivyo, atalazimika kukamauliwa Tsh 1100 kwa siku, sawa na Tsh 33,000 kwa mwezi = Tsh 396,000 kwa mwaka = Tsh 3,168,000 hadi awamu ya kwanza ya utawala wa serikali ya awamu ya 5 itakapoisha. Ikiwa gharama zitaendelea kubaki kama zilivyo hadi mwaka 2025, mwekezaji huyu wa kiwanda kidogo atakuwa amekamuliwa jumla ya Tsh 15,840,000 (shilingi milioni kumi na tano, laki nane na elfu arobaini).
Namba huwa hazidanganyi. Hapa ndipo hii serikali yetu ya viwanda ilipotufikisha. Mantiki ya gharama hizi mpya haifahamiki vizuri kwa wananchi wengi kama ilivyo kwa makato ya VAT, EWURA na REA. Kwa gharama za ajabuajabu kama hizi, viwanda vitaendeshwaje katika nchi hii? Hapa nimetolea mfano mdogo tu kwa mwekezaji mdogo anayemiliki kiwanda cha saluni ya nywele. Ikiwa hali ndiyo hii kwa wawekezaji wadogo, je wawekezaji wakubwa kama akina Dangote si wataikimbia nchi?
Ifike wakati serikali hii iwaonee huruma wananchi wapatao milioni 65 wanaoishi maisha magumu katika nchi hii. Kampuni za simu zina huruma zaidi kwa wananchi kuliko serikali yao kandamizi inayowakamua fedha bila huruma kila kukicha. Kampuni za simu ziliona ni busara huduma hii itolewe bure lakini serikali hii imeona wanachi wanafaidi sana hadi kufikia uamuzi wa ajabu kuwakamua fedha zaidi bila sababu za msingi. Inauma sana.