Gharama mpya za kununua umeme wa LUKU hizi hapa!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,759
18,177
Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kupepesa macho. Tangu kampuni za simu za mkononi zivumbue njia mpya ya kununua umeme wa LUKU bure kupitia mpesa, tigo pesa, airtel money, etc, ununuzi wa umeme umekuwa rahisi sana. Ununuzi wa umeme unaweza kufanyika muda wowote, iwe usiku au mchana au wakati hali ya hewa inapokuwa mbaya, kwa mfano, wakati wa mvua. Mtu kulala giza wakati una salio kwenye mpesa, tigo pesa au airtel money, ni kujitakia mwenyewe.

Baada ya serikali ya awamu ya tano kugundua kwamba wananchi wanafaidi bure huduma hii ya kununua umeme, ambayo kimsingi serikali haichangii chochote, serikali tukufu ya awamu ya tano, wameamua kuwakamua wananchi bila shuruti na bila sababu zozote za msingi. Mwanzoni huduma hii ilikuwa ikipatikana bure kabisa lakini sasa wananchi wanyonge watahitajika kukamuliwa 1.1% ya gharama za kununua umeme. Hii ni mbali na 18% VAT, 3% REA na 1% EWURA tunazokamuliwa kila kukicha.

Serikali hii inayojinasibu kuwajali wanyonge imeamua, kwa makusudi kabisa, kuwaongezea wanyonge mzigo wa gharama za maisha kwa kuwakamua zaidi fedha kidogo walizobaki nazo mifukoni mwao. Sijawahi kuona serikali yenye roho mbaya kwa wananchi wanyonge kama serikali hii ya awamu ya 5.

Kwa wale ambao hamfahamu mzigo wa 1.1% ya gharama za kununua umeme, itabidi twende taratibu mpaka muelewe. Kwa mfano, mwananchi anayemiliki kiwanda kidogo kama saluni, hutumia umeme usiopungua Tsh 100,000 kwa siku. Hivyo, atalazimika kukamauliwa Tsh 1100 kwa siku, sawa na Tsh 33,000 kwa mwezi = Tsh 396,000 kwa mwaka = Tsh 3,168,000 hadi awamu ya kwanza ya utawala wa serikali ya awamu ya 5 itakapoisha. Ikiwa gharama zitaendelea kubaki kama zilivyo hadi mwaka 2025, mwekezaji huyu wa kiwanda kidogo atakuwa amekamuliwa jumla ya Tsh 15,840,000 (shilingi milioni kumi na tano, laki nane na elfu arobaini).

Namba huwa hazidanganyi. Hapa ndipo hii serikali yetu ya viwanda ilipotufikisha. Mantiki ya gharama hizi mpya haifahamiki vizuri kwa wananchi wengi kama ilivyo kwa makato ya VAT, EWURA na REA. Kwa gharama za ajabuajabu kama hizi, viwanda vitaendeshwaje katika nchi hii? Hapa nimetolea mfano mdogo tu kwa mwekezaji mdogo anayemiliki kiwanda cha saluni ya nywele. Ikiwa hali ndiyo hii kwa wawekezaji wadogo, je wawekezaji wakubwa kama akina Dangote si wataikimbia nchi?

Ifike wakati serikali hii iwaonee huruma wananchi wapatao milioni 65 wanaoishi maisha magumu katika nchi hii. Kampuni za simu zina huruma zaidi kwa wananchi kuliko serikali yao kandamizi inayowakamua fedha bila huruma kila kukicha. Kampuni za simu ziliona ni busara huduma hii itolewe bure lakini serikali hii imeona wanachi wanafaidi sana hadi kufikia uamuzi wa ajabu kuwakamua fedha zaidi bila sababu za msingi. Inauma sana.
 
mtoa mada umesahau, achana na hayo maasilimia ya keep constant.

Iko hivi siku hizi nikiwa na 30,000/= mkononi nkienda kwa wakala kununua umeme wa hio pesa inabidi nimuongeze miatano yakwake kama wakala au ninunue umeme wa 29500/= hio miatano inabaki kwake
kumbuka hapo bado sijakatwa hayo makodi unayoyasema,

kuna mtu alikuwa na elfu tano kwa tigo pesa akataka kununua umeme wa elfu tano haikuwezelana akalazimka kununua wa elfu nne alakatwa elfu moja, hapo bado hayo makodi kodi

zaman haya mambo hayakuwepo kabisa au ni huku tu wakuu , huko kwenu vipi?
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kupepesa macho. Tangu kampuni za simu za mkononi zivumbue njia mpya ya kununua umeme wa LUKU bure kupitia mpesa, tigo pesa, airtel money, etc, ununuzi wa umeme umekuwa rahisi sana. Ununuzi wa umeme unaweza kufanyika muda wowote, iwe usiku au mchana au wakati hali ya hewa inapokuwa mbaya, kwa mfano, wakati wa mvua. Mtu kulala giza wakati una salio kwenye mpesa, tigo pesa au airtel money, ni kujitakia mwenyewe.

Baada ya serikali ya awamu ya tano kugundua kwamba wananchi wanafaidi bure huduma hii ya kununua umeme, ambayo kimsingi serikali haichangii chochote, serikali tukufu ya awamu ya tano, wameamua kuwakamua wananchi bila shuruti na bila sababu zozote za msingi. Mwanzoni huduma hii ilikuwa ikipatikana bure kabisa lakini sasa wananchi wanyonge watahitajika kukamuliwa 1.1% ya gharama za kununua umeme. Hii ni mbali na 18% VAT, 3% REA na 1% EWURA tunazokamuliwa kila kukicha.

Serikali hii inayojinasibu kuwajali wanyonge imeamua, kwa makusudi kabisa, kuwaongezea wanyonge mzigo wa gharama za maisha kwa kuwakamua zaidi fedha kidogo walizobaki nazo mifukoni mwao. Sijawahi kuona serikali yenye roho mbaya kwa wananchi wanyonge kama serikali hii ya awamu ya 5.

Kwa wale ambao hamfahamu mzigo wa 1.1% ya gharama za kununua umeme, itabidi twende taratibu mpaka muelewe. Kwa mfano, mwananchi anayemiliki kiwanda kidogo kama saluni, hutumia umeme usiopungua Tsh 100,000 kwa siku. Hivyo, atalazimika kukamauliwa Tsh 1100 kwa siku, sawa na Tsh 33,000 kwa mwezi = Tsh 396,000 kwa mwaka = Tsh 3,168,000 hadi awamu ya kwanza ya utawala wa serikali ya awamu ya 5 itakapoisha. Ikiwa gharama zitaendelea kubaki kama zilivyo hadi mwaka 2025, mwekezaji huyu wa kiwanda kidogo atakuwa amekamuliwa jumla ya Tsh 15,840,000 (shilingi milioni kumi na tano, laki nane na elfu arobaini).

Namba huwa hazidanganyi. Hapa ndipo hii serikali yetu ya viwanda ilipotufikisha. Mantiki ya gharama hizi mpya haifahamiki vizuri kwa wananchi wengi kama ilivyo kwa makato ya VAT, EWURA na REA. Kwa gharama za ajabuajabu kama hizi, viwanda vitaendeshwaje katika nchi hii? Hapa nimetolea mfano mdogo tu kwa mwekezaji mdogo anayemiliki kiwanda cha saluni ya nywele. Ikiwa hali ndiyo hii kwa wawekezaji wadogo, je wawekezaji wakubwa kama akina Dangote si wataikimbia nchi?

Ifike wakati serikali hii iwaonee huruma wananchi wapatao milioni 65 wanaoishi maisha magumu katika nchi hii. Kampuni za simu zina huruma zaidi kwa wananchi kuliko serikali yao kandamizi inayowakamua fedha bila huruma kila kukicha. Kampuni za simu ziliona ni busara huduma hii itolewe bure lakini serikali hii imeona wanachi wanafaidi sana hadi kufikia uamuzi wa ajabu kuwakamua fedha zaidi bila sababu za msingi. Inauma sana.
Mtoa post ulitaka kutuonyesha bei ya umeme au mgawanyo wa pesa pindi unaponunua umeme. Sijakuelewa naona tu unajenga hoja badala ya kutuonyesha bei za umeme kama zimebadilika kama kichwa cha habari hapo juu. Tujadili mambo muhimu kama.ni siasa sema tukupatie mchango uende wenzio wako Dodoma
 
Watanzania bwana. Kama hutaki kukatwa hiyo % 1.1 nenda kanunue kwenye kibanda cha Tanesco. Unataka mitandao inayokusogezea huduma mkononi ipate wapi faida. Kumbuka zamani mitandao ilikuwa inalipwa commission na Tanesco. Kabla hujalalamika kaa upande wa mfanyabiashara kwanza ndio uanze kumwaga povu
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja pasipo kupepesa macho. Tangu kampuni za simu za mkononi zivumbue njia mpya ya kununua umeme wa LUKU bure kupitia mpesa, tigo pesa, airtel money, etc, ununuzi wa umeme umekuwa rahisi sana. Ununuzi wa umeme unaweza kufanyika muda wowote, iwe usiku au mchana au wakati hali ya hewa inapokuwa mbaya, kwa mfano, wakati wa mvua. Mtu kulala giza wakati una salio kwenye mpesa, tigo pesa au airtel money, ni kujitakia mwenyewe.

Baada ya serikali ya awamu ya tano kugundua kwamba wananchi wanafaidi bure huduma hii ya kununua umeme, ambayo kimsingi serikali haichangii chochote, serikali tukufu ya awamu ya tano, wameamua kuwakamua wananchi bila shuruti na bila sababu zozote za msingi. Mwanzoni huduma hii ilikuwa ikipatikana bure kabisa lakini sasa wananchi wanyonge watahitajika kukamuliwa 1.1% ya gharama za kununua umeme. Hii ni mbali na 18% VAT, 3% REA na 1% EWURA tunazokamuliwa kila kukicha.

Serikali hii inayojinasibu kuwajali wanyonge imeamua, kwa makusudi kabisa, kuwaongezea wanyonge mzigo wa gharama za maisha kwa kuwakamua zaidi fedha kidogo walizobaki nazo mifukoni mwao. Sijawahi kuona serikali yenye roho mbaya kwa wananchi wanyonge kama serikali hii ya awamu ya 5.

Kwa wale ambao hamfahamu mzigo wa 1.1% ya gharama za kununua umeme, itabidi twende taratibu mpaka muelewe. Kwa mfano, mwananchi anayemiliki kiwanda kidogo kama saluni, hutumia umeme usiopungua Tsh 100,000 kwa siku. Hivyo, atalazimika kukamauliwa Tsh 1100 kwa siku, sawa na Tsh 33,000 kwa mwezi = Tsh 396,000 kwa mwaka = Tsh 3,168,000 hadi awamu ya kwanza ya utawala wa serikali ya awamu ya 5 itakapoisha. Ikiwa gharama zitaendelea kubaki kama zilivyo hadi mwaka 2025, mwekezaji huyu wa kiwanda kidogo atakuwa amekamuliwa jumla ya Tsh 15,840,000 (shilingi milioni kumi na tano, laki nane na elfu arobaini).

Namba huwa hazidanganyi. Hapa ndipo hii serikali yetu ya viwanda ilipotufikisha. Mantiki ya gharama hizi mpya haifahamiki vizuri kwa wananchi wengi kama ilivyo kwa makato ya VAT, EWURA na REA. Kwa gharama za ajabuajabu kama hizi, viwanda vitaendeshwaje katika nchi hii? Hapa nimetolea mfano mdogo tu kwa mwekezaji mdogo anayemiliki kiwanda cha saluni ya nywele. Ikiwa hali ndiyo hii kwa wawekezaji wadogo, je wawekezaji wakubwa kama akina Dangote si wataikimbia nchi?

Ifike wakati serikali hii iwaonee huruma wananchi wapatao milioni 65 wanaoishi maisha magumu katika nchi hii. Kampuni za simu zina huruma zaidi kwa wananchi kuliko serikali yao kandamizi inayowakamua fedha bila huruma kila kukicha. Kampuni za simu ziliona ni busara huduma hii itolewe bure lakini serikali hii imeona wanachi wanafaidi sana hadi kufikia uamuzi wa ajabu kuwakamua fedha zaidi bila sababu za msingi. Inauma sana.
Hata huruma ya makampuni ya simu nayo imeisha... Vifurushi vimepunguzwa mno.. Yaani ni kupunwa pesa mwanzo mwisho kuanzia alfajiri mpaka usiku wa manane na manene... Hakuna utakachogusa usiambiwe kodi
 
Waliondoa service charge na Prof. Mhongo, wamezirudisha kwa mlango wa nyuma. Wapuuzi CCM na serikali yao
 
Swali langu ni kwamba, hiyo 1.1% niyanini hasa mteja anachangia? Je niya huduma au vipi ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom