Gharama kiasi gani kulisha kuku 500 wa nyama kwa Dar es Salaam mpaka kuuza?

Hawa kuku challenge yao kubwa ni soko tu, unatakiwa uwe na soko la uhakika ili wiki ya tano kamili wote wanatoka na kwa bei nzuri..

Ila wakifika wiki ya tano ndiyo unaanza kuhangaikia wateja, utalia kwa kilugha chenu..ukizubaa utauza hadi simu kuwanunulia chakula.

Ukiwa na mtaji wa Mil moja kwa kuku 500 inatosha chakukla hadi unawatoa wiki ya 5.
 
kufuga kuku 100 ni 500,000....hivyo 500,000 x 5 = 2,500,000 ....andaa 3,000,000 (500,000 ya dharura yeyote itakayotokea).
 
Hili Banda langu la fully bati Lina miaka 6 ,hiyo picha nimeipiga Sasa hivi ,hao kuku vishingo wapo Mia tano na nilichanganyia na kroiler 10 Kama zawadi.

Kuku 500 wastani wa mfuko Ni 64,500 x 21=
Chanjo huwa nachanganya Newcastle na gomboro nawapa at the same time Mara mbili kila siku Saba za mwanzo.
12,000 * 2 =24,000

Maranda ya mbao kiroba Cha debe 8 sh 4000

Vitamin ya dad is the best 1 x15,000

Glucose pakt 2 sh 2000

Mkaa wa 15,000 kwa siku nne tu

Umeme wa 15,000

Hapo chakula na maji hakikisha kill kuku hafwati mbali na havikauki kwenye vyombo vyao week 4 mzigo unauzika
 
banda sijaliona kiongozi
 
Kupata vifanga imekuwa mtihani mzito ,Kama una connection nanunua kwa 2000 ,

Kama una mashaka nipigie tuelekezane huku jf hatunyimani

0688607473

Picha zinagoma
 
Natumia drinkers za Lita 10 zipo 12 nikiweka maji asbh Hadi kesho yake asbh kupunguza kuingia bandani kila muda

Na chakula nawajazia asbh na jioni nakuja kuongezea na kukagua maendeleo .

It's easy kuwafuga ukishazoea Wala Sina Cha kijana hapa

Ila Nina mradi wa ngombe ,na nguruwe hapa hapa
IMG_20210623_100728_4.jpg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom