Ghana wamefikia default; IMF wamesema watawadhamini. Je, tupo salama kiuchumi huko tuendako?

Midimay

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
2,907
4,771
Habari za jioni wakuu.

Miaka miwili nyuma, Ghana ilikuwa nchi ya mfano katika ukuaji wa uchumi barani Afrika. Bin Vuu, 2022 Ghana ipo katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Ghana inaelekea kwenye default. Ghana ipo katika njia ya Sri Lanka. Inaelekea kushindwa kulipa madeni yake inayodaiwa katika fedha za kigeni.

Chanzo cha mgogoro wanavyosema wao ni kuja kwa Covid-19, rushwa na economic mismangement. Wakati wa Corona 2020, Rais wao alisema tutajua namna ya kurudisha uchumi back to life lakini hatujui namna ya kurudisha maisha ya kibinadamu, akapiga "lock down". Ni kauli nzuri kibinadamu lakini ni kauli mbaya kiuchumi.

Uchumi haudanganyi. Muda umefika, serikali ya Ghana haijui ifanye nini. Taarifa zilizopo ni kwamba IMF wamejitolea kubail out(kuwadhamini katika mikopo yao). Yaani mkopo juu ya mkopo.
Sisi Tanzania tuliweza kuvuka salama wakati wa "lockdown" duniani kwa ukakamavu na ushujaa wa serikali iliyokuwa madarakani.

Baada ya kuvuka serikali ikabadilika. Serikali iliyoingia ikaanza kwa kasi kukopa mikopo isiyokwenda kwenye miradi ya uzalishaji. Mikopo kwa ajili ya utoaji wa huduma za jamii.

Tunahitaji huduma za jamii lakini huo ni mtego. Kama raia mwema, najiuliza maswali yafuatayo;
1. Tutapata wapi dola za kulipa madeni itokanayo na mikopo hiyo?
2. Je, tutaendelea kukopa ili kupata dola za kulipia madeni hayo?
3. Tuna mkakati gani wa kupata dola zaidi huko tuendako?
4. Je, tuna bidhaa za kuuza nje kwa kiwango cha kupata dola za kulipa madeni?
5. Kwanini serikali haiweki tena nguvu katika miradi ya import substitution?
6. Tutaepukaje matumizi makubwa ya dola katika importation ya bidhaa bila kusisitiza manufacturing ndani ya nchi? Slogan ya nchi ya viwanda imepotelea wapi?
7. Je, tupo salama huko tuendako au na sisi tutafikia default?
8. Nani anawajibika kuitahadharisha serikali katika kasi yake ya kukopa?
9. Je, export zetu zinaongezeka mwaka hadi mwaka ili tuweze kulipa madeni bila kudefault katika siku zijazo?

Tujifunze kwa wenzetu Sri Lanka na Ghana ambao wamefikia default. Hata Pakistan wanaelekea huko.
Nchi zote hizo yaani Sri Lanka, Ghana na Pakistan zina chumi kubwa yaani GDP kuliko Tanzania na zimefikia hapo kwa sababu ya economic mismanagement, rushwa na ufisadi na kuiga iga hasa katika swala la UVIKO-19.

Ni mpumbavu pekee anayefanya sherehe kusherehekea serikali yetu inapokopa bila kujali tutairudishaje mikopo hiyo, na hata tukikopa, Je, fedha hizo zinatumika sehemu iliyolengwa? Au zinaingia midomoni mwa walamba asali?

Hatuwezi kuwa nchi ya wakopaji na wakati tuna kila kitu!!
 
Habari za jioni wakuu.
Miaka miwili nyuma, Ghana ilikuwa nchi ya mfano katika ukuaji wa uchumi barani Africa.
Bin Vuu, 2022 Ghana ipo katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi.
Ghana inaelekea kwenye default. Ghana ipo katika njia ya Sri Lanka. Inaelekea kushindwa kulipa madeni yake inayodaiwa katika fedha za kigeni.
Chanzo cha mgogoro wanavyosema wao ni kuja kwa Covid-19, rushwa na economic mismangement.
Wakati wa Corona 2020, Rais wao alisema tutajua namna ya kurudisha uchumi back to life lakini hatujui namna ya kurudisha maisha ya kibinadamu, akapiga "lock down". Ni kauli nzuri kibinadamu lakini ni kauli mbaya kiuchumi.

Tutauza Mlima Kilimanjaro
 
Tuendako kwa huu mfumuko wa bei, kunatia mashaka mengi,
Wanatuongoza inabidi waje na hatua makini za kukabiliana na hii hali,
Natumaini tunaweza kuvuka hiki kikwazo,
 
Ni mpumbavu pekee anayefanya sherehe kusherehekea serikali yetu inapokopa bila kujali tutairudishaje mikopo hiyo, na hata tukikopa, Je, fedha hizo zinatumika sehemu iliyolengwa? Au zinaingia midomoni mwa walamba asali?

Hatuwezi kuwa nchi ya wakopaji na wakati tuna kila kitu!!
Uvccm wanataka sa100 aendelee kukopa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kilimo cha bhangi, opium, mirungi na coke kiruhusiwe na mapato yake yakalipe madini. Ardhi yetu ina rutuba sana na ndani ya muda mfupi tutakuwa hatudaiwi.
 
Unataka Tanzania iwe "narco state" unajua madhara yake lakini? Mexico wanachinjana kama wanyama, kule Colombia miaka ya 80s na 90s walichinjana sana kwa sababu za hayo madude.
 
Back
Top Bottom