GHANA: Jamaa wachukua mwili wakati ukitaka kuzikwa kisa deni la chumba cha kuhifadhia maiti

Kweli usukuman kabisa ufanye ujinga kama huu hiyo kitu haiwezekani aisee mikoma lazima itumike wamwise
Tena siyo mikoma tu had mbasa na magembe yatatumika

hahahahah! yaya ekishimbe gete!!
 
Hamna kitu hapo, hebu fuata mwili wa jamaa yako mochwari halafu ugome kutoa hela ya maji kwa wadau wa pale ndani uone shughuli yake, yaani mwili watauburuza buruza hadi utakoma. Wale wahudumu wa mochwari yaani bangi ishakolea.
 
882c22882eb66f75d3882b199ad60579.jpg
Kizaazaa kilitokea wakati wahudumu katika makaburi walitoa mwili katika jeneza na 'kuuteka nyara' kwasababu ya deni

Kisa hicho cha kushtua kilitokea Accra, Ghana. Iliripotiwa kuwa familia ya marehemu walishindwa kuwalipa wahudumu hao wa chumba cha kuhifadhia maiti waliodai familia hiyo Sh3,000 za Ghana

Kisa kilianza wakati wanaume wawili wamesimama juu ya jeneza huku mamia ya watu wakiwa wamesimama kutazama kisa hicho

Wahudumu hao wenye ghadhabu waliwapigia kelele umati huo huku wakiendelea kuutoa mwili huo katika jeneza

Muda mfupi baadaye, wanaume hao wanaonekana wakibeba mwili huo mabegani! Baadhi ya watazamaji wanajaribu kuongea na wanaume hao ambao kwa hasira wanatumia mwili huo kuwaashiria watu kuondoka
37c92e6daf4ef2fe2fa1751a09f69116.jpg
Wanaume hao waliondoka nao kabisa bila kujutia hatua yao hiyo. Haikujulikana ikiwa marehemu alizikwa na hao wanaume au waliendelea kumshikilia kwa kutaka kulipwa.

Chanzo: TaifaLeo
Kwenye hayo mazishi hapakuwa na wanaume otherwise hao 2 wasingebeba mwili
 
Maongengezeko ya maasi,chuki,fitina,visasi n.k, dunia inazidi kuleemewa na mzigo wa maasi.Ni ishara mbaya za mwisho wa hii dunia.marehemu kakosa nn hata atendewe hivyo!!?? binadamu wakati mwingine ni wabaya mno.ni heri ukutane na Simba nyikani,kuliko binadamu wa namna hii.
 
Back
Top Bottom