Ghadhabu ya Mungu; Yesu anaendelea kufundisha

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
.ExternalClass .ecxhmmessage P{padding:0px;}.ExternalClass body.ecxhmmessage{font-size:10pt;font-family:Verdana;} Alikuwepo kuhudhuria sherehe za Passover Jerusalem Myahudi mmoja tajiri kutoka Crete,na akafika kwa Andrew kuomba kuonana na Yesu faragha. Andrew akaupanga huu mkutano wa siri katika nyumba ya Flavius jioni ya siku ya pili. Huyu mtu hakuweza kuyaelewa mafundisho ya Mwalimu,na alikuja kwa vile alikuwa ana hamu ya kupata maelezo zaidi kuhusu ufalme wa Mungu. Akasema Yakobo kwa Yesu,''Lakini,Rabbi,Mose na manabii wa zamani wanatuambia kwamba Yahweh ni Mungu mwenye wivu,ni Mungu mwenye ghadabu kubwa na hasira sana. Manabii wanasema anawachukia watenda uovu na analipizia kisasi kwa wale ambao hawaitii sheria yake. Wewe na mitume wako mnatufundisha kwamba Mungu ni Baba mpole na mwenye huruma,ambaye anawapenda watu wote kiasi kwamba anataka kuwakaribisha kwenye huu ufalme wa mbinguni,ambao mnasema upo karibu sana.''

Yakobo alipomaliza kuzungumza,Yesu akajibu;''Yakobo,umeelezea vizuri sana mafundisho ya manabii wa zamani waliowafundisha watoto wa vizazi vyao kulingana na mwangaza wa siku zile. Baba yetu wa Paradiso habadiliki. Lakini dhana[concept] ya jinsi alivyo imepanuka na kukua toka siku za Mose mpaka siku za Amos mpaka siku za nabii Isaya.Na sasa nimekuja katika mwili kumfunua Baba katika utukufu mpya na kuonyesha kwa wote upendo na huruma zake kwa watu wote na dunia zote. Injili ya ufalme huu itakapoenea duniani na mafundisho yake ya kutaka watu wawe na furaha na nia njema kwa watu wote,kutakuwa na mahusiano mazuri zaidi miongoni mwa familia za mataifa yote. Muda utakavyozidi kwenda,baba na watoto wao watapendana zaidi,na itaeleweka vizuri zaidi kuhusu upendo wa Baba mbinguni. Kumbuka,Yakobo,baba mzuri wa kweli siyo tu anaipenda familia yake kwa jumla-kama familia-lakini pia anampenda kwa dhati na kwa hakika kila mmoja wao.

Baada ya majadiliano marefu kuhsu tabia[character] ya Baba wa mbinguni,Yesu akatua kidogo na kusema,''Wewe ,Yakobo,ukiwa kama ni baba wa wengi,unafahamu fika ukweli wa maneno yangu.'' Na Yakobo akasema,;Lakini,Mwalimu,nani amekuambia kwamba mimi ni baba wa watoto sita? Umefahamu vipi hili kuhusu mimi?'' Na Mwalimu akajibu;''Inatosha tu kusema kwamba Baba na Mwana wanajua mambo yote,kwa sababu,kwa hakika,wanaona yote. Kwa vile unawapenda watoto wako kama baba duniani,lazima sasa ukubali kwamba ukweli wa upendo wa Baba wa mbinguni kwako wewe-siyo tu kwa watoto wote wa Abrahamu,lakini kwa roho yako .''

Halafu Yesu akaendelea kusema,''Wakati watoto wako ni wadogo na wana tabia za kitoto,na ikibidi uwaadhibu,wanaweza kufiria kwamba baba ana hasira na ghadhabu na tabia za kulipiza kisasi. Hii tabia yao ya kitoto inawazuia kuipenya ile adhabu,kuelewa kuwa baba anaona mbali na anataka kufanya marekebisho kwa upendo wake. Lakini kama watoto hawa hawa wamekua,na kuwa wanaume au wanawake wakubwa,haitakuwa ujinga kushikilia maoni ya awali na yaliyopotoka kuhusu baba yao? Wakishakuwa wakubwa sasa lazima wauone upendo wa baba katika hizi nidhamu za awali. Haipaswi pia kwa binadamu,karne zinapopita aelewe vizuri zaidi maumbile ya kweli ya tabia upendo ya Mungu ?. Unafaidika nini na mafundisho ya kiroho ya vizazi baada ya vizazi iwapo utang'ang'ania kumuelewa Mungu kama Mose na manabii walivyomuona? Nakwambia,Yakobo,katika mwangaza mkubwa wa saa hii umtazame Baba sio kama wale wa zamani walivyomuona. Na ukimtazama namna hiyo,utafurahi na kuingia katika ufalme ambao Baba huyu mwenye huruma anatawala,utajitahidi utashi wake wa upendo uongoze maisha yako kuanzia hapo''

Na Yakobo akajibu,''Rabbi,naamini,nina hamu uniongoze katika ufalme wa Baba.''
 
Back
Top Bottom