My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,293
Wanadamu tuna kawaida ya kuishi duniani kwa raha na kwa dhiki pia, lakini kila tupatapo dhiki huwa tunajiridhisha kuwa huo ni mpango wa Mungu na hata tukifiwa huwa tunasema ni mpango wa MUNGU, huwa hatutathimini kwa kina, je? Kila jambo kwetu ni mpango wa Mungu?
Na kama kila jambo kwetu ni mpango wa Mungu, je? Shetani huwa hana mipango? Ina maana kila zuri na baya yote ni ya Mungu tu? Shetani kazi zake kwetu ni zipi?
Watanzania Kwa Muda mrefu sana tumekuwa tukiishi maisha ya kinafiki kupindukia yasiyompendezesha Mungu, si raia wala Viongozi wa dini wala serikali, sote tumekuwa tukimkosea sana MUNGU kwa unafiki uliotukuka, kila uchaguzi unapofika, Viongozi wa dini huwaaminisha waumini wao kuwa Rais aliyepatikana ni chaguo la Mungu.
Na waumini nao kwa sababu tu wameshiba na wana uhakika wa kula na kulala huwa wanakubaliana kuwa ni kweli kabisa huyo Rais ni chaguo la Mungu.
Mungu si mwanadamu, njia zake siyo njia za mwanadamu, mawazo yake si mawazo ya mwanadamu, ni Mungu tu, na Mungu ni mtakatifu kupindukia, ana huruma sana na ni mwingi wa rehema, ndo maana tunamtenda dhambi lakini anaturehemu tu na kutupatia Muda mwingi wa kutubu dhambi zetu.
Mungu hapendi kutajwa hovyo na kuhusishwa na mambo asiyohusika. Ndo maana anakaa mbali na taifa hili la Tanzania kwa sababu ya unafiki wetu. Hebu jiulize hao hao wafanyakazi 9,932 waliofukuzwa kazi, 73% walikuwa wakisema tumepata chaguo la Mungu, bila ya kuwa na ushahidi kuwa kweli tuna kiongozi chaguo la Mungu.
Na wafanyakazi hao hao wametumika sana kuibeba CCM na hata viongozi wa TUCTA wengi sana ni makada wa CCM, chama kilichokaa madarakani miaka 60 na bado kila kitu hakiendi utadhani ndo nchi imepata Uhuru leo. Leo wafanyakazi wanalia, familia zao zinalia, ndugu zao wanalia, wafanyakazi 9,932 ni blockchain ya watu zaidi ya 250,000 nyuma yao waliopata maumivu na stress nzito maishani mwao.
Naam, ghadhabu ya Mungu imewaka juu yao na bado inaendelea kuwaka juu ya wengine. Kibinadamu kabisa na kiongozi mwenye hofu ya kweli ya Mungu, huwezi kufukuza kazi watu 9,932 kikatili hivyo na wasipate hata mafao yao hata kama wana makosa, huyo aliyeidhinisha hao watu wafukuzwe yeye ana usafi gani?
Kwanini amekuwa mtu wa kubeza tu na kudharau kila kilichofanywa na watangulizi wake? Hii ni ghadhabu ya Mungu juu yetu watanzania, tuache unafiki, hili pigo wamelia malaki ya watu, unajiuliza, wataenda wapi na hali ya nchi ilivyo ngumu kiasi hiki? Mbaya zaidi wamekaa kazini zaidi ya miaka 30 eti hata mafao hakuna kuchukua, wanaenda kuishi vipi mitaani? Chaguo la Mungu anaweza kuwa katili kiasi hicho?
Ole wako Tanzania umemwasi Mungu wako, na ghadhabu ya Mungu i juu yako.