Geza ulole yaja kwa mtindo wa kumba kumba

niah

R I P
Sep 26, 2015
7,019
9,291
Nimemsikiliza kaka wa kaya leo wakati anaapisha wakuu wa mikoa, kuna uzi already upo kuhusu hii isue ila nimeona nifungue wangu kuwakumbusha kuhusu Geza ulole mama Geza ulole mama weeeee? Mnaukumbuka huu wimbo? Viazi na karanga na kila kitu tutalima huko! Watakapopelekwa wacheza pool.

Swali, tulipokuwa tunaanzisha Azimio la Arusha 1967, sisi tuliokuwa shuleni tulianzisha mashamba ya mfano kila shule. Tulikuwa na mashamba ya migomba, kahawa, pamba, korosho, karanga na tuliletewa wataalamu wa kutuelimisha.

Tulipomaliza la saba tulitengwa waliofaulu vizuri labda wawili au watatu walienda sekondari, wanne domestic science colleges, watano nursing schools, National service kwa wale walioomba, vyuo vya ufundi, usista.

Tuliweza kuwa na skills sababu tulifundishwa upishi, uashi, kutengeneza vyungu, kuchonga, kuchora na tuliuza hivi vitu wakati wa open day. Wazazi waliona fahari kuona watoto wao wanatengeneza kamba kutumia katani (za kufungia mbuzi/ng'ombe). Viko wapi sasa?

Mtoto anamaliza la saba hana skill yoyote, hawezi hata kupika mchicha kitu ambacho tulifundishwa. Hawezi kuchonga mpini wa jembe, hajui kina cha mgomba ni futi ngapi? na bado ni mtoto ambaye hawezi hata kukaanga yai! Elimu elimu elimu. Mnaijua elimu nyie????

Watu tulikuwa tunafunga chakula kila siku kwenda shule. Bila chakula husomi. Lazima ule saa sita na lazima kushare au mle kwenye group kwa wale maday. Boarders ni kwenye bwaro. Chakula tulikuwa tunalipia lakini uzuri kulikuwa na vyama vya ushirika vina subsidize 75% hivyo unakuta mzazi yeyote alimudu.

Tulicheza mpaka kwenye mashindano ya taifa, tukawakilisha mikoa yetu na bado tukafanya vizuri kwenye masomo. Watu walipata schollaships sababu ya michezo iko wapi sasa na ni nchi hii huru ambayo sasa siyo changa tena.

Kama tuliweza miaka ya 60s na 70s even early 80s kwanini baada ya Mwalimu kuondoka madarakani kila kitu kiliisha. Mwalimu aliondoka na kasma madarakani au aliondoka na akili za watu wote aliowaongoza? Machozi yangu yanapitia kwenye vidole basi tu.
 
lazima machozi yakulengelenge ukikumbuka hayo!
Hayo yalikosa nguvu hasa wakati wa Mwinyi! Mwinyi hakujali misingi uongozi na pia hakuwa mawazo yeyote kuhusu uchumi wa mbeleni

Viwanda alivimaliza
 
Back
Top Bottom