Getrude Ndibalema, Dickson Kibona watimuliwa uanachama na BAVICHA kwa ‘Uasi’

pepsin

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
3,465
6,109
CCM hawajui timing kabisaaa. Kumrudisha pandikizi wao aliyekuwa kiongozi BAVICHA mapema ni uono mfupi.
Sasa Maasai na rungu lake!!

==========

Arusha. Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama watatu wa chama hicho.

Waliofutwa uanachana ni pamoja na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara,Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Kilimanjaro, Dickson Kibona.

Akizungumza leo Mei 21, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha, Ole Sosopi amesema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kufuata taratibu zote za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa.

Amesema viongozi hao wamehojiwa baada ya kuwepo tuhuma za usaliti ambalo ni kosa kubwa kwenye chama hicho.

Sosopi amesema Bavicha imeridhia kuwaondoa wanachama hao baada ya kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.
 
C CM hawajui timing kabisaaa. Kumrudisha pandikizi wao aliyekuwa kiongozi BAVICHA mapema ni uono mfupi.
Sasa Maasai na rungu lake!!

Arusha. Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la
Chadema, Patrick Ole Sosopi, ametangaza
kuwafuta uanachama wanachama watatu
wa chama hicho.
Waliofutwa uanachana ni pamoja na
aliyekua Naibu Katibu Mkuu Bara,
Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa
Bavicha mkoa wa Kilimanjaro, Dickson
Kibona.
Akizungumza leo Mei 22, katika mkutano
na waandishi wa habari jijini Arusha, Ole
Sosopi amesema kwamba uamuzi huo
umekuja baada ya kufuata taratibu zote
za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa.
Amesema viongozi hao wamehojiwa
baada ya kuwepo tuhuma za usaliti
ambalo ni kosa kubwa kwenye chama
hicho.
Sosopi amesema Bavicha imeridhia
kuwaondoa wanachama hao baada ya
kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.
Masai na RUNGU MKONONI
 
C CM hawajui timing kabisaaa. Kumrudisha pandikizi wao aliyekuwa kiongozi BAVICHA mapema ni uono mfupi.
Sasa Maasai na rungu lake!!

Arusha. Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la
Chadema, Patrick Ole Sosopi, ametangaza
kuwafuta uanachama wanachama watatu
wa chama hicho.
Waliofutwa uanachana ni pamoja na
aliyekua Naibu Katibu Mkuu Bara,
Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa
Bavicha mkoa wa Kilimanjaro, Dickson
Kibona.
Akizungumza leo Mei 22, katika mkutano
na waandishi wa habari jijini Arusha, Ole
Sosopi amesema kwamba uamuzi huo
umekuja baada ya kufuata taratibu zote
za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa.
Amesema viongozi hao wamehojiwa
baada ya kuwepo tuhuma za usaliti
ambalo ni kosa kubwa kwenye chama
hicho.
Sosopi amesema Bavicha imeridhia
kuwaondoa wanachama hao baada ya
kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.

May 22 mwaka gani huu?
 
Baraza kuu la Vijana Chadema taifa limewafukuza uanachama wanachama Getrude Ndibalema aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo na Dickson kibona aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro kwa kosa la usaliti ndani ya chama.

Akiongea na wanahabari Patric Ole Sosopi, Mwenyekiti wa baraza hilo amesema kuwa wamefikia hatua ya kuwafukuza uanachama watu hao baada ya uchunguzi kufanyika na kubainisha kuwa wana makosa ya usaliti ambapo hivyo kuanzia leo Mei 21 sio wanachama wala Viongozi wa chama hicho.

Ameeleza kuwa pia baraza hilo limemchagua Baraka Mfilinge Mwenyekiti wa baraza hilo Mkoa wa Iringa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo.

Amesema wametafakari hali ya kisiasa nchini na wameweza kugundua kuwa kuna mkwamo wa demokrasia hapa nchini..

Pia wamelitaka Jeshi la Polisi kujitokeza hadharani na kutangaza kuwa wameshindwa kuwakamata watu waliofanya tukio la kumpiga Mbunge Tundu Lissu na waruhusu vyombo vya uchunguzi vya kimataifa kufanya kazi hiyo.
 
Back
Top Bottom