Getrude Mongella: Ni heri kumpigia kura mgombea mwanaume kuliko mwanamke anayeona aibu kuzungumzia matatizo na maendeleo ya wanawake

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Mongella.jpg

BALOZI Getruda Mongela, amesema ni heri kumpigia kura mgombea mwanaume katika chaguzi mbalimbali kuliko mwanamke anayeona aibu kuzungumzia matatizo na maendeleo ya wanawake.

Akizungumza jana katika mkutano uliowakutanisha viongozi wanawake nchini, Balozi Mongela alisema siku ambayo Bunge litafikia kuwa asilimia 50 ya wanawake hatajali mbunge ametoka chama gani.

Alisema isipokuwa atajali kama mambo wanayozungumza wanawake nchini anayajua na kuyapenda.

“Kama mwanamke yoyote anaingia bungeni akiwa kama ameenda katika maonyesho ya Sabasaba ni heri nimpigie (kura) mwanaume. Ni hasara kuwa na wanawake viongozi wanaoona aibu kuzungumza maendeleo ya wanawake,” alisema.

Alihoji kama wabunge wanawake wanaangalia bajeti ya Serikali ambayo nyingi inaingia katika ujenzi na ni ngapi ambazo zinawafikia wanawake kule vijijini.

“Tunafanya nini fedha nyingi ambazo na wakinamama wamezihangaikia zinafika hadi mikononi mwa wanawake. Na tunatafuta wapi hizo rasilimali?”alihoji.

Naye, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini, Hodan Addou alisema kuwa leo Mtandao wa Wanawake Afrika tawi la Tanzania, utazinduliwa ukiwa na malengo mbalimbali ikiwemo kuwahimiza wanawake na viongozi wanawake kutimiza majukumu yao katika kuibadilisha Afrika.

Alitaja lingine ni kuhamasisha majadiliao ili kupitia viongozi kuhusu mambo yanayowasumbua wanawake barani Afrika.

“Kuwasaidia wanawake viongozi wa kisiasa na wa bara, taifa na ngazi za chini kuweza kutimiza malengo yao ya uongozi,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mweza wa Mtandao huo, Mary Rusimbi alisema uwepo wao katika mkutano huo unalenga katika kujiangalia, kujitathimini, kujitafakari uongozi wa mwanamke uliko.
 
Blah blah tu...mmekaa uongozini miaka dahali bado wajawazito wanahangaika hawapati huduma stahiki..piteni hv
 
mbenge, Wabunge wa viti maalum ni pasua kichwa kwa sababu mchakato na utaratibu wa kuwateua unawadharilisha wanawake wenyewe na kupunguza nguvu za kupigania haki.

Balozi Mongella naye anakwaa kisiki kwa hoja ya kuwataka wanawake viongozi kutetea haki za wanawake. Hoja hiyo inapingana na itikadi ya chama chake kuwa "binadamu wote ni sawa".
 
Back
Top Bottom