Gesi yetu ya Mtwara bado ipo?

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,453
Nauliza ili pia wengine wajue. Hivi ile Gesi yetu ya katika kampeni bado ipo au imekauka? Kama ipo, kwa nini tunahangaika na bakuli wakati tuliahidiwa neema wakati wa kampeni?

Kama kuna anayejua ukweli wa hii gesi tunaomba atusaidie majibu kwa sababu nijuavyo mimi, mara ya mwisho Mwijage alipeleka hoja ya muswada wa dharura bungeni kuhusu hii gesi, sasa sijui labda iliondoka na muswada ule wa dharura !,
 
Mosi, kuna gas za aina mbili: Gas ambayo imegundulika miaka kadhaa iliyopita na Gas Boom!!

Gas iliyogunduliwa miaka kadhaa iliyopita ni kama ile ya Songosongo Lindi na Mnazi Bay!! Kwa ujumla wake, hiki ni kiasi kidogo sana cha gas na tayari imeshachimbwa! Na ndio hii ambayo imejengewa bomba kutoka Mtwara na Songosongo na kubisha hodi Ubungo!!

Gas Boom kwa kiasi kikubwa ipo deep sea na nyingi ya hii ipo kwenye pwani ya Lindi ingawaje inasifika sana Mtwara! Hii bado haijachimbwa kabisa! Na haitaanza leo wala kesho!

Hii ndio ile gas inayokusudiwa kujengewa Plant pale Lindi itakayoghrimu $30 million (kama kumbukumbu zangu zipo sawa) na ndio gas ambayo inashawishi upanuzi wa bandari ya Mtwara!!!

Remember, wawekezaji walitaka hii plant iwe huko huko deep sea lakini serikali ikakataa kwahiyo ujenzi wa pale Lindi ni kwa shingo upande na ndio maana sishangai kuona kusua sua kwingi!!

Kwa hii gas boom, tumewahi sana labda senti yake tutaanza kuiona kuanzia 2022 hadi 2025 hapa katikati!!! Lakini tukienda na mpango wa ku-abuse sekta binafsi, usishangae ikafika 2030 haijachimbwa hata tone!!!
 
Suala la Gas bado halijaeleweka na wengi!

Mosi, kuna gas za aina mbili: Gas ambayo imegundulika miaka kadhaa iliyopita na Gas Boom!!

Gas iliyogunduliwa miaka kadhaa iliyopita ni kama ile ya Songosongo Lindi na Mnazi Bay!! Kwa ujumla wake, hiki ni kiasi kidogo sana cha gas na tayari imeshachimbwa! Na ndio hii ambayo imejengewa bomba kutoka Mtwara na Songosongo na kubisha hodi Ubungo!!

Gas Boom kwa kiasi kikubwa ipo deep sea na nyingi ya hii ipo kwenye pwani ya Lindi ingawaje inasifika Mtwara! Hii bado haijachimbwa kabisa! Na haitaanza leo wala kesho!

Tumewahi sana labda senti yake tutaanza kuiona kuanzia 2022 hadi 2025 hapa katikati!!! Lakini tukienda na mpango wa ku-abuse sekta binafsi, usishangae ikafika 2030 haijachimbwa hata tone!!!
Sawa mkuu, kwa hiyo yale maneno ya kwenye kampeni yalikuwa ni ya uongo? Sababu walituambia mpaka 2020 tanzania tutakuwa na uchumi wa Kati kupitia Gesi
 
Sawa mkuu, kwa hiyo yale maneno ya kwenye kampeni yalikuwa ni ya uongo? Sababu walituambia mpaka 2020 tanzania tutakuwa na uchumi wa Kati kupitia Gesi
Mkuu gesi imekumbwa na mambo mengi na sio Tanzania tu kuna issue ya BEI YA GESI katika soko la dunia iko chini so kampuni nyingi zimerudi nyuma kuwekeza na kuendeleza hii rasilimali ukizingatia gesi tuliyonayo inategemea kuuzwa nje ya nchi.
 
Sawa mkuu, kwa hiyo yale maneno ya kwenye kampeni yalikuwa ni ya uongo? Sababu walituambia mpaka 2020 tanzania tutakuwa na uchumi wa Kati kupitia Gesi
Kama kuna mwanasiasa yeyote ambae alisema by 2020 basi ulikuwa ni uongo wa wazi tena wa bila aibu!
 
Sawa mkuu, kwa hiyo yale maneno ya kwenye kampeni yalikuwa ni ya uongo? Sababu walituambia mpaka 2020 tanzania tutakuwa na uchumi wa Kati kupitia Gesi
Usimuamini mwanasiasa %100 hasa wa ccm
 
Mkuu gesi imekumbwa na mambo mengi na sio Tanzania tu kuna issue ya BEI YA GESI katika soko la dunia iko chini so kampuni nyingi zimerudi nyuma kuwekeza na kuendeleza hii rasilimali ukizingatia gesi tuliyonayo inategemea kuuzwa nje ya nchi.
Sasa tutafanyaje ili Uchumi wetu usonge mbele mkuu, maana sasa hivi naona kila kukicha bora ya Jana.
 
Sasa tutafanyaje ili Uchumi wetu usonge mbele mkuu, maana sasa hivi naona kila kukicha bora ya Jana.
Hapa mkuu panahitajika wanauchumi na watalaam wakae waisaidie nchi kuliko wanasiasa na manabii
 
Hapa mkuu panahitajika wanauchumi na watalaam wakae waisaidie nchi kuliko wanasiasa na manabii
Mkuu hata ile bandari tuliyokuwa tunategemea nayo ni hoi, Ee Mungu Tusaidie,
 
Amen.

Ila Mkuu nakuona umekata tamaa na Tz yetu
Sasa mkuu hata wewe utaacha kukata tamaa, sawa kweli kusoma hujui lakini hata picha huoni?. Mkuu kwa kusema tu ukweli hali ya uchumi wetu ni Taabani, pesa yoote inayokusanywa na Serikali inatosha tu kulipa madeni na inayobaki haitoshi hata kulipa mishahara, Serikali kwa sasa miradi yake yote imeamua Kuifanya yenyewe. Hakuna hata tenda moja imetoka. Sasa mkuu hapo wewe Kama una akili, utaacha kukata Tamaa?
 
Major sema gesi yao na madini yao...sisi tuna gesi faida yake ipo wapi
Mkuu, kwa kweli tunakoelekea siko kabisa, na sijui nani atakuja kutuokoa. Yule mshua wetu wa Msoga naye ndiyo katuacha mazima! EE Mungu Utuhurumie.
 
Nauliza ili pia wengine wajue. Hivi ile Gesi yetu ya katika kampeni bado ipo au imekauka? Kama ipo, kwa nini tunahangaika na bakuli wakati tuliahidiwa neema wakati wa kampeni?

Kama kuna anayejua ukweli wa hii gesi tunaomba atusaidie majibu kwa sababu nijuavyo mimi, mara ya mwisho Mwijage alipeleka hoja ya muswada wa dharura bungeni kuhusu hii gesi, sasa sijui labda iliondoka na muswada ule wa dharura !,
Gesi ni moja ya madudu ya nchi hii ambayo ukiyasikia,MASIKIO YATAKUWASHA NA TUMBO KU UMA.
 
Gesi ni moja ya madudu ya nchi hii ambayo ukiyasikia,MASIKIO YATAKUWASHA NA TUMBO KU UMA.[/QUOTE Ah, mkuu Mimi huwa nasikiaga kizungu zungu kabisa, ila niaamini ktk nchi hii kuna watu wana tamaa iliyozidi kipimo, Ila kuna kauli moja aliwahi kuongea mkuu wetu huyu kwamba, Sintafukua Makaburi. Hii kauli mpaka Leo imeniletea matatizo ya Tumbo
 
Back
Top Bottom