Gesi ya Songosongo kutoka Lindi ilishaisha?

TIASSA

JF-Expert Member
Jun 17, 2014
2,893
3,423
Habari wakuu,

Naomba kuuliza gesi ya Songosongo ya tokea enzi za Mwalimu.

1. Iliishia wapi? Mbona sikuwahi kusikia hata siku moja ikiongelewa?
2. Hii gesi ilikuwa ikitumikaje?
3. Je, gesi ya Songo Songo na ya Mtwara zinatofauti gani.? Kwa maana ya aina ya gesi.

Asante.
 
Ndo inatumika songas, pale ubungo! Hii ya kinyerezi ndo mpya, bomba linauwezo wa kuzalusha 3000Megawatt ila kwa ss linalisha mitambo yenye kuzalisha 150Megawatt ila by end of 2016 litakuwa linalisha mitambo yenye kuzalisha 1500Megawatt
 
Hata ubungo bomba jipya limeishafika coz la songas ni dogo gesi haitoshi kulisha mitambo yote
 
Gesi ya songo songo ilianza uzalishaji wakati wa raisi mkapa ,pan African energy kampuni inayomiliki kwa ubia na serikali wanafanyia ukarabati visima vinavyozalisha hiyo gesi ndiyo sababu wamesimamisha uzalishaji wake.
Tanzania viongozi wakiwa wabunifu wakiacha ubinafsi wakawa wazalendo nchi inaweza kuuza umeme kenya,Uganda,Burundi,Rwanda,Congo,Zambia,Zimbabwe,Sudan ya kusini kwa bei nafuu kwani umeme WA gesi Ni rahisi kuliko WA maji.
 
Gesi ya Songosongo bado ipo na inaendelea kufanya kazi. Tatizo lililotokea mwanzoni ni kwamba walijenga bomba dogo sana. Kwa hali hiyo, gesi iliyokuwa inazalishwa Songosongo na kupelekwa Dar es Salaam ilikuwa haitoshelezi mahitaji ya mitambo yote ya gesi. Gesi hiyo ilikuwa inatumika pale Ubungo kwenye mitambo ya Songas pamoja na kule Tegeta kwenye mitambo ya IPTL almaarufu mitambo ya ESCROW.

Baada ya kugundulika kwa gesi ya Mtwara na uamuzi wa serikali kujenga bomba kubwa hadi Kinyerezi Dar es Salaam, bomba hilo lina matawi mawili. Tawi la kwanza linatoka Madimba Mtwara hadi Nangurukuru. Tawi la pili linatoka Songosongo hadi Nangurukuru. Pale Nangurukuru mabomba ya kutoka Songosongo na Mtwara yameunganishwa kwenye line moja. Hii ni kusema kuwa vyanzo vyote vya gesi yaani Songosongo na Madimba vimeunganishwa kwenye njia moja na hivyo kuwa na kiwango kikubwa cha gesi.

In short, gesi ya Songosongo bado ipo na inaendelea kuzalishwa na inatumika sambamba na gesi ya Mtwara. Pitia mradi wa ujenzi wa bomba la gesi utaelewa
 
gesi ya songosongo upembuzi wake ulikua si makini, walakini unaonekana wazi. rasilimali nyingi imetumika kwa matokeo madogo kama kuna mgombea anayeliona hili na kuahidi kuwashughulikia wahusika atapata kura yangu bure!
 
Habari wakuu,

Naomba kuuliza gesi ya Songosongo ya tokea enzi za Mwalimu.

1. Iliishia wapi? Mbona sikuwahi kusikia hata siku moja ikiongelewa?
2. Hii gesi ilikuwa ikitumikaje?
3. Je, gesi ya Songo Songo na ya Mtwara zinatofauti gani.? Kwa maana ya aina ya gesi.

Asante.

Hiyo gesi sio mali ya serikali tena.
Wameuziwa wachina.
Kwahiyo huna haki ya kuuliza.
 
Gesi ya Songosongo bado ipo na inaendelea kufanya kazi. Tatizo lililotokea mwanzoni ni kwamba walijenga bomba dogo sana. Kwa hali hiyo, gesi iliyokuwa inazalishwa Songosongo na kupelekwa Dar es Salaam ilikuwa haitoshelezi mahitaji ya mitambo yote ya gesi. Gesi hiyo ilikuwa inatumika pale Ubungo kwenye mitambo ya Songas pamoja na kule Tegeta kwenye mitambo ya IPTL almaarufu mitambo ya ESCROW.

Baada ya kugundulika kwa gesi ya Mtwara na uamuzi wa serikali kujenga bomba kubwa hadi Kinyerezi Dar es Salaam, bomba hilo lina matawi mawili. Tawi la kwanza linatoka Madimba Mtwara hadi Nangurukuru. Tawi la pili linatoka Songosongo hadi Nangurukuru. Pale Nangurukuru mabomba ya kutoka Songosongo na Mtwara yameunganishwa kwenye line moja. Hii ni kusema kuwa vyanzo vyote vya gesi yaani Songosongo na Madimba vimeunganishwa kwenye njia moja na hivyo kuwa na kiwango kikubwa cha gesi.

In short, gesi ya Songosongo bado ipo na inaendelea kuzalishwa na inatumika sambamba na gesi ya Mtwara. Pitia mradi wa ujenzi wa bomba la gesi utaelewa

Si kweli. Mabomba hayajaunganishwa. Kila bomba limekuja hadi dar es salaam kivyake. Ila lile la mnazibay limekuja hadi somanga fungo kilichofanyika ni kwamba kuanzia somanga fungo mabomba yote yamepita kati njia moja. Namaanisha on the same way leave. Lakini kamwe hajaunganishwa.
 
Ingebaki ardhin tu hakuna cha maana wala faida hii gesi imetuletea kwanza imetuzidishia umaskin. Na kama kuna faida yeyote bas naomba yeyote ajitokeze na kuorodhesha kama cjamtrack na qumphirah. Taifa la watu wa ajab sana hodari kwa kuelezea mabomba ya gesi tu
 
Habari wakuu,

Naomba kuuliza gesi ya Songosongo ya tokea enzi za Mwalimu.

1. Iliishia wapi? Mbona sikuwahi kusikia hata siku moja ikiongelewa?
2. Hii gesi ilikuwa ikitumikaje?
3. Je, gesi ya Songo Songo na ya Mtwara zinatofauti gani.? Kwa maana ya aina ya gesi.

Asante.

3.Gesi ya Songosongo na Mtwara hazina tofauti na zote zina zaidi ya 98% ya methane (CH4).
2. Gesi ya Songosongo ipo na kwa sasa inazalisha umeme kwa na kampuni ya Songas baada ya kuchakatwa na kampuni ya Pan Africa.
1.
 
Habari wakuu,

Naomba kuuliza gesi ya Songosongo ya tokea enzi za Mwalimu.

1. Iliishia wapi? Mbona sikuwahi kusikia hata siku moja ikiongelewa?
2. Hii gesi ilikuwa ikitumikaje?
3. Je, gesi ya Songo Songo na ya Mtwara zinatofauti gani.? Kwa maana ya aina ya gesi.

Asante.

ina miaka ya kuendelea kuwepo hivyo haiwezi kuisha
 
3.Gesi ya Songosongo na Mtwara hazina tofauti na zote zina zaidi ya 98% ya methane (CH4).
2. Gesi ya Songosongo ipo na kwa sasa inazalisha umeme kwa na kampuni ya Songas baada ya kuchakatwa na kampuni ya Pan Africa Energy.
1. Kama nilivyosema hapo juu gesi ipo na kwa sasa serikali imejenga mtambo wa kuchakata gesi hiyo hapo kisiwani na bomba linalopita baharini mpaka Kilwa masoko na kuunganika na lile la kutoka (Madimba) Mtwara pale Somanga Fungu kuja Dar es salaam Kinyerezi. Uzalishaji wa Songosongo unategemewa kuanza kabla mwisho wa mwaka huu au mapema mwakani.
 
Si kweli. Mabomba hayajaunganishwa. Kila bomba limekuja hadi dar es salaam kivyake. Ila lile la mnazibay limekuja hadi somanga fungo kilichofanyika ni kwamba kuanzia somanga fungo mabomba yote yamepita kati njia moja. Namaanisha on the same way leave. Lakini kamwe hajaunganishwa.

Naona hapa tunachanganya uelewa japo maana yawezekana ikawa ileile, Songosongo kuna Plant mbili, yaani ile ya Pan Africa Energy ambayo bomba lake linakuja moja kwa moja mpaka Dar es salaam kupitia baharini, Kilwa, Somanga Fungu. Plant nyingine imejengwa na serikali ambayo bomba lake linafuata njia hiyo mpaka Somanga Fungu na kuunganika na lile la Mtwara mpaka Kinyerezi, Ubungo mpaka Tegeta.
 
Kuna kuchanganya habari hapa. Kuna miradi miwili tofauti ya gas:
1. Songosongo ambayo ilianza uzalishaji June 2004. Inazalisha umeme kwa mitambo ya Songas na Tanesco. Pia baadhi ya viwanda Dar vinatumia hii gas. Inakuja kwa bomba la 16" kutoka Songosongo -Dar na muendeshaji ni Panafrican Energy.
2, Songosongo na Mnazibay ni miradi ya TPDC ambayo ndio wamenza uzalishaji Mnazibay Mtwara na kuleta gas kwa bomba la 36". Muda si mrefu wataanza uzalishaji kwa mitambo ya Songosongo na kuleta gas kwa bomba la 24" linaloungana na lile la Mtwara pale Somanga.
 
Ndo inatumika songas, pale ubungo! Hii ya kinyerezi ndo mpya, bomba linauwezo wa kuzalusha 3000Megawatt ila kwa ss linalisha mitambo yenye kuzalisha 150Megawatt ila by end of 2016 litakuwa linalisha mitambo yenye kuzalisha 1500Megawatt
asante kwa majibu mazuri
 
Gesi ya Songosongo bado ipo na inaendelea kufanya kazi. Tatizo lililotokea mwanzoni ni kwamba walijenga bomba dogo sana. Kwa hali hiyo, gesi iliyokuwa inazalishwa Songosongo na kupelekwa Dar es Salaam ilikuwa haitoshelezi mahitaji ya mitambo yote ya gesi. Gesi hiyo ilikuwa inatumika pale Ubungo kwenye mitambo ya Songas pamoja na kule Tegeta kwenye mitambo ya IPTL almaarufu mitambo ya ESCROW.

Baada ya kugundulika kwa gesi ya Mtwara na uamuzi wa serikali kujenga bomba kubwa hadi Kinyerezi Dar es Salaam, bomba hilo lina matawi mawili. Tawi la kwanza linatoka Madimba Mtwara hadi Nangurukuru. Tawi la pili linatoka Songosongo hadi Nangurukuru. Pale Nangurukuru mabomba ya kutoka Songosongo na Mtwara yameunganishwa kwenye line moja. Hii ni kusema kuwa vyanzo vyote vya gesi yaani Songosongo na Madimba vimeunganishwa kwenye njia moja na hivyo kuwa na kiwango kikubwa cha gesi.

In short, gesi ya Songosongo bado ipo na inaendelea kuzalishwa na inatumika sambamba na gesi ya Mtwara. Pitia mradi wa ujenzi wa bomba la gesi utaelewa

IPTL siyo mafuto mazito?au nimesahau?
 
Back
Top Bottom