Gesi ya matumizi ya majumbani yapanda bei

ccm mbele kwa mbele...
Pongezi ziifikie serikali ya CCM kwa jinsi ilivyo na uwezo wa kukandamiza maisha ya Watanzania lakini inawazuga na wanabaki kuisifia na kuipongeza. Hongera sana CCM kwa ulaghai uliotukuka.
Hongera pia kwa Rais Magufuli kwa kuwa Rais mwenye uwezo wa kuwaambia wananchi SIONGEZI MSHAHARA na bado akapigiwa makofi na kushangiliwa kama malaika mkuu.
Jee hili ni aina mpya ya Limbwata ambalo wamelishwa Watanzania na kupumbazika? Au ni ujinga wao tuu ndio hawawezi kutambua hata wakinyanyasika? Ni kama vile kauli ya Marehemu Kenyatta kuhusu Watanzania kuwa ilikuwa sahihi.
Kutoifuta CCM ni janga LA kitaifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iwura mkigundua kuwa oryx alipandisha Bei kinyume na Sheria au taratibu, hukumu yake siyo kushusha Bei tu. Iangaliwe Bei inapandishwa lini na ilidumu mpaka lini.
Kisha kwa muda ule ule ipunguzwe Mara mbili kwa kiwango alichopandi ( pesa aliyoongeza Kila mtungi)ili kufidia pesa za walaji waliozurumiwa. Haiwezekani Kisha waibia watanzania alafu aambiwe Sasa punguza be.
VINGINEVYO TUTATAFSIRI KUWA ULIKUWA NI MPANGO NA WENYE MAMLAKA KUJIPATIA PESA.
TAIFA GESI IMEFIA WAPI?
Bei ya gesi za majumbani (LPG) yapanda mara dufu

Mtungi mdogo, 6kg: Kutoka TZS 19000/- hadi TZS 22000/-

Mtungi wa kati, 15kg: Kutoka TZS 48000/- hadi TZS 54000/-

Mtungi mkubwa, 30kg; Kutoka TZS 75000/- hadi TZS 100500/- #MMM


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sudan Bei ya Mkate ilipanda , Bashir akapoteza Madaraka na leo huyo wanampeleka ICC.
Tatizo la kwetu hapa Tanzania, hakuna wa kuwasemea Wananchi ,kila Mbunge yupo busy kuwaza Uchaguzi.
Wasudan hawakusubiri kusemewa na mbunge, walilianzisha wananchi wenyewe, hao wabunge, wanaharakati na wanajeshi waliwakuta mbele ya safari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TAIFA GESI IMEFIA WAPI?
Bei ya gesi za majumbani (LPG) yapanda mara dufu

Mtungi mdogo, 6kg: Kutoka TZS 19000/- hadi TZS 22000/-

Mtungi wa kati, 15kg: Kutoka TZS 48000/- hadi TZS 54000/-

Mtungi mkubwa, 30kg; Kutoka TZS 75000/- hadi TZS 100500/- #MMM

Mkuu unajua maana mara dufu? Yaani ongezeko la elfu 2 ni mara dufu hiyo? Hivi UKAWA mkoje lakini?
 
Alafu mfumo wetu siyo wa kumtetea raia, ukumbuke hilo, askali wenyewe wanafanya mazoezi ya kuua kama si kupiga raia anayedai haki yake.
Sudan Bei ya Mkate ilipanda , Bashir akapoteza Madaraka na leo huyo wanampeleka ICC.
Tatizo la kwetu hapa Tanzania, hakuna wa kuwasemea Wananchi ,kila Mbunge yupo busy kuwaza Uchaguzi.
 
Meneja wa EWURA, Titus Kaguo amekiri kupanda kwa bei ya gesi za majumbani na amesema wameshaanza kuchukua hatua kwa kufuatilia makampuni ili kujua changamoto na sababu za bei kupanda. Ni vema tukawa tu wavumilivu kwa kipindi hiki lakini naamini bei zitashuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom