Gesi Ya Kupikia Kuagizwa kutoka nje ya nchi kuanzia Septemba 2016

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,079
7,967
83adebdef81c2b974e7af851aede1c6b.jpg

Serikali itaanza kutumia mfumo wa uagizaji wa pamoja wa nishati ya gesi ya kupikia (LPG), kama inavyofanyika kwa mafuta ya ndege, petroli, dizeli na mafuta taa ifikapo Septemba mwaka huu.

Akizungumza wakati wa semina ya wadau wa sekta ya mafuta kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, Mkurugenzi wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Godwin Samuel alisema mpango huo utasaidia kupunguza gharama na bei ya gesi hiyo inayoanza kutumika kwa kasi majumbani.

Samuel alisema mpango huo pia utaongeza udhibiti wa mapato ya Serikali katika sekta hiyo inayoshika kasi nchini.

Kuhusu uagizaji wa mafuta ya ndege, petroli, dizeli na mafuta ya taa, Mkurugenzi huyo alisema mchakato unaendelea kuboresha mfumo wa sasa kwa kukusanya maoni na mapendekezo ya wadau yatakayotumika kubadilisha taratibu zilizopo ifikapo Novemba, mwaka huu mikataba ya sasa itakapomalizika.

“Tunakusudia kuongeza ushindani wenye tija katika uagizaji wa pamoja wa mafuta ya ndege, petroli, dizeli na mafuta taa kwa kuongeza idadi ya kampuni kulinganisha na kandarasi zilizopo zinazofikia kikomo ifikapo Novemba mwaka huu,” alisema Samuel.

Kuhusu elimu kwa wadau, Mkurugenzi huyo alisema Ewura inalenga kuwawezesha kujua na kuzingatia mabadiliko yanayotokea katika sekta na biashara ya mafuta ili kuwezesha kila upande kutimiza wajibu kulingana na sheria, kanuni na taratibu.

“Changamoto zinazoikabili sekta na biashara ya mafuta hayawezi kutatuliwa na Ewura pekee bali ni kwa ushirikiano wa wadau wote,” alisema.

Chanzo: Mpekuzi

Wadau hii imekaaje??
Kwani hapa nchini kwetu hatuna gesi mpaka tuagize kutoka nje??
 
Wawe makini sana maana kama mafuta ya ndege yalichakachuliwa wasije kutuchakachulia na gesi tukalipukiwa majumbani mwetu
 
Hahahahahah usilolijua ni usiku wa giza mkuu .Gesi ipi le ya helium ama?[/QUO
mtwara hawajagundu ya Helium
ile ya mtwara pia inaweza kutumika kwa matumizi ya nyumbani
tofauti iliyopo kati ya hizi mbili ni kuwa
LPG hii tunayoiona sasa ni zao la mafuta wakati ile ya Mtwara ni natural product
 
Hahaha najua mkuu nilikua na joke tuu najua industry in and out na kwa taarifa tu pia gesi ya Mtwara haifai kwa matumizi ya nyumbani.
 
Kuhusu elimu kwa wadau, Mkurugenzi huyo alisema Ewura inalenga kuwawezesha kujua na kuzingatia mabadiliko yanayotokea katika sekta na biashara ya mafuta ili kuwezesha kila upande kutimiza wajibu kulingana na sheria, kanuni na taratibu.

Hivi hiyo elimu kwa wadau itfundishwa na kusambazwa kwa mwezi mmoja?
Au ndo kaupenyo kwa EWURA kupiga chao?
 
Hahahahahahahaha najua huezi amini nilishangaa kama wewe bt thats the fact for industrial use only and mind you tuna viwanda vingapi currently?Tafuta wataalam wa huko wakueleze vizuri .
Hiyo gesi hata ikiuzwa huko viwandani hatutapata pesa?? Kama sie hatuna viwanda, tutashindwa kuiuza kwa wenye viwanda??

Halafu aliyekudanganya haifai kutumika majumbani ni nani??
 
Hiyo gesi hata ikiuzwa huko viwandani hatutapata pesa?? Kama sie hatuna viwanda, tutashindwa kuiuza kwa wenye viwanda??

Alafu aliyekudanganya haifai kutumika majumbani ni nani??
Mkuu yaishe lakini endelea kuisubiria tuu lakini ningefurahi kama ungeende TPDC au ktk makampuni yaliyopo yanayojishughulisha na hii rasilimali ungepata picture ya story nzima ya gesi
 
Mkuu yaishe lakini endelea kuisubiria tuu lakini ningefurahi kama ungeende TPDC au ktk makampuni yaliyopo yanayojishughulisha na hii rasilimali ungepata picture ya story nzima ya gesi
Kwanini wewe usiweke hiyo picha hapa?? Fanya hivyo usaidie na wengine
 
Kuhusu elimu kwa wadau, Mkurugenzi huyo alisema Ewura inalenga kuwawezesha kujua na kuzingatia mabadiliko yanayotokea katika sekta na biashara ya mafuta ili kuwezesha kila upande kutimiza wajibu kulingana na sheria, kanuni na taratibu.

Hivi hiyo elimu kwa wadau itfundishwa na kusambazwa kwa mwezi mmoja?
Au ndo kaupenyo kwa EWURA kupiga chao?
Isije kuwa kama kerosene haionekan watu wanalanguliwa mpaka sh2000
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom