Gesi, Viazi Mbuga za Wanyama Siyo vya Muungano?

Highlander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
3,093
1,075
Warioba angeweka gesi, viazi, mbuga za wanyama, makaa ya mawe na mengineyo kwenye mambo ya muungano naona lingemsumbua kidogo hili. Rasimu ya Katiba mpya inapendekeza uundwaji wa Serikali ya Shirikisho, ili kila sehemu ipate nafasi ya kufanya mambo fulanifulani kivyakevyake; kwamba si vitu vya muungano. Mwenye gesi, hayaaa; mwenye viazi hayaaa ruksa kufanya mnavyotaka... Haviko kwenye muungano hivi.

Na ndipo hapo napata kijiswali wadau: hivi haiwezekani ikatokea siku huko mbele mikoa mmojammoja wakatumia mwanya huu kutaka uhalali wa kuwa na bendera yao ya pekee? Hili wazo la Serikali Tatu si mtego huu kweli? Napata mashaka ipo siku inakuja tunaweza tukajikuta tuna serikali nne, serikali tano na kuendelea huko mbele kwa sababu ya katiba hii. Nyerere alitaka serikali moja. Isije kuwa aliona tatizo hili la mikoa kutaka kujiendesha kila moja kivyakevyake ndo maana hakutana serikali tatu.

Kwa nini Nyerere alitaka serikali moja?


Mambo ya muungano yanayopendekwa ni:


  1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  3. Uraia na Uhamiaji
  4. Sarafu na Benki Kuu
  5. Mambo ya Nje
  6. Usajili wa Vyama vya Siasa
  7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom