Gesi nyingi tumboni, na kuipumua bila udhibiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gesi nyingi tumboni, na kuipumua bila udhibiti

Discussion in 'JF Doctor' started by pmwasyoke, Feb 22, 2012.

 1. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kuna kijana - wa umri wa A level hivi - ana tatizo la kiafya linalomkera sana na kumfanya hata kusoma darasani imnyanyase sana. Gesi nyingi hutengenezeka tumboni na mbaya zaidi inajitokea inavyotaka makalioni bila control.

  Wadau naomba yeyote mwenye ushauri kuhusu kushughulikia hali hii asaidie. Kaishafika hospitali kadhaa lakini mafanikio bado.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Hapo inaonekana unakula sana maarage ya boarding pia sfinta masozi za nyuma zimeachia ndio maana unaachia mabomu ya mbagala ovyo ovyo,pia mkuu sisi ni binadamu matatizo ni kawaida haina haja ya kumsingizia ugonjwa jamaa yako wkt unaeumwa ni wewe,hakuna hatakayekucheka ukisema wewe kwani si jambo geni hilo na lina tiba nzuri subiri madocta waje wakusaidie.
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Japo hukuwa na lazima ya kuandika yale unayoyadhania tu, asante kwa mengine uliyosema!
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  too much fibre consumption
   
 5. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Kwenda hopitali nakupewa dawa siyo sababu je mwambia anapoenda hospitali akapime full blood picture maana kunaweza kuwa bacteria infection ambao wanatabia ya kutoa gesi mpaka tumbo linajaa ,kama vipi mwambie atumie asali kwa ajili ya mmengenyo
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Mwenye Ugonjwa wa Gesi Na Maumivu

  abugie unga laini wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja kabla ya kula chakula ukifuatisha na glasi ya maji yenye Uvuguvugu iliotiwa Asali ya Muwa kiasi cha vijiko vitatu, utumie kila siku kwa muda wa wiki moja.
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Thanks MadameX - I suppose by fibre you imply beans and vegetables.
   
 8. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hii inaweza kuwa Giardia Infection,...Kamwone Dr kupima choo kwanza kabla ya kupata Tablets Tinidazole
   
 9. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  ndo unga gani tena huo mkuu ?
   
 10. Mabwepande

  Mabwepande JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Dawa ni kujamba tu.
   
 11. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Tabu yake kwa dawa hiyo inabidi uwe antisocial kabisa
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Unga unao itwa kwa jina la ( Habbat-Sawdaa) kwa lugha ya kiingereza inaitwa (nigella sativa seed
  )
  unapatikana nenda pale Kariakoo kaulize kwenye maduka ya

  Dawa za kiarabu utapata hiyo Dawa utakwenda nayo nyumbani kuipasha moto kidogo kama unavyo pasha moto karanga mbichi angalia isiunguwe weka katika moto kidogo ipate moto kishaa twanga uchekeche ili uwe unga kisha waweza kutumia hiyo Dawa angalia hii picha chini


  [​IMG]
  [​IMG]
  Nigella sativa seed
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mzizi,
  Unaposema Asali ya Muwa unamaanisha Juisi ya Muwa? au sukari gulu?...au kuna kitu tofauti, maana sijapata kuiona!
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  ipo Asali ya muwa waulize wafugaji watakwambia namna ya utengenezaji wake mimi sio mfugaji mkuu vipi arusha unatunyima nini huko?
   
 15. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Asante kwa ushauri
   
 16. k

  kamili JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Pole kwa shida hiyo ambayo haikondeshi ila inatia aibu, na hivyo yaweza kukuletea sonono.

  Sababu yake

  Kitalaamu hali hiyo inaitwa Flatulence. Watu wote na karibu wanyama wote wanapata flatulence (kiswahil kujamba), na kila mtu ambaye ni mzima aweza ajambe angalu mara ishirini kwa siku (yaani katika saa 24). Katika hali ya kawaida kutoa hewa kwa njia ya nyuma kunatokana na baadhi ya hewa huingia tumboni wakati wa kula na kumeza chakula. Na japokuwa baadhi ya hewa hiyo hufyonzwa na kuingia kwenye damu na baadae kutoka nje kupitia mapafu, sehemu ya hewa hiyo hubaki tumboni na ndio hiyo hupitia njia ya nyuma. Pili inafahamika tumboni kuna Organism wengi hasa aina ya bakteria. Pamoja na kazi nzuri yenye manufaa wanayoifanya lakini pia huchachusha baadhi ya vyakula vilivyoliwa, Na hivyo kutengeneza hewa (gas) hasa aina ya oxyegen, carbondioxide, methane,nitrogen nk.
  Hata hivyo pamoja na sababu hizo hapo juu ambazo ni za kibiologia mtu aweza apate shida ya kujamba kuliko ilivyo kawaida. maradhi mengi yaweza sababisha hali hiyo. Hata hivyo shida ambayo imeonekana kusababisha hali hiyo kwa watu wengi ni mfumo wa uyeyushaji chakula kushindwa kuyeyusha vyakula aina ya wanga (carbohydrate) kikamilifu. Kama upo A level kama ulivyosema basi utakumbuka wanga huliwa ukiwa katika hali ya Polysaccaride, then huanza kumeng'enya tangu ukiwa mdomoni na kuwa disaccaride, na halafu ukiwa tumboni humeg'enywa na kuwa monosaccaride (yaani glucose) na hivyo kufyonzwa (absorbtion)kwenye utumbo na kuingia mwilini. Kuna kemikali zinaitwa mimeng'enyo
  (enzymes or digestivu juice) ndio ambazo hufanikisha shuhuli hiyo. Kuna baadhi ya watu wana upungufu wa hiyo mimeng'enyo tumboni, na hivyo vyakula vya aina ya wanga huwa haviyeyushwi kikamilifu kufikia ile hali ya mwisho inayofyonzwa na mwili yaani monosaccaride. Hivyo masalia ya chakula aina ya wanga ambacho hakijayeyushwa kufikia monosaccaride hubaki kwenye utumbo na hivyo kuchachuswa ( fermentation) na hao organism wa tumboni na hivyo kuzalisha gas nyingi. Gas hizo hazina mahali pakutokea bali njia ya nyuma.

  Nini cha kufanya?
  Kwanza kuna baadhi ya vyakula ambavyo huzidisha shida hiyo, kama inawezekana itabidi upunguze kuvila, naamini unavifahamu. Chakula ambacho kikiliwa hakina gas hata kama una shida niliyoitaja hapo juu ni wali peke yake. Bahati mbaya huwezi kula wali peke yake!!??
  Hata hivyo bahati nzuri ni kuwa uyeyushaji wa vyakula vya wanga huanzia mdomoni (kumbuka salivary amylase) hivyo hata kama una upungufu wa enzymes zingine hiyo iliyo kwenye mate yaweza kusaidia sana. Hivyo basi hakikisha unapokula chakula unatafuna polepole na kwa muda mrefu mpaka tonge lote au funda lote la kinywaji kama chai, soda nk. vimechanganyika vyema na mate ya kutosha. maana yake ni kwamba hivyo vyakula aina ya wanga vinapofika tumboni vitakuwa vimeyayuswa kiasi cha kutosha na hivyo kuanza kufyonzwa, kwa maana hiyo hao intestinal organism hawatakuwa na wanga wa ku ferment, na shida yako yaweza kwisha.
  Hongera kwa kuiweka shida yako wazi.   
 17. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Niwashukuru wote wanaJf mliochangia mawazo kwa nia ya kutusaidia. Kwa vile naamini yawezekana mwingine akapata shida kama hii siku za mbele, nieleze kwamba baada ya utafiti hospitali kubwa za Dar kijana aligundulika na ugonjwa uitwao procto colitis. Anaendelea na matibabu.
   
 18. H

  Hamfrey New Member

  #18
  Mar 14, 2016
  Joined: Mar 13, 2016
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pmwasyoke nina shida sana ww. Naomba unitafute kwenye hizi namba 0787474202
   
Loading...