Gesi na Makaa tunayo. Kwanini hatujitoshelezi kwa umeme kupitia Tanesco?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
32,985
60,480
..kitu cha habari hapo juu chahusika.

..pamoja na vyanzo hivyo vya umeme nilivyovieleza hapo juu tuna mito mikubwa yenye maporomoko ya maji, pia kuna maeneo yenye upepo wenye nguvu za kuzalisha umeme.

..kwanini nchi hii imeshindwa kuzalisha umeme wa kutosheleza mahitaji yetu na kuuza nje kupitia shirika la umeme Tanesco?

..wenzetu wa ETHIOPIA wana mradi mkubwa wa umeme kupita yote inayofikiriwa Tanzania, na wanatekeleza mradi huo kupitia SHIRIKA LAO LA UMMA LA UMEME.

..Binafsi sielewi kwanini Tanesco inaendeshwa kwa hasara wakati mahitaji ya umeme ni makubwa kuliko uzalishaji.

..Vilevile sina imani na wawekezaji toka nje ktk sekta ya umeme. Uganda wana mgogoro mkubwa na muwekezaji waliyeingia naye mkataba kuzalisha umeme.

..Naomba kuelimishwa kuhusu sababu za Tanesco kushindwa kuzalisha umeme kutosheleza mahitaji yetu. Pia naomba kuelimishwa kuhusu faida za kukaribisha wawekezaji kuzalisha umeme, badala ya kuendelea kuwapa Tanesco monopoly hiyo.

cc Engineer2014 , Tetty, The Boss, Kimweri, MsemajiUkweli, salaama, Bukyanagandi , Pasco
 
Back
Top Bottom