Gesi mnayopiga kelele kuuzwa Kenya haitatumika kwenye Viwanda vya Tanzania?

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,666
8,582
Kwani hii gesi haitumiki au haitatumika kwenye viwanda vya Tanzania? Kama inatumika au itatumika kwenye viwanda vya Tanzania tatizo lipo wapi? Kwani kuna ubaya gani kama una chakula cha kutosha nyumbani kwako ukaamua kumuuzia jirani yako ili kupata pesa ya ziada kufanya mambo yako mengine?

Kama viwanda vya ndani vitakuwa vinatumia hii gesi au vitatumia hii gesi basi mama yupo vizuri sana. Kama taifa lazima tupambane kuuza bidhaa zetu nje ili kupata fedha za kigeni na hiki ndio mama anafanya

Kuna hoja watu wanaileta kuwa bidhaa za kenya zita-dominate soko la ndani kwa sababu vitakuwa vinazalishwa kwa gharama ndogo hivyo vitauzwa kwa bei ya chini. Hii hoja haina mashiko kama na sisi viwanda vyetu vitatumia gesi kwa sababu vitaweza pia kuzalisha bidhaa kwa gharama ya chini na kupelekea kuuza bidhaa zetu kwa bei ya chini pia.

Mwisho kabisa nawaomba watanzania tumuunge mkono mama. Nasikia mama ni mwanauchumi kitaaluma hivyo anajua anachokifanya, tumpe support atupeleke kwenye nchi ya asali na maziwa. Rais aliyesomea uchumi ndio tunamtaka kwa sasa.
 
Lijengwe tu kwanza sisi tunatumia kuni, pia wajenge LNGP plant Lindi, sisi tutafaidi stiglers ikikamilika.
 
Kuna hoja watu wanaileta kuwa bidhaa za kenya zita-dominate soko la ndani kwa sababu vitakuwa vinazalishwa kwa gharama ndogo hivyo vitauzwa kwa bei ya chini. Hii hoja haina mashiko kama na sisi viwanda vyetu vitatumia gesi kwa sababu vitaweza pia kuzalisha bidhaa kwa gharama ya chini na kupelekea kuuza bidhaa zetu kwa bei ya chini pia.
Mkuu shida kuna watu wana mahaba na mwenda zake hadi hawatumii akili zao tena.
 
Hiyo gesi ni nyingi mno, ndio maana inatakiwa iuzwe ilete fedha za kigeni, zilete maendeleo nchini kwetu, hivyo ndivyo nchi zote zenye gesi duniani zanafanya, Urusi wanauza gesi hadi ulaya na wana bomba la gesi kuelekea nchi nyingi tu.
 
Hiyo gesi ni nyingi mno,ndio maana inatakiwa iuzwe ilete fedha za kigeni,zilete maendeleo nchini kwrtu,hivyo ndivyo nchi zote zenye gesi duniani zanafanya,urusi wanauza gesi hadi ulaya na wana bomba la gesi kuelekea nchi nyingi tu
Mama yupo vizuri. Nasikia ni mwanauchumi hivyo anajua anachokifanya.
 
Gesi yenyewe ipo wapi ww, porojo za ajabuajabu tu humu, ww umesha wahi kusikia gesi ikitumika wapi, ni ipi hiyo ya kutosha mpaka kuuza kwa jirani wakati huku Kwetu haitutoshi, nilisikiaga kisiwa cha mahali ilipo gesi kina karibia ku potea, pia ilitakiwa mpaka tufikie kuuza gesi nje Basi Tz ingekuwa na unafuu wa nishati gas ili kuokoa mazingira, lakini ndiyo kwanza tunanunua gas 50k+, kwa mtungi wa 14+kg.

Sasa hapo ndipo nina choka kabisa, nchi yenye nishati yeyote kwa kawaida inatakiwa kuwa nchi tajiri Sana na wananchi wafaidike kwa nihati hiyo na siyo et bomba litengenezwe kupeleka nishati nchi jirani bali nishati husika I be processed nchini na iuzwe Kama bidhaa, nilitegemea Sasa hv kusikia Tz Kuna kiwanda kikubwa cha Taifa kilicho ajiri maelfu ya wa Tz kuchuja gas husika kuwa na thamani zaidi, but cc tunaweza kuipeleka Kenya.
 
Watu hawana jema, kibaya zaidi wanapiga kelele bila hata kujua makubaliano na mkataba unasemaje.

Ukiwa na tabia ya unyimi sana unawezajikuta unakufa njaa sababu tuu hutaki kuuza mali usiyoitumia ili mwenye uhitaji aitumie akupe pesa nawe upate chakula.
 
Hapa tatizo la hao watu wanaopingana na hili la gas kusafirishwa Kenya, ni wale wale ambao akili zao zilishikwa na shujaa na bado mawazo yao yako kwa shujaa.
 
Mkuu una uhakika gesi haitutoshi? Hivi unadhani kama kweli gesi haitutoshi mama angeiuza nje? Unadhani mama hana akili mpaka auze nje gesi ambayo sisi wenyewe tunaihitaji? Binafsi nadhani zingine ni propaganda tu. Sidhani mama atakuwa na akili ya kujihujumu mwenyewe.
 
mkuu shida kuna watu wana mahaba na mwenda zake hadi hawatumii akili zao tena.
Shujaa alikamata akili za watu na hata baada ya kwenda zake, bado zimeganda hawawezi kuwaza tena. Itawachukua muda kurudi kwenye ufahamu wao. Tuwape muda.
 
Wakenya ni 'makanjanja' full stop
Wewe ni punguani

Weka facts tatizo wa tz mnajifanya wajuaji kumbe hakuna kitu

Mijitu mioga kama kunguru pumbavu kabsaa

Toka ndani mkapambane na wengine sokoni huko

Safiiii kabsaa Mama tupo pamoja hawa wavivu lazima tuwanyooshe wazembe wazembe tu

Matagaaaaaaaa matagaaaaaaaa matagaaaaaaaa matagaaaaaaaa uuuuwwiiiiiiii njoooniii huku
 
Back
Top Bottom