Gesi, mafuta yako bara tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gesi, mafuta yako bara tu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Brooklyn, Nov 13, 2009.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Serikali jana ilitangaza maeneo 13 ambayo kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana mafuta na gesi, ikimaanisha hakuna uwezekano kwa nishati hizo kupatikana visiwani Zanzibar.

  Sehemu hizo ni Tanga, Dar, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Bigwa, Mafia, Mandawa, Kisangire, Nyuni, Kilwa, Ruvu na Mnazi Bay. Hayo yamesemwa na Waziri Ngereja.

  Source: Mwananchi la tarehe 13/11/09 pg 2

  Wadau ina maana Baraza la Wawakilishi na vurugu zote zile za kutaka suala la mafuta liondolewe kwenye masuala ya Muungano kumbe hata mafuta yenyewe hayako!!!!

  Kweli ingekula kwao!!!
   
 2. A

  AM_07 Member

  #2
  Nov 13, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  basi kama ni hivyo mafuta na gesi ni vya muungano!
   
 3. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2009
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hodi kwanza. Kisha najiuliza hayomafuta yaliyokua yakiwatoa roho ni ya karafuu nini ?
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hapa suala si mafuta, kinachowachefua wa Zanzibar ni jinsi serikali inavyowaburuza especially inapokuja issue za Uchaguzi pale Chimwaga.
   
 5. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SERIKALI jana ilitangaza maeneo 13 ambayo kuna uwezekano mkubwa wa kupatikana mafuta na gesi, ikimaanisha hakuna uwezekano kwa nishati hizo kupatikana visiwani Zanzibar.

  Suala la mafuta na gesi limekuwa gumzo kubwa visiwani Zanzibar kiasi cha kutaka liondolewe kwenye masuala ya Muungano, licha ya mtaalamu aliyekodishwa na serikali kushauri kuhusu mafuta kueleza bayana kuwa uwezekano wa nishati hiyo kupatikana Zanzibar ni mdogo.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alitaja maeneo ambayo yana uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa mafuta na gesi kuwa ni Tanga, Dar es salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Bigwa, Mafia, Mandawa, Kisangire, Nyuni, Kilwa, Ruvu na Mnazi Bay.

  Akifungua mkutano kuhusu utawala bora katika sekta ya petroli jana, Waziri Ngeleja alisema hadi sasa harakati za utafutaji mafuta nchini bado hazijazaa matunda, lakini matarajio yaliyopo ni makubwa.

  Alisema utafiti wa kuwepo mafuta na gesi katika maeneo mbalimbali ya nchi unafanywa na makampuni kutoka Ufaransa, Uingereza, Australia, Brazil, Canada, Norway na Dubai.

  “Tangu zianze harakati za utafutaji mafuta mwaka 1950 hadi sasa bado hatujapata mafuta lakini matarajio ni makubwa sana kwa sababu tuna imani na makampuni yanayofanya utafiti,” alisema Ngeleja.

  Suala la mafuta limekuwa likiibuka kila mara Baraza la Wawakilishi linapokuwa na mikutano yake na mara kadhaa suala hilo huwaunganisha wawakilishi wa CCM na wa chama kikuu cha upinzani visiwani humo, CUF.

  Baada ya mshauri mtaalamu kueleza kuwa uwezekano wa kupata mafuta visiwani humo ni mdogo, wawakilishi walidiriki kusema “hata hayo mafuta yakiwa madogo kiasi cha kujaa glasi, watuache tutagawana ili tujipake”.

  Hata hivyo, Rais Jakaya Kikwete akijaribu kutuliza moto huo wa wawakilishi, alisema hakuna haja ya kugombea kitu ambacho hakuna uwezekano wa kukipata na akaeleza kuwa tafiti nyingi zilizofanywa zimeonyesha kuwa ukanda wa eneo la Mashariki mwa Afrika hauna mafuta.

  Waziri Ngeleja pia alisema sekta ya petroli inakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo kupanda na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia hasa wakati huu ambao dunia imekumbwa na mtikisiko wa uchumi.

  Waziri huyo alisema tayari wameliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) lianze kuagiza mafuta kupitia kampuni ya COPEC ili iwarahisishie kupata taarifa za kweli na ambazo hazitakuwa na upotoshaji.

  Kuhusu suala la mikataba na rushwa, Ngeleja alisema wamejipanga vizuri kisera na kisheria na kwamba, hata mikataba iliyopo ina uwazi wa kutosha na kuna utaratibu mzuri ambao hautoi fursa ya kuingia kwenye rushwa.

  Akitoa mada katika mkutano huo, Dk Inge Amundsen kutoka taasisi ya Michelsen ya nchini Norway alisema serikali inatakiwa kuwa makini katika suala la rushwa na uwazi wakati inaposaini mikataba mbalimbali, kuepuka migogoro ya ardhi na utunzaji wa mazingira.

  Mmoja wa wabunge walioshiriki mkutano huo, Hamad Rashid alisema mkutano huo utawasaidia katika harakati za utafutaji mafuta na gesi na namna ya kuingia mikataba mbalimbali.

  Naye Charles Keenja alisema mafunzo hayo waliyaomba kutoka kwa waziri wa nishati wa Norway wakati walipokwenda nchini humo kikazi na kwamba yatawasaidia kuwa na ufahamu mpana hasa wakati huu wanapojiandaa kutunga sheria ya mafuta na gesi mwakani.  Chanzo: Mwananchi.  Zanzibar hakuna mafuta hata tone hili halina ubishi tayari wataalamu wameshawaambia sasa sijui kwanini wapemba bado wanalazimisha mambo siyokuwepo.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Nov 13, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama mafuta yapo bara pekee tunaomba yarudishwe kwenye Muungano! Baraza la Wawakilishi likae tena kurekebisha ile orodha isomeke "Mambo ya Muungano: 1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, 2. Mambo ya Nchi za Nje, 3. Ulinzi na Usalama...15. Maliasili ya Mafuta...22. Uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo."
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Acha uongo...Zanzibar ina mafuta ya nazi na karafuu kibao...
   
 8. a

  alex50 JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Badala ya wawakilishi kuzungumzia mambo ya maendeleo, wamepoteza muda kuzungumzia wasichonacho, na kupinga ushauri wa mtaalam elekezi aliyewaambia hawana mafuta.
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Usimtukane mkunga...........

  Amandla......
   
 10. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mi nafikiri wakishagundua kwamba zenji hakuna mafuta wala gesi, watakuja na statement kwamba walisoma vibaya list ya masuala ya muungano na hivyo wanatamka rasmi kwamba mafuta ni suala la muungano!!!
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwiba na kundi lake wako wapi?

  Mwiba bado anakula kifungo?

  Nakumbuka miaka ya 90, Wazenji wengi sana walianza kujiita Wazanzibar. Wakaanzisha hadi mitandao yao. Wakawa busy kututenga wenzao ingawa walikuwepo waqchache wakorofi waliokuwa hawataki huo upuuzi. Hawa hadi leo tuna uhusiano nao mzuri.

  Maadamu Mafuta hamna, mie wazo langu bado ni lile lile.

  1. Tunaungana kikweli na Zanzibar inakuwa ni MKOA na si nchi ingawa inaweza kupewa upendeleo ili watu wasiwe wengi na ikibidi wengine wahamishiwe bara maana huko tatizo la ardhi litakuwa ni kubwa muda si mrefu.

  2. Tuvunje muungano na kila mtu aende zake.

  Hii itasababisha hizi kelel kuisha milele....
   
 12. October

  October JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Du umenichekesha sana!!!. kwa hiyo unataka kusema Chetu ni Chao,lakini Chao si chetu?
  Na kweli ikiwa hivyo utasikia chokochoko na wakati wenyewe wamesha set precedence.
  Unafiki mwinge wa ajabu sana.
   
 13. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Zanzibar hawajisifii cha mtu na wala hawataki cha mtu ,wacha niulize ipo siku nyie mshawahi hata siku Mmoja ukasikia wamejivunia chochote kile kilichokuwepo Tanganyika kuwa ni chao?hutosikia hata siku mmoja kwani wanaelewa kuwa sio vyao ni (kupakana mafuta kwa nyuma ya chupa) ni sawa na watowa maoni ya hii issue mnajidanganya Bure wenye kunemeka mnawaelewa fika, nyinyi ni sawa na wapiga Debe poor you ,I realy feel sorry for you guys.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  And to add insult to injury the islands of Zanzibar are slowly sinking. Hawa nilishawakaribisha Bara kitambo. Long live the Union!
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Na hii global warming sijui watakimbilia wapi? Wenzao maldives wameishaanza kufanya mazoezi ya vikao vyao vya bunge "underwater"!

  Amandla.....
   
Loading...