Gesi asili: Is it "day light robbery?!" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gesi asili: Is it "day light robbery?!" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Pascal Mayalla, Jul 27, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,461
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Nimekutana na hii kitu, nimeisoma, sio tuu nimeshangaa, bali nimechoka, imeniacha hoi, mtu unaweza kupata wazimu, ukikamata SMG, unaweza kuwamiminia risasi Watanzania wenzetu wanauiuza nchi yetu na maliasili zake kwa bei ya bure kwa wageni kwa jina la wawekezaji kwa kisingizio kuwa sisi hatuna uwezo wa kuwekeza!.

  Tumeibiwa sana kwenye madini na mpaka sasa tunaendelea kuibiwa kwa mikataba mibovu, Mungu katupa gesi asili angalau ituokoe kutoka katika hili lindi la umasikini uliotopea...lakini kumbe..., masikini Watanzania!,, na kwenye gesi asili, Watanzania tunaendelea kuibiwa mchana kweupee!. Hatuna Sera, Hatuna Sheria, na bado tunashadadia kugawa vitalu!. Hii ni "day light Robbery!" na inafanywa na viongozi hawa hawa tulio nao tukidhani ni wenzetu lakini kumbe. ..

  Hebu soma hapa chini!.

  After studying the experience from other countries, the following lessons were learnt:
  • Location of LNG Plant – should be constructed on land (not floating LNG
  on sea)
  • Reasons: Mainly for monitoring and control purposes – monitoring is challenging because of lack of technology and control means
  • There should be only one plant.
  • The GoT/Tanzanians/Public should have majority shares to the entire
  Infrastructure say not less than 51% – to have authority say and decision
  making for the benefit of the country. It may be on PPP model.
  • The proposed land for construction of LNG and other industries utilizing natural gas should be owned by the government. Facilities like roads, water and electricity should be put by GOT and appropriate tariff should be determined for the government.
  1. KWA GESI ALIYOTUJALIA MWENYEZI MUNGU, TUKIJIPANGA VIZURI, TUTAPATA MAENDELEO MAKUBWA KULIKO AMA KAMA SOUTH AFRICA.
  2. MAKAMPUNI MAKUBWA YA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI YANAELEWA NA YANATAKA TUBAKI KWENYE HALI YA KUTOELEWA HALI YA BIASHARA YA GESI. YANATULAGHAI KWA NJIA YA UZOEFU NA WALIONAO.
  3. GAS HATA KAMA IKO CHINI YA BAHARI AU CHINI YA ARIDHI NI MALI YETU NA INAYO VALUE YAKE NA SIO MWENYE UWEZO WA KUITOA ARIDHINI BASI NDIE MWENYE GAS DARWIN THIORY ISITUMIKE KWA MALIASILI YA NCHI YETU.
  MY TAKE!.
  1. Kumbe gesi yote inayovunwa nchini sasa na itakayoendelea kuvunwa miaka ijayo, siyo yetu!, ni ya mwekezaji!.

  2. Kumbe eti hiyo gesi huko ilipo haina thamani yoyote kwetu ikiwa huko chini ardhini ilipo, na wala sio mali yetu!, bali ni mali ya mwekezaji anayeichimba na sisi tunauziwa kwa bei ya soko, na faida yote ni ya mwekezaji anayechimba, ila taifa litafaidika na kodi!.

  Nimeshindwa kuendelea kwa sasa kutokana na hasira!, unaweza ukaua mtu! . Labda mbele ya safari, kutakuja kutokea kichaa mmoja akiyajua haya atawamiminia risasi wahusika wote wakuu walio yafanya haya au kuachia yafanyike katika ardhi ya Tanzania.

  Mungu Ibariki Tanzania!.

  Paskali
   

  Attached Files:

 2. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  MKuu Pasco,
  Kutokana na hali uliyokumbana nayo naelewa kiasi cha hasira au gadhabu ya maswahibu haya.
  Juzi nimeona kwenye vyanzo mbalimbali vya habari, Raisi wa nchi yetu akifanya mazungumzo na watu wa British Gas, nafikiri wako mbioni kuja kama hawajafika tayari. Huku nimeona British high commissioner wakifanya mpango wa kuwatrain vijana wetu wa VETA, namna watakavyofaidika na uchimbaji huo wa gesi huko Mtwara, nafikiri hawakuona umuhimu wa vijana wa Tanzania kama nchi, wamewaona hao wachache watakaofundishwa namna ya ufagizi, uchimbaji mitaro, na ulinzi. Lakini sio kushika piperange na kufunga mabomba ya gesi.
  Huu ni unafiki tu, kwani wangeweza kutusaidia technical knowledge ya vyuo vyote vya kiufundi kwa gharama tu kidogo ya hicho wanachokipata kwa kutuibia mchana.
   
 3. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,174
  Trophy Points: 280
  Wewe huoni kwanini Magamba hawataki tuwe na elimu ya kutosha.... Wamepigwa Mkwara waendeshe nchi kama inavyoendeshwa... ili tubaki wajinga tuibiwe hadi pale yatakapobaki mashimo matupu ndio watatuachia...

  Kayumba Shule za Kata ... mikopo kwa shida Hospitalini no vifaa wanatuacha tufe tu kwani tuna faida Gani... na wewe ukionekana unaleta Utata na kujua sana Dawa yako unapelekwa Misitu ya Pande koreo linakusubiri huko... Haki ina Gharama Mkuu kuipata
   
 4. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 491
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Nasikia kuna sheria mpya ya gesi inakuja Je serikali inategemewa kuwa na intézése ya kiasi gani?
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Basically British Gas will put LNG processing plant with intention to export the gas to Asian and European markerts. I hope mikataba haitakuwa kama ile ya dhahabu...I also hope tutaweka baadhi ya mambo wazi...mfano kuweka katika sheria partnership na local companies/firms katika suala zima la uendeshaji wa industry nzima ya petroleum. Tukumbuke tunahitaji knowledge transfer na hakuna namna tutaipata kama hatutakuwa part of the big picture sustaining the industry.
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Pasco, nataka kuhamia Ntwara...nimechoka na siasa za JF. Nimeamua kwenda kushinda km 200 katikati ya bahari na mabepari wanaotafuta gesi nijue moja.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Nikisikia kuhusu gas yaani moyoo wangu unavunjika kabisa, najua haitatusaidia na itavunwa sana...yaani napatwa na ubaridi moyoni halafu mafanikio nayaona kwa mbali sana...tutabakia mifupa tu hapa kwenye gas
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,375
  Likes Received: 19,619
  Trophy Points: 280
  Tukija kushagaa tutakuta gesi imeisha
   
 9. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Silly season,silly people,silly government,this proves we have reached advanced stage of silliness as a country and its people.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Sasa Pasco unayemuunga mkono awe next President anasemaje?
  si yupo bungeni na haya yako kwenye corridors zake?
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  The Boss, hilo ni swali zuri sana...maana inaonekana watu wanataka power tu bila kujua hiyo power wataifanyia nini wakiipata. Na Pasco ni sehemu ya mchakato huo maana ni watu wawili tofauti ameshaonyesha ishara za kuwaunga mkono
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  na yoote haya ya mikataba ya gesi yanatokea while hao presidential hopefulls wako
  kwenye bunge na kwenye kamati za nishati na kadhalika
  kila kinachopita wanashiriki kupitisha
  sasa Pasco si bora hiyo SMG aende akaitumie huko Bungeni?
   
 13. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naona sasa Wazanzibari watakubali mafuta na gas viwe mambo ya muungano, si hata bara vipo. Maana hawa watu hupenda tu kujisikia wana utajiri wa mafuta na gas lakini hawazungumzii jinsi wanavyoweza faidika na huo utajiri. Wazenji tuungane sasa kuhakikisha tunafaidika kwa kuishinikiza serikali kuingia mikataba/mipango yenye maslahi.

  Hongera Pasco, ila tokeza barabarani tushirikiane kumaliza hasira tulizonazo.
   
 14. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #14
  Jul 29, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mimi niliamuaga kuwekaga ile mode ya kupotezea maana ukifikiri sana unaweza kufanya the unthinkable
  Lakini sasa i can't take it anymore....kila nikitizama muelekeo wetu na hawa policy makers wetu najionea giza, najionea siasa badala ya National interest. Do we really have to dance to their silly tunes? Maana ni maneno maneno while twaliwa na hata wale tulioweka a little faith kwao are disappointing us now....the only way out of this is elimination. Dont ask me how they are going to be eliminated....but they will.....
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  pole saana
   
 16. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nilifikiri tungejifunza kutokana na madudu tuliyofanya kwenye migodi ya dhahabu! Kumbe bado tumelala usingizi wa pono.
  Nadhani inabidi hali ya hewa ibadilike angalau kwa kipindi cha mwaka mmoja ili heshima ipatikane nchi hii.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,461
  Trophy Points: 280
  Mkuu the Boss, juzi Ijumaa nilikaa naye Dodoma, amenipa matumaini fulani!.
  Kwa vile you can't miss what you never had, hiyo gesi siyo yetu, ni ya atakayeichimba!. Kwani dhahabu ni yetu?, au Tanzanite?, au urani?. Hii ndio nchi yetu!.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,461
  Trophy Points: 280
  The Boss, hii game imechezwa na the executives, wabunge wako gizani kabisa ila kijana tulionana na kupanga mipango mkakati kuhakikisha hatuibiwi tena!.
   
 19. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #19
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,349
  Likes Received: 10,485
  Trophy Points: 280
  pasco unadhani kwa nini opinion za wengi zinaonyesha kuichoka ccm?sababu ni hizi hizi.ccm haijali maslahi ya nchi,ccm inaogopa wawekezaji badala ya sisi wapiga kura.hata lowassa akishika madaraka hataweza kwenda kinyume na sera za ccm.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Kwa nini tusizuie isichimbwe hadi hapo tutakapokubaliana terms za kututosheleza sote?
   
Loading...