Gertrude Ederle: Mwanamke wa kwanza Kuvuka mlango bahari kati ya Uingereza na Ufaransa (The English Channel) kwa kuogelea Kilomita 56.327 kwa masaa 14

Polycarp Mdemu

Senior Member
Jun 2, 2019
165
209
Tarehe 6 August 1926 mdada huyu alikuwa mwanamke wa kwanza Kuvuka mlango bahari kati ya Uingereza na Ufaransa (The English Channel) kwa kuogelea Kilomita 56.327 kwa masaa 14½ tu. Aliporudi kwao baada ya kuvunja rekodi hiyo alipokelewa na Parade maarufu ya Canyon of Heroes kwa umati wa watu waliotanda Km 21 Broadway

Wachambuzi wa michezo humuita Malkia wa Mawimbi (Queen of the Waves) kwakuwa anashikilia record zaidi ya Tano za Kuogelea akiwa kama #Olympic Champion, American competition swimmer.

Ni mzaliwa wa New York, USA mwaka 1905 na Alikufa New Jersey mwaka 2003 akiwa na miaka 98, Maisha yake yote hakuwahi jiingiza katika Mahusiano, hivyo pia hakuolewa kabisa, Mwaka 1940 alipata Ukiziwi kamili, Na akawa akifundisha kuogelea watoto viziwi.

Mwaka 2001 alidhoofika Mwili na hakuwa na nguvu kabisa hivyo alilelewa katika nyumba ya wazee na mauti ikamkuta mwaka 2003 na kuzikwa katika makaburi ya Woodlawn.

Mwandishi: Polycarp MdemuView attachment 1882414View attachment 1882416View attachment 1882417View attachment 1882415

800px-Gertrude_Ederle_parade_NYWTS.jpg

1200px-Gertrude_Ederle.jpg
 
Kwanini Waafrika tunaogopa sana kufa, kiasi kwamba hata hatutaki kushiriki michezo hatarishi ili kuweka historia?
Umbali alio ogelea huyo Mama bado kidogo ukaribiane na Umbali was Darling to Zanzibar
Atasindikizwa na nini
 
Back
Top Bottom