Gerson Msigwa: Serikali inawasiliana na watoa huduma wa mitandao ya WhatsApp, Facebook na Instagram kuhusu kukosekana kwa huduma

Msemaji mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa ametoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu wakati serikali inawasiliana na makampuni ya WhatsApp, Facebook na Instagram kuhusu changamoto ya kukosekana kwa huduma ya mawasiliano ya mitandao hiyo.

Huduma za mitandao hiyo zilikwama kwa saa kadhaa tarehe 04 Oktoba 2021.

Taarifa hiyo ya wito wa serikali iliyotolewa usiku wa tarehe 4 Oktoba 2021 haikuwezekana kusambaa haraka kama ilivyo kawaida kwa kuwa mitandao hiyo ya kijamii haikuwa hewani.

Hata hivyo, baada ya juhudi mbalimbali za wataalamu huduma hizo zilirejea baadae usiku wa kuamkia tarehe 05 Oktoba 2021.

Kwa hatua hiyo serikali imeonesha kujali wananchi wake na kuthamini umuhimu wa mawasiliano. Pongezi kwa serikali.

View attachment 1964256

Huduma ilivyorejeshwa, msemaji mkuu wa serikali alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutaarifu kuhusu kurudi kwa huduma hiyo.

View attachment 1964500
Aanze na mitandao ya simu ya Tanzania ambayo speed ya internet ni changamoto,pia gharama za mb na muda wake wa matumizi haviendani mfano unanunua mb za wiki unatumia siku moja ama kwa masaa kwakifupi in wizi mtupu (day light robbery)
 
Nilitegea serikali itoe tenda kwa wajasiria maliwetu wa mambo ya mtandao watengeneze mfumo wetu wa kimawasiliano kiasi kwamba hizo nyingine zikifeli tusipate shida. Tujitegemee jamani!
 
Ni muda sasa msemaji wa serikali atueleze kwanini website za porn hazipatikani hewani hapa Tanzania?
 
Aanze na mitandao ya simu ya Tanzania ambayo speed ya internet ni changamoto,pia gharama za mb na muda wake wa matumizi haviendani mfano unanunua mb za wiki unatumia siku moja ama kwa masaa kwakifupi in wizi mtupu (day light robbery)
Kweli
 
Back
Top Bottom