Gerson Msigwa: Serikali inawasiliana na watoa huduma wa mitandao ya WhatsApp, Facebook na Instagram kuhusu kukosekana kwa huduma

Huyu naye aache sifa za kijinga sasa..kama wanajali kweli wapambanie kilio cha wananchi juu ya bei kubwa za vifurushi vya mitandao ya simu..Serikali ina mengi ya kufanya aisee na sio kutia aibu kwa kuwasilian na Facebook Inc na wakati wameshatoa taarifa kuwa ni tatizo la dunia nzima kuwauliza nini tatizo kwa sasa ni kuonyesha jinsi ulivyo outdated
Alafu unawaulizaje na wakati huna mkataba nao kama siyo upumbafu?
 
Hivi hizi fb, twitter and insta, si private entities au ni public bodies ? siku mmiliki wao akisema anaifunga kwa sababu tu ya kuchoka kupokea fedha, tutakimbilia wapi kama serikali? kwa nini serikali yetu nayo isianzishe kitu kama huko Egypt ambayo FB imepigwa marufuku au kama huko China wenye wechat au Russia wenye telegram?
Akili hiyo wanayo basi?. Wao wanacho jua ni kubambikiana maugaudi
 
Msemaji mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa ametoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu wakati serikali inawasiliana na makampuni ya WhatsApp, Facebook na Instagram kuhusu changamoto ya kukosekana kwa huduma ya mawasiliano ya mitandao hiyo.

Huduma za mitandao hiyo zilikwama kwa saa kadhaa tarehe 04 Oktoba 2021.

Taarifa hiyo ya wito wa serikali iliyotolewa usiku wa tarehe 4 Oktoba 2021 haikuwezekana kusambaa haraka kama ilivyo kawaida kwa kuwa mitandao hiyo ya kijamii haikuwa hewani.

Hata hivyo, baada ya juhudi mbalimbali za wataalamu huduma hizo zilirejea baadae usiku wa kuamkia tarehe 05 Oktoba 2021.

Kwa hatua hiyo serikali imeonesha kujali wananchi wake na kuthamini umuhimu wa mawasiliano. Pongezi kwa serikali.
View attachment 1964256

Huduma ilivyorejeshwa, msemaji mkuu wa serikali alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutaarifu kuhusu kurudi kwa huduma hiyo.
View attachment 1964500
Msigwa angepunguza camera ili atengeneze strategy ya serikali kuongea na wananchi hasa kwenye issues za messaging na kurelate closely na watu wa kawaida
 
Nasikia mdogo wangu MALCOM LUMUMBA ndie alipewa kazi ya kuwasiliana directly na Maki Zhakabharg.

Hongera mdogo wangu kwa kuongea na Youngest Dollar Billionaire!!

Halafu ningekuwa jirani na Gerson wakati anaongea hayo mambo, wallah ningemtia makofi!!
 
Msemaji mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa ametoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu wakati serikali inawasiliana na makampuni ya WhatsApp, Facebook na Instagram kuhusu changamoto ya kukosekana kwa huduma ya mawasiliano ya mitandao hiyo.

Huduma za mitandao hiyo zilikwama kwa saa kadhaa tarehe 04 Oktoba 2021.

Taarifa hiyo ya wito wa serikali iliyotolewa usiku wa tarehe 4 Oktoba 2021 haikuwezekana kusambaa haraka kama ilivyo kawaida kwa kuwa mitandao hiyo ya kijamii haikuwa hewani.

Hata hivyo, baada ya juhudi mbalimbali za wataalamu huduma hizo zilirejea baadae usiku wa kuamkia tarehe 05 Oktoba 2021.

Kwa hatua hiyo serikali imeonesha kujali wananchi wake na kuthamini umuhimu wa mawasiliano. Pongezi kwa serikali.
View attachment 1964256

Huduma ilivyorejeshwa, msemaji mkuu wa serikali alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutaarifu kuhusu kurudi kwa huduma hiyo.
View attachment 1964500
Vingine awe anakaa kimya, anajiabisha
 
Back
Top Bottom