Gerson Msigwa: Rais ameagiza kufunguliwa kwa Online TV tu na sio Vyombo vingine vya Habari

kauli ya rais namnukuu hapa
"nasikia kuna vivyombo vya habari mlivifungia sijui vile vi tv vya mkononi vifungulieni lakini wafate sheria"
 
Huu utawala mnauoverate

1.Agizo la kusitisha vifurushi limetolewa, lakini leo hii kuna mitandao bado haijabadili vifurushi na haijachukuliwa hatua zozote

2. Kauli ya kufungulia vyombo vya habari inatolewa, baadae eti tunaambiwa ni vijiTV vya mitandaoni tu

Sasa siku nyingine tuache kushangilia kauli kabla ya vitendo.

Huyu mama anatafuta kukubalika kwa maneno kwanza, tusiingie mtegoni mpaka tuone vitendo
 
UFAFANUZI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza Televisheni za Mtandaoni (Online TV) tu ndio zifunguliwe na SIO vyombo vya habari vingine yakiwemo magazeti vilivyofungiwa kwa mujibu wa Sheria.

Gerson Msigwa
Msemaji Mkuu wa Serikali
Asanteeee
 
Naam, ushauri murua kabisa
Ufafanuzi unaotelewa na msemaji wa serikali hauwezi kuwa wake lazima atakua amewasiliana na mtoa kauli ilikujiridhisha.
Sasa mkimlaumu mtoa taarifa mtakua mnalaumu asiehusika kabisa yeye ni mjumbe tu sio muamuzi.

Vyama vya siasa jIkiteni kwenye kudai katiba mpya mintarafu tume huru ya uchaguzi lasihivyo baada ya uchaguzi 2025 tutasikia malalamiko yaleyale wakati sasa mmejikita kwenye kusifia na kuzungumza hoja zisizo na msingi.
 
Msemaji wa serikali akitamka maana yake kapata ufafanuzi kutoka kwa mtoa kauli - rais wetu Samia. Hatamki ya kwake au uelewa wake, yeye ni mdomo wa serikali ya rais Samia
Madam President Samia,mbona watu wako hawaelewi wanachokisema.Ulizungumza kwa kiswahili fasaha na sanifu kuwa vyombo vya habari vilivyofungiwa ,vifunguliwe ili mradi tu wafuate sheria...
 
Nawasalimu kwa jina la JAMHURI
Ndugu zangu hili la kutafsiri kauli ya RAIS juu ya kufungulia vyombo vya habari baadhi na kuacha vingine linaleta DOUBLE STANDARD isiyo ya lazima.
Najiuliza shida ni nn? mbona aliongea vizuri nn kimebadilika? nani anataka kuhujumu dhamira njema ya Mh. RAIS?
Tunaposema yaliyopita sindwele tugange ya yajayo si ndo maana halisi ya kuvifungulia vyombo vya habari? au magazeti yalikua na case ya"kuua' ila online TV zilulikua na case ya "wizi wa kuku"?
Waziri BASHUNGWA anasema watu wamagazeti waende ofisini waangalie sheria iliyofunga magazeti case by case na kuona uwezekano kama yafunguliwe ama laaa, swali langu je ONLINE TV hazikufungiwa kwa mujibu wa sheria,kuna kigugumizi gani kwenye magazeti na kuna siri gani kwenye kufungulia online TV hadi kupelekea Mh.RAIS,KATIBU wa WIZARA ,Msemaji wa serikali na hatimae WAZIRI..kauli zao kukinzana kila mmoja?
Hisia zangu mama alipelekewa hoja juu juu kwa maslahi ya watu flani flani maana haingii akilini RAIS anaongea vizuri kesho tunasikia tena tafsiri za kukinzana.
mama anasema ......."wafungulieni wasipate kusema tunaminya uhuru wa habari" je kuendelea kufungia hayo magazeti dhamira ya mama itatimia ya watu kutoongea kwamba kuna kukandamiza vyombo vya habari?
Mama mbona alisema fungulieni ila wekeni kanuni zilizo wazi kwamba kosa hili adhabu yake ni hiii.....shida iko wapi kufungulia hayo magazeti na kuweka kanuni zilizo wazi kwa kila kosa.

Kwa nn tunapata kigugumizi? basi tuseme mama alimaanisha ivyo vi jionline TV kwani hawezi kushauriwa juu ya vyombo vingine vya habari...kwann KATIBU MKUU anajenga picha kwamba mama ashauriki ivyo tunasubiri kama kutakua na maelekezo mengine....Bw Bashungwa,Abbas na Msigwa mbona mnaonekana ni vijana kabisa inakuaje mna mawazo yasiyoeleweka? msaada wenu katika hii nyanja upo wapi? au bado mnaweweseka na msiba?
Acheni hizo bana TANZANIA ni yetu sote na kama kuna makosa kuhusu ivyo vyombo vya habari waelekezwe na vifunguliwe maana umo pia kuna ajira za watu....Tumsaidie Rais kwa dhati kabisa na si kutafuta njama za kumkwamisha na kuonekana hafai kwa sababu zenu binafsi.
 
Mkuu ukweli ni kwamba kuna watu wamepewa nafasi ila ni wajinga na hawatakiwi kuwepo ofisin unapozungumzia vyombo vya habari ni kwa upana wake yaani kuanzia Redio, TV, magazeti mitandao ya kijamii online TV na vyanzo vingine vya kupata habari, Sasa rais na watendaji wake wanapotoa maelekezo halafu wakawa wanasema ni online tv tu Yeye na wasaidizi wake watakuwa na shida maana lazima ajue je ni watu wangapi wana access ya online tv, ina maana kuna gepu mahala linakuwa limeachwa., mama samia tusizinguane:
 
Tangu lini Chadema wakaitakia mema ccm hadi wajipe kazi ya kumsifia rais Samia?.

Kazi ya kumsifia rais Samia ni ya MATAGA siyo ya chadema
Hii si awamu ya MATAGA, hii ni awamu ya MATHA ( Make Tanzania Happy Again)
 
Baada ya tamko la katibu mkuu wizara ya habari maelezo furaha za watanzania zimezimika ghafula kama mshumaa
Watanzani kimya!! kama vile wamemwagiwa maji baridi hawaamini kilichotokea mpaka sasa hivi...
Tutulie waziri kawaita wamiliki wa magazeti yaliyofungiwa
 
Mtahama nyie msio tahiriwa. Mijitu mizima mna magovi ya mwilini na akilini
Kwa hiyo Wahaya na Wanyakyusa pia Wajaluo wahame Nchi acha uzwazwa kila jamii ina mila na destuli zake acha kutulazimisha kufuata mila na destuli za kabila lako kupanga ni kuchagua bwasheeeee!!!!!
 
Kilichofanyika hapa, Rais katoa maagizo.. Alafu watekelezaji wanamhariri....

Amesema Vyombo vya Habari.... Alafu Abbas anasema TV za mitandaoni tu.....

Hii kitu imenichefua sana....
 
Rikiboy mambo yako ni kula tunda kumasihara huku wapi tena (jokes),

Abbas kakosea sana yaa kiufupi ameanza kupandisha mabega juu wakati huu si muda wa hayo mambo, pia watu waache kupalilia moto maana Mh Rais anaona na kusikia, hizi tabia za watz kuchongea watu ili wakose ajira hazina afya kabisa, wengi wanataka Abbas aondolewe sasa sijui akitoka wanafaidika na nini, kwanza yale si majukumu yake bali ni Msigwa
Aaha acha tu mkuu.. Haya nayo ni masiharaa kazini

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom