Gerson Msigwa, mwanahabari nguli, anaswa na mtego wa habari potoshi

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
332
1,000
Nimeshangazwa sana na Ndg. Gerson Msigwa kunaswa na mtego huu.

Sina hakika kama kafanya hivi makusudi akiwa anajua uhalisia, ama anajua huu ndiyo uhalisia.

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu na Sasa Msemaji Mkuu wa Serikali ameshindwa kuona kwamba hii video imetengenezwa tu kwa kuburudisha au, huenda, kupotosha? Ajabu!

Cha! Nimeishiwa nguvu. Sema nini, kila mtu huwa anakosea. Haijalishi cheo ama wadhifa.

Naona kafuta chap baada ya comments za wana. Ila raha ya teknolojia ndiyo hii – kumbukumbu inabaki. Naweka kumbukumbu sawa; ameposti hii leo tarehe 28 Agosti, 2021.

Asingefuta huenda angekuwa na room ya kubadili narrative. Lakini pia, kufuta kumeonesha kuwa kasanuka.

Takribani watu buku tuliiona hii posti.

Pointi yangu ni kwamba, hivi vitu vya mtandaoni ni vema ukajiridhisha kabla ya kuvidaka juujuu kwa unazi wa namna fulani. Hizi ni zama hatari.

Nadhani Gerson kajifunza jambo.

Video hii iliwahi kuletwa hapa jukwaani mwaka 2019 au 2020 ila kwa werevu wa Mods, ikanyofolewa.

Muhimu: Naambatanisha video na posts za Bwana Gerson hapa chini.


photo_2021-08-28_11-12-06.jpg

Gers 1.jpg

Gers 4.jpg
 

Toxic Concotion

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
2,679
2,000
Kupitia mambo kama haya ndio maana jamaa wa 'tuma kwa namba hii' hawaachi. Ni wazi Bw. Msigwa alishapigwa sana na jamaa design hiyo.

Hapa aliona fursa ya kujipatia umaarufu, kesho ungesikia yeye ndio alimvumbua mpaka wa TZ kumjua.

Ama kweli unaweza mtoa mwanakijiji kijijini lakini kamwe huwezi kutoa kijiji ndani ya mwanakijiji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom