Gerson Msigwa: Makubaliano ya kero za Muungano kuanikwa Septemba 18, 2021

Imajine wameshindwa kukubaliana kwa miaka 57 halafu wanafanikiwa ndani ya miezi 4. Kuna wa lakini mkubwa..... Wanajaribu kufurahisha Maza.
Naam,Naona majibu yamepatikana!Kero za Muungano zimetatuliwa!Zanzibar kalamba dume huku bara ikilamba galasa!
 
Vipi aliaanika hizo kero..hivi wa kuisemea Tanganyika ni nani katika hizi kero za muungano?

#MaendeleoHayanaChama
 
Jumapili ya Septemba 18, 2021 Serikali itaweka wazi kilichosainiwa na Mawaziri wa pande mbili za Muungano katika kutatua kero za Tanganyika na Zanzibar.

Ahadi hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumzia mipango ya Taifa leo alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dodoma.

Msigwa amesema siku hiyo atamuita mtaalam ambaye atajibu swali hilo moja kwa moja kutipia mitandao ya kijamii ili Watanzania wajue pande mbili zimesaini kitu gani kwani siyo siri.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali lililouzwa na mwananchi kwa njia ya simu akitaka kujua vitu gani vimesainiwa na pande mbili katika mkutano wao.

Hivi Karibuni Makamu wa Rais Dk Philip Mpango aliongoza kikao cha pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano kikilenga kupunguza changamotoza muungano ambazo zimedumu kw amuda mrefu.

“Swali zuri sana hili, lakini naomba nisimalize uhondo tusubiri siku ya Jumapili nitamleta mtaalamu hapa hapa atasimama na kutoa maelezo ya kina nini kimeuznguma na utekelezaji wake utakuwaje,” alisema Msigwa.

Msigwa amesema Tanzania imepania kumaliza migogo ambayo imekuwa ni kero kwa pande zote hivyo wananchi waendelee kuamini kuamini kuwa serikali yao iko kazini na mambo yanaendelea.
mh Rais atusaidie kuondoa makandokando yote ya yule mtu, tukiendelea kuyaona yanatukia kichefuchefu. awamu hii hatutaki iwe ya watu wanafiki, iwe ya watu genuine, sio waropokaji, sio wapenda sifa as if sisi wote ni watoto, iwe ya watu wasio wanafiki. sijasema mtu yeyote ni mnafiki hapa, ila kuna baadhi ya watu tunatakiwa tusiendelee kuwaona wakiwa kweney nyadhifa zozote zile kwasababu wanatutonesha vidonda. asante.
 
Waziri mkuu,Tulia,Msigwa,.........!
Hao wote ni wateuliwa wa mwendazake,au unamaanisha makandokando gani ya yule mtu?
 
Mimi. Bado nauliza kwenye meza ya mazungumzo ya kutatua kero za muungano nani alikua mwakilishi wa Tanganyika?

#MaendeleoHayanaChama
 
Mimi. Bado nauliza kwenye meza ya mazungumzo ya kutatua kero za muungano nani alikua mwakilishi wa Tanganyika?

#MaendeleoHayanaChama
Hayo mambo ni Siri!Unachotakiwa kufurahia bila kuhoji ni kwamba kero zimetatuliwa na SSH!
 
Kwenye mjadala uliopelekea hayo makubaliano nani aliiwakilisha Tanganyika??
 
Waziri mkuu,Tulia,Msigwa,.........!
Hao wote ni wateuliwa wa mwendazake,au unamaanisha makandokando gani ya yule mtu?
wala wanaweza kuwa sio hao. kuna aina fulani ya watu walikuwa wanafanya kazi kwa kujipendekeza na kwa masifa fulani kwasababu alikuwepo. waleeee, waliokuwa wanaamini yeye kuliko hata Mungu wale..ndio ninao maanisha. ujue kwenye maisha huwa sipendi unafiki kabisa, napenda mtu real. Pm NI REAL, hafeki. naongelea hawa vijana wadogowadogo hawa ambao walikuwa wanaimba mapambio halafu hata sasaivi bado wanazo zile elements za kuimba mapambio wakati maza hata hayuko huko.
 
Imajine wameshindwa kukubaliana kwa miaka 57 halafu wanafanikiwa ndani ya miezi 4. Kuna wa lakini mkubwa..... Wanajaribu kufurahisha Maza.
Eeeh, tatizo ni lipi migogoro ikimalizwa ndani hata ya siku moja na mama?
 
Jumapili ya Septemba 18, 2021 Serikali itaweka wazi kilichosainiwa na Mawaziri wa pande mbili za Muungano katika kutatua kero za Tanganyika na Zanzibar.

Ahadi hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumzia mipango ya Taifa leo alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dodoma.

Msigwa amesema siku hiyo atamuita mtaalam ambaye atajibu swali hilo moja kwa moja kutipia mitandao ya kijamii ili Watanzania wajue pande mbili zimesaini kitu gani kwani siyo siri.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali lililouzwa na mwananchi kwa njia ya simu akitaka kujua vitu gani vimesainiwa na pande mbili katika mkutano wao.

Hivi Karibuni Makamu wa Rais Dk Philip Mpango aliongoza kikao cha pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano kikilenga kupunguza changamotoza muungano ambazo zimedumu kw amuda mrefu.
Hawawezi kuweka hadharani.. itabaki kuwa siri kwa kuwa kuna upande mmoja umepigwa na kugaragazwa vibaya🙄
 
Back
Top Bottom