Gerson Msigwa: Makubaliano ya kero za Muungano kuanikwa Jumapili

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
896
1,000
Jumapili ya Septemba 18, 2021 Serikali itaweka wazi kilichosainiwa na Mawaziri wa pande mbili za Muungano katika kutatua kero za Tanganyika na Zanzibar.

Ahadi hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumzia mipango ya Taifa leo alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Dodoma.

Msigwa amesema siku hiyo atamuita mtaalam ambaye atajibu swali hilo moja kwa moja kutipia mitandao ya kijamii ili Watanzania wajue pande mbili zimesaini kitu gani kwani siyo siri.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali lililouzwa na mwananchi kwa njia ya simu akitaka kujua vitu gani vimesainiwa na pande mbili katika mkutano wao.

Hivi Karibuni Makamu wa Rais Dk Philip Mpango aliongoza kikao cha pamoja kati ya Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano kikilenga kupunguza changamotoza muungano ambazo zimedumu kw amuda mrefu.

“Swali zuri sana hili, lakini naomba nisimalize uhondo tusubiri siku ya Jumapili nitamleta mtaalamu hapa hapa atasimama na kutoa maelezo ya kina nini kimeuznguma na utekelezaji wake utakuwaje,” alisema Msigwa.

Msigwa amesema Tanzania imepania kumaliza migogo ambayo imekuwa ni kero kwa pande zote hivyo wananchi waendelee kuamini kuamini kuwa serikali yao iko kazini na mambo yanaendelea.
 

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,812
2,000
Hayo makubaliano yatakuwa yamaana kwa Tanganyika kama Zanzibar wataanza kuchangia gharama za muungano badala ya kulilia migao ya mapato na faida
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,476
2,000
Bila kushirikisha Wananchi wa pande zote mbili huu utakuwa ni UPUUZI MTUPU!!!
Rasimu ya Katiba ya Warioba ilishamaliza kila kitu kuhusiana na "kero za muungano". Hayo mengine maigizo tu funika kombe! CCM wanadhani wataendelea na hadaa zao hadi lini? Wakati ukuta!
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,780
2,000
Wanahangaika sana katika kuizima rasimu ya Warioba wahuni hawa.
Rasimu ya Katiba ya Warioba ilishamaliza kila kitu kuhusiana na "kero za muungano". Hayo mengine maigizo tu funika kombe! CCM wanadhani wataendelea na hadaa zao hadi lini? Wakati ukuta!
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,476
2,000
Wanahangaika sana katika kuizima rasimu ya Warioba wahuni hawa.
Ugaidi wa Mbowe ni kwa sababu ya Katiba ya Warioba. Badala ya kutafuta suluhu ya kudumu ya matatizo ya kitaifa ikiwemo kero za muungano wanaendeleza hadaa zao! Sijui hadi kizazi cha ngapi!
 
  • Love
Reactions: BAK

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
11,003
2,000
Hayo makubaliano yatakuwa yamaana kwa Tanganyika kama Zanzibar wataanza kuchangia gharama za muungano badala ya kulilia migao ya mapato na faida
Kumbuka maraisi wanao endesha nchi hizi mbili wana asili ya wapi? Ukijua hilo basi utajua hayo makubaliano yameibeba nchi gani kati ya hizo mbili
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,938
2,000
Haya mambo huwa siyaelewi kabisa
Kwanza area code ilibadilika au bado
Nasubiri mtaalamu huyo
Labda wakaomba Uraia pacha
 

KingCobra95

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,631
2,000
Uzeni nchi kbsa,kila rais wa nchi apewe fungu lake,,maana hizi sarakasi zinatupa fatigue😆
 

chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,032
2,000
Bila kushirikisha Wananchi wa pande zote mbili huu utakuwa ni UPUUZI MTUPU!!!
Umeniwahi apo... Nilitaka kuuliza wananchi wameshirikishwa wa pande zote mbili? Haya masuala si yanapelekwa kwenye mabunge? wanataka kutwambia kuwa wamekaa uchochoroni wamekubaliana afu wanakuja kutuhabarisha.
 
  • Love
Reactions: BAK

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom