GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Nakufahamu sana Kiutendaji hasa tokea ulipokuwa TBC na nadhani kama nikisema nitaje kati ya Maripota na Watangazi wenye Ueledi mzuri usio na shaka basi katika list yangu Gerson Msigwa hutokosa na ukiona hadi GENTAMYCINE anakukubali jua upo vizuri na utafanikiwa sana tu.
Kamarada Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Habari Ikulu nimekuwa nikiona ukifanya haya mapungufu mara kwa mara na hasa pale Mheshimiwa Rais anapokuwa anahutubia na nikadhani kuwa labda ulikuwa tu unapitiwa pengine kwa kutaka Sifa kwa Bosi wako Mheshimiwa Rais ili azidi kukuamini lakini baada ya kuona tena Kitendo kile kile umekirudia na leo tena ukiwa huko Mtwara ziarani nimeshawishika kulisema ili likufikie na ubadilike.
Kamarada Gerson Msigwa umekuwa na tabia ya kuingilia sana Majukumu ya Kiutendaji ya Watu wa PSU ( Presidential Security Unit ) ambapo mara kwa mara umeonekana na Wewe ukijifanya kuwa ni sehemu yao na kibaya zaidi kila mara ninapokuona unakuwa ni Mtu unayewakaripia hao Vijana huku ukitoa taratibu zote za Kiprotokali kitu ambacho nina uhakika nacho hukijui na wala hujakisomea na kama una uelewa nacho basi ni basic tu.
Nina uhakika kuwa hata hao Watu wa PSU huwa unawakwaza sema tu wanakunyamazia ila kwa ninavyowajua kuna siku uvumilivu utawashinda na watakupa Nakoz za maana tu ili ukome na uache kuwaingilia na kuwa na kiherehere.
Hivi Majukumu yako unayajua lakini? Gerson Msigwa ni lini :
Fanya tu yale ambayo umeajiriwa nayo na hayo ya masuala ya Kiprotokali tafadhali waachie wenyewe na ndiyo maana wenzako wameenda Vyuo mbalimbali kusomea na Wametukuka navyo hivyo wanajua wanachokifanya na Wewe uliyeenda kusomea Habari na Utangazaji pale TSJ ya Zamani au SJMC baki na Utendaji wako uliotukuka wa mambo hayo kwa kuwapanga tu vizuri Vijana wako wa Kurugenzi ya Habari wafanye Kazi zao huku Wewe ukitulia tu na kuangalia wanavyotenda na siyo kuzunguka zunguka tu hovyo huku ukiwa umekunja Uso utadhani huwa unagombana na Mtu.
Nimeumbwa kuwa mkweli na unafiki kwangu mwiko hivyo kama utalichuklulia bandiko hili ( uzi huu ) kwa hasira hutofaidika na chochote ila kama utayachukua haya halafu ukajitathmini na kujirekebisha nina uhakika utakuwa bora zaidi ya ulivyo sasa Kamarada Gerson Msigwa.
Jumapili njema na Majukumu mema pia.

- Umeruhusiwa kuwakagua Watu Rais anapowaita mbele?
- Umeruhusiwa kuhakiki Microphones za High Table Kijasusi?
- Umeruhusiwa kutoa maelekezo na kufoka foka hovyo kwa hao Jamaa wa PSU?
- Umeruhusiwa kuzunga zunguka hovyo ili mradi tu uonekane?
- Umeruhusiwa kumfundisha Mtu jinsi ya kuongea mbele ya Rais?
- Umeruhusiwa na Wewe kujifanya ni Mwana PSU?
- Umeruhusiwa kuwa na Mamlaka juu ya Watu wa PSU?