Gereza la mafisadi lijengwe kisiwani Mbudya

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
7,420
7,080
Kutokana na kasi ya kesi kubwa kubwa za mafisadi ni bora sasa kujenga gereza special kwa ajili yao kama ilivyo Guantanamo (magaidi) au Roben island (enzi za Mandela)
 
Wewe unaona nchi ina changamoto kibao za kupata pesa huku TRA wakikusanya pesa kidogo,huku MCC wakikataa kusaidia nchi kutokana na magumashi yaliyotokea,huku ELIMU BURE,huku wafanyakazi HEWA nk halafu wewe unataka MAFISADI wajengewe gereza lao (speacial) haya magereza yaliyopo hayana ubora wa kuitwa magereza kutokana na kuchoka vibaya.
Kwanza tangu Uhuru sijaona anayeitwa FISADI amefungwa nchi hii,labda vidagaa vya ufisadi.
"Binafsi sina hakika kama MAFISADI wapo nchi hii"
Fikiri mara mbii halafu upost au ucomment!!!


Kutokana na kasi ya kesi kubwa kubwa za mafisadi ni bora sasa kujenga gereza special kwa ajili yao kama ilivyo Guantanamo (magaidi) au Roben island (enzi za Mandela)
 
Hoja hii inataka ufikiri sana kung'amua busara yake. Mafisadi wapo ndo maana inaanzishwa mahakama maalum kwa ajili yao (si maneno yangu haya, nimenunua tu). Kwa busara ile ile ni bora kuwajengea magereza maalum kwa ajili yao (ikibid na familia zao).
Cc. Prince mstaafu.
BCc. Waziri wa zamani wa viwanja.
BCc. Waziri wa zamani wa umeme+Tanzanite.
BCc. Waziri wa zamani wa watalii.
 
Kwan gereza la karanga moshi limejaa... Gereza la keko limejaa... Gereza la bangwe kigoma limejaa....

Msituharibie pesa zetu watanzania kwa matumizi ya ovyo.... Kamata tupa hata porin kenge haooooo
 
Fikiria nchi chini ya Utawala wa Mzee Mamvi. Kina Siyoi ndo wangewekwa NSSF, mapachu=mambo ya nje,mboe=Waziri Mkuu, kuMBATIWA= fedha. Ingekuwa vurugu tupu.Dili zingepigwa asubuhi alfajir. MUNGU katuonea huruma asee
 
Kwanini serikali iingie garama ya kuwajengea gereza,hao wezi/mafisadi wanatakiwa wapelekwe ktk magereza ya kilimo huko ni kazi wanafanya mwanzo mwisho mpk watatia akili
 
Kama litajengwa gereza kwa ajili ya mafisadi pekee, basi litajazwa na wana CCM pekee, kama akina Richard Ndassa, Kangi Lugora, Mary Mwanjelwa, Mary Nagu na wengineo toka kwenye hicho chama ambacho kimekithiri vitendo vya rushwa.
 
Tuseme Dr. Mary ni mtuhumiwa wa kuchukua mlungula kwenye kamati? Tusubir wiki hii tuwaone pale Kisutu kwenye lile benchi maarufu
 
Ningekuwa mimi ningewafilisi na kuwaachia huru kuliko kupata tena shida ya kuwatunza na kuwahudumia wakati wa kifungo chao
Hiyo bajeti ya kujenga gereza na gharama za kuwatunza zielekezwe kwenye huduma nyingine muhimu za kijamii
 
Kutokana na kasi ya kesi kubwa kubwa za mafisadi ni bora sasa kujenga gereza special kwa ajili yao kama ilivyo Guantanamo (magaidi) au Roben island (enzi za Mandela)
Weee kule ni full bata unapiga kazi mchangani, wakajengewe au wakae huko huko na wenzao wale taabu
 
Kutokana na kasi ya kesi kubwa kubwa za mafisadi ni bora sasa kujenga gereza special kwa ajili yao kama ilivyo Guantanamo (magaidi) au Roben island (enzi za Mandela)
nitaomba nipewe kazi ya kuwasimamia na kuwa torture hadi wausahau ufisadi wao nitaenda na huko na pliers pilipili upupu nyuki siafu nk
 
Mkuu mbudya ipo karibu sana alaf usifananishe na Roben island,kwaza ubaya wa roben(seal kwa kidachi)kimezungukwa na hawa viumbe ambao ni chakula cha papa,kwa maana hyo kisiwa cha roben ukitoroka.ujue umeliwa na papa.Hivo basi kuna visiwa vingi tu kati ya Tanzania na Mauritius ambavo.mafisadi wanatunzwa bila kutoroka
 
Back
Top Bottom