Naomba kujuzwa Gereji nzuri ya kufanyia Diagnosis Dar es Salaam

kaka km

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
1,336
681
Wenyeji wa Dar naomba msaada wenu.

Gari yangu ina tatizo na nadhani watu wa Diagnosis wataweza kujua tatizo lake ni nini, huko mikoani nimeipeleka kwa mafundi wengi hawajagundua tatizo.

Gari ni Vanguard, ikiwa spidi ama gia ndogo kuanzia 0-30 inakua kama inashtuka, kama inataka kusimama ghafla ila kuanzia 40 kwenda juu haina tatizo. Yani ukiwa hiyo spidi utanotisi hilo tatizo mara chache chache. Hii inanikosesha furaha na amani.

Sasa niko Dar, naomba kufahamu gereji nzuri naweza kupata huduma. Nimeshauriwa toyota ila wale jamaa najua wana bei kubwa sana ingawa huduma zao pia ni uhakika, checkup tu ni karibu 300k kama sijakosea.

Natanguliza shukrani ndugu zanguni.

MREJESHO 9.7.2021.

Nawashukuru wote mliotoa ushauri wenu huku, nilibadili oil nikaweka ya CVT na lile tatizo limeisha kabisa.

Siku 2 za mwanzo baada ya kubadili oil nilikua nahisi lile tatizo mara moja moja ila baadae likaisha kabisa. Hii ni wiki ya 2 sijasikia tena lile tatizo.

Nawashukuru sana mlionipa ushauri. Mbarikiwe sana.
 
Ukiwa umesimama ila gear ipo kwenye D linatetemeka au linatikisika sana au?

Service history? Tatizo lilianza lini?

Hafu gereji nyingi diagnosis Bure ila unafanya service kwao.
 
Kama umenunua gari kwa zaidi ya 25m mbona jiwe 3 ni ndogo kupata huduma ya uhakika?
Mkuu na mimi hapo ndo waswahili wenzangu wananishinda. Ananunua gari mpaka ya million 100+ lakini kwenda CFAO a u Toyota afanye service ya uhakika ni ngumu sana.

Sana sana atakwambia kwamba fundi wangu yupo Pugu na anafanya kazi CFAO. Na wabongo tulivyo na akili nyingi..huyo huyo fundi wa Toyota ukimpelekea gari yako aitengeneze chini ya mwembe....ni changamoto sana.
 
Ukiwa umesimama ila gear ipo kwenye D linatetemeka au linatikisika sana au?

Service history? Tatizo lilianza lini?

Hafu gereji nyingi diagnosis Bure ila unafanya service kwao.
Hapana, kustuka kama inataka kusimama ghafla ni kwenye gia ndogo tu ama spid ndogo. Binafsi nahisi labda inamis gia ndogo ama namna gani.

Services inafanyiwa on time.
 
Mkuu na mimi hapo ndo waswahili wenzangu wananishinda. Ananunua gari mpaka ya million 100+ lakini kwenda CFAO a u Toyota afanye service ya uhakika ni ngumu sana. Sana sana atakwambia kwamba fundi wangu yupo Pugu na anafanya kazi CFAO. Na wabongo tulivyo na akili nyingi..huyo huyo fundi wa Toyota ukimpelekea gari yako aitengeneze chini ya mwembe....ni changamoto sana.
Mkuu tunakimbia gharama.

Huyo fundi mtaani hana service charge, akikukagulia gari anakwambia tatizo na kama huna hela ya kutengeneza wakti huo utampa hela ya supu tu haizidi 30k, CFAO ana Toyota check up tu bila matengenezo ni 250k, hiyo ni gharama ambayo ukimpa huyo fundi atengenezee kwenye muembe inatemgemaa na hela ya supu inabaki.

Watu tunachokwepa ni kununua chips kuku 25k wakati unaweza kuipata kwa 5k.
 
uko sawa mkuu,watu hawajui gari umeipataje na uwezo wa mfukoni kwa kipindi hiki tunatofautiana,nimeshuhudia watu wamepaki gari ndogo kama ist na vitz,na wengine wametelekeza ccm,hela ya yard imekuwa ngumu...
 
Wenyeji wa Dar naomba msaada wenu.

Gari yangu ina tatizo na nadhani watu wa Diagnosis wataweza kujua tatizo lake ni nini, huko mikoani nimeipeleka kwa mafundi wengi hawajagundua tatizo.

Gari ni Vanguard, ikiwa spidi ama gia ndogo kuanzia 0-30 inakua kama inashtuka, kama inataka kusimama ghafla ila kuanzia 40 kwenda juu haina tatizo. Yani ukiwa hiyo spidi utanotisi hilo tatizo mara chache chache. Hii inanikosesha furaha na amani.

Sasa niko Dar, naomba kufahamu gereji nzuri naweza kupata huduma. Nimeshauriwa toyota ila wale jamaa najua wana bei kubwa sana ingawa huduma zao pia ni uhakika, checkup tu ni karibu 300k kama sijakosea.

Natanguliza shukrani ndugu zanguni.

Kwenye gari yako, ukifungua mlango wa mbele wa abiria, kwente frame ya gari, kuna kibati kina taarifa za gari kama hiki hapa chini.

IMG_20210613_181325.jpg

Hiyo namba niliyoipigia msitari mwekundu kwa chini naomba uipost hapa au picha kibati chote post hapa.

Naweza nikawa na cha kukusaidia.
 
Okay hiyo ni gearbox ya CVT.

Anyway hiyo ni gearbox ya gear 6 CVT.

Kwa maelezo yako mwenyewe ni kwamba hilo tatizo linatokea kwenye speed ndogo.

I suspect ni tatizo linalohusiana na gearbox.
Okay. Basi ngoja nikaicheki.

Ahsante kwa ushauri na muda wako mkuu.
 
Mkuu na mimi hapo ndo waswahili wenzangu wananishinda. Ananunua gari mpaka ya million 100+ lakini kwenda CFAO a u Toyota afanye service ya uhakika ni ngumu sana.

Sana sana atakwambia kwamba fundi wangu yupo Pugu na anafanya kazi CFAO. Na wabongo tulivyo na akili nyingi..huyo huyo fundi wa Toyota ukimpelekea gari yako aitengeneze chini ya mwembe....ni changamoto sana.
Kuna boss mmoja alipeleka gari CFAO akaletewa invoice milioni 40, ilikuwa ni E-class kainunua milioni 45🤣
 
mkuu kwaharaka haraka na kwa uzoefu wangu hapo gearbox ndio anaanza kuwa bye bye na mara nyinyi wenye magari ndio mnaziua bila shaka gari yako gearbox yako ni ya CVT sasa wengi wenu niwabishi mnaweka oil ya kawaida hapo ndio shida huanza na itaendelea hivyo mwishowe kwa style hiyo itakata chain..

lkn vizuri kuipima
 
Hapo chain ya zile puley mbili imeanza kuteleza so ina malfunction kutokana na kuwekewa fluid isiyo yake.

Oil ya CVT ipo tofauti na hizi za kawaida na material yake yanaifanya kuifanya chain ile kufanya kazi vema kisawa sawa.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom