Gereji na oil nzuri kwa Nissan Dualis

Tebajanga

Member
Sep 14, 2011
68
102
Habari wakuu.

Ninatarajia kuchukua Nissan Dualis. Napenda kujua ni oil zipi (Brand na vipimo) na ni gereji ipi kwa hapa Dar es Salaam wana mafundi wazuri wa Nissan?

Pia kuna uzi niliusoma unasema oil ya engine inabidi iwe 5w 30, je kuna ukweli kuhusu hilo?

Na oil ya transmission, gearbox oil inabidi kuweka ipi? (Brand na vipimo)

Pia nimesikia kuwa si vizuri kuweka maji ya bomba kwenye rejeta, je maji yapi yanafaa?

Kwa wale wanao miliki Nissan Dualis, mnaweza mkashare njia mbalimbali mnazozitumia kutunza ubora wa gari na injini?

Swali la nyongeza, ni vizuri gari litakapofika kutoka Japan nilifanyie service kabla ya kuanza kulitumia? Kama ndio ni services zipi za muhimu?

Natanguliza shukrani.
 
Kuna fundi mmoja mtaalam sana wa magari alinishauri kitu akaniambia achana na hizi nissan, akanisistiza endelea na toyota ukichoka hamia kwenye European Car.

Nimeandika kama kibwagizo, gereji nzuri ni pale kwa Jerry mikocheni kama unaelekea Kairuki hosp, ukifika wao wataikagua gari na kukwambia nini kinatakiwa kubadilisha.
 
Kuna fundi mmoja mtaalam sana wa magari alinishauri kitu akaniambia achana na hizi nissan,akanisistiza endelea na toyota ukichoka hamia kwenye European Car.Nimeandika kama kibwagizo,gereji nzuri ni pale kwa jerry mikocheni kama unaelekea kairuki hosp,ukifika wao wataikagua gari ni kukwambia nini kinatakiwa kubadilisha

Asante king90, fundi wako alikuambia sababu zipi uachane na gari za Nissan?
 
Asante king90 , fundi wako alikuambia sababu zipi uachane na gari za Nissan?
Mkuu, bila shaka umefanya uchunguzi wa kutosha kuhusu hiyo gari. Sina uhakika kama taarifa ni za ukweli lakini nasikia Dualis ni pasua kichwa

Kuna fundi mmoja mtaalam sana wa magari alinishauri kitu akaniambia achana na hizi nissan,akanisistiza endelea na toyota ukichoka hamia kwenye European Car.Nimeandika kama kibwagizo,gereji nzuri ni pale kwa jerry mikocheni kama unaelekea kairuki hosp,ukifika wao wataikagua gari ni kukwambia nini kinatakiwa kubadilisha
Huyu fundi wako naye ana shida, Nissan ni hazina shida yeyote.
 
Dualis tumia engine oil yenye viscosity ya 5w30 tu mkuu..

Dualis tumia genuine coolant

Dualis tumia genuine transmission fluid tu..kama ni ya cvt itakuwa NS2au NS3...kama ni automatic ya kawaida soma deep stick wamependekeza kitu gani..

Dualis ina tatizo sugu la kushuka kwa roof la ndani...hii siyo issue...inatengenezeka..

Otherwise matunzo mengine hayajaachana sana na xtrail...

Wanaosema ni kimeo hawana hela za kuhudumia hiyo gari....au hawana tabia ya utunzaji..
 
Habari wakuu.

Ninatarajia kuchukua Nissan Dualis. Napenda kujua ni oil zipi (Brand na vipimo) na ni gereji ipi kwa hapa Dar es Salaam wana mafundi wazuri wa Nissan?

Pia kuna uzi niliusoma unasema oil ya engine inabidi iwe 5w 30, je kuna ukweli kuhusu hilo?

Na oil ya transmission, gearbox oil inabidi kuweka ipi? (Brand na vipimo)

Pia nimesikia kuwa si vizuri kuweka maji ya bomba kwenye rejeta, je maji yapi yanafaa?

Kwa wale wanao miliki Nissan Dualis, mnaweza mkashare njia mbalimbali mnazozitumia kutunza ubora wa gari na ingini?

Swali la nyongeza, ni vizuri gari litakapofika kutoka Japan nilifanyie service kabla ya kuanza kulitumia? Kama ndio ni services zipi za muhimu?

Natanguliza shukrani.
Tafuta Manual ya hiyo gari ujue nini kimekuwa recomended kuweka.
 
Dualis tumia engine oil yenye viscosity ya 5w30 tu mkuu..

Dualis tumia genuine coolant

Dualis tumia genuine transmission fluid tu..kama ni ya cvt itakuwa NS2au NS3...kama ni automatic ya kawaida soma deep stick wamependekeza kitu gani..

Dualis ina tatizo sugu la kushuka kwa roof la ndani...hii siyo issue...inatengenezeka..

Otherwise matunzo mengine hayajaachana sana na xtrail...

Wanaosema ni kimeo hawana hela za kuhudumia hiyo gari....au hawana tabia ya utunzaji..
Xtrail nikitumia engine oil 20w-50 Kuna ubaya?
 
Kwa Nissan Dualis tumia oil ya Castro 5W~40, maji ya wiper usitumie yenye chlorine ya DAWASA, yanaweka punjepunje fulani nyeupe baadae inafanya tundu za wiper zizibe, tumia maji ya chupa atlist kwa mwaka 1 bajeti ikibana rudi na maji ya dawasco
 
Hiyo oil 5W-40 mbona Kama sio iwa Dualis inayotumika nchi za joto?
 
Attachments

  • maslo-dlya-nissan-xtrail.jpg
    maslo-dlya-nissan-xtrail.jpg
    11.2 KB · Views: 46
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom