Gerala Hando wa Clouds Radio anajipendekeza kwa JK na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gerala Hando wa Clouds Radio anajipendekeza kwa JK na CCM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jatropha, Sep 22, 2012.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Jana katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa hewani na Clouds Radio mtangazaji Gerald Hando alikuwa akijipendekeza kwa JK na na CCM kwa kuwamwagia sifa kibao kwa miradi mbali mbali ya barabara zinazojengwa na kuwekwa mawe ya msingi hususan barabara ya Bagamoyo-Msata na mradi wa mabasi yanayoenda kasi.

  Kilichonishangaza ni kitendo cha mtangazaji mwenye heshima kubwa kama yeye kujipendekeza kiasi kile ilhali ni wazi kuwa miradi kama hii ni "long overdue". Ilitakiwa Serikali amabyo iko makini kuwa na "urban master plan" kupima viwanja katika surburbs zote za majiji yote ya nchi hii (maeneo yaliyoko pembzoni mwa jiji) kujenga miundo mbinu kama vile barabara za lami ikiwemo "flyovers" ,mtandao wa maji safi na maji taka na mtandao wa nishati ya umeme kabla ya kuruhusu wananchi kuanza ujenzi wa makazi katika maeneo hayo na kuhamia huko.

  Kitendo cha serikali ya CCm kushindwa kufanya hayo mapema ni udhaifu mkubwa na ndio unaopelekea majiji yote katika nchi hii kukubwa na msongamano wa magari, watu kukosa maji safi ya bomba ilihali nchi hii ina vyanzo mbali mbali vya maji ikiwemo mito, maziwa na maji yaliyo ardhini na watu kukosa nishati ya umeme ilihali nchi hii imejhaaliwa vyanzo mbalimbali vya nishati hiyo ikiwemo maporomoko ya mji. gesi, maka ya mawe, uranium na petroli.

  Ni ajabu sana kuona mtangazaji mweny heshima kubwa najipendekeza katika kidogo kinachofanyika tena kutokana na msukumo wa wapinzani. Na kidogo hicho hakina uwianao na raslimali za nchi hii zinzoporwa. Ni dhahiri kuwa kama Serikali ya CCM na Mkapa na JK wangekuwa makini matatizo ya miundo mbinu ya barabara, maji safi ya na nishati ya umeme nchi nzima sasa yangekuwa historia katika utawala wa miaka 20 ya Mkapa na Jk

  Ni kutokana na CCM na watawala kufahamu kuwa wapo wapumbavu kama akina Gerald Hando katika nafasi nyeti za uelimishaji wa umma ndio maana wanafanya sherehe kubwa za uwekaji majiwe ya msingi mapya kabla ya kukamilisha miradi ya ujenzi wa barabara ambayo ilikuwemo katika bajeti ya 2011/12 amabpo wizara ya ujenzi ilipatiwa 40% tu ya fedha ilizotengewa na wakandarasi wa miradi mbali mbali ya barabara kulazimika kusimamisha kazi hizo na kuidai Serikali fedha zaidi kuliko ilivyotarajiwa.

  Kwa mtindo huu wa Serikali ya CCm na Jk kushindwa kufikisha fedha zilizotengwa kwa wizara husika tuna uhakika gani kuwa miradi hii inayowekewa mawe ya msingi sasa itakamilika ipasavyo? Ni kutokana na utaratibu huo ndio maana barabara ta Bagamoyo-Masata aliyoisifia Gerala Hando imefunguliwa pasipo kukamilika madaraja, haijawekewa alama za barabara na miundo mbinu mingine kuwezesha barabara kuweza kukabidhiwa.

  Nilitegemea investigative reporter kama anavyojiita Gerald Hando kujiuliza na kutafiti iweje barabara hii ikafunguliwe kabala ya kukamilika badala ya kutupigia propaganda katika redio.

  Nilitegemea mwandishi wa mwenye heshima kubwa kama Gerald Handio na kituo bora cha redio kama Clouds kiwaelimishe wananchi hususan vijana kinachojidai ndio wateja wake wakuu kuhusu athari za ufisadi wa kutumia fedha fedha za pensheni za uzeeni wa wafanyakazi kujenga barabara ya Kigamboni badala ya dhababu zetu za kiasi cha Bilioni 10 kwa wiki zinazooporwa na wazungu kwa ruhusa ya CCM
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Only time will tell, ni tatizo la makanjanja hilo wala sishangai!!!
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Nimeacha kusoma hii thread yako pale tu uliposema Gelard Hando ni mmoja wa Watangazaji wenye heshima kubwa!! hizi ni pumba tupu unazotuletea hapa.
   
 4. mak89

  mak89 JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 974
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 80
  Jatropha Nani kwa kuambia gerald hando mwandishi? Yule dogo hana taaluma ya uandishi hata kidogo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Unahangaika na mapunga hayo
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mhhhhh!!!!! Hivi Yule mropokaji mwenzake anajua siku hizi zile dozi anazopiga zimeingia na feki pia?
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  How trained is he? Na ni yeye mwenye tatizo au mfumo wa uendeshaji wa kampuni aliyoajiriwa ndio unatoa mwongozo afanye nini?
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Ina maanisha nini hii? Wengine tumezaliwa Nachingwea. Mjini tumekuja tukusindikiza mwenge
   
 9. K

  Kamura JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watu bwana! kumbe kuzungumza hata zuri moja analofanya Rais na Serikali ni ujinga? mbona Serikali imefanya mambo mengi mazuri sasa ibezwe kwa lipi?
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  CCM si hupeana vyeo kwa kujipendekeza..... Hayo ndio maisha yao
   
 11. B

  BigMan JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  acheni watu wafanye kazi,hiyo ni ahadi ya tangu uhuru kama jk kaweza kuifanikisha na ni kitu kinachooneka watanzania twapaswa kumsifia,hando hana kosa katimiza jukumu lake tusiwe na wivu wa kijinga kwa kufikiri kuwa kikifanyika kitu ni kuisaidia ccm,bt jk alitoa ahadi watu wakakemkejeli kwamba hataweza na siku za karibuni amesema anzeni kuhesabu moja baada ya nyingine,sasa kama ameanza kosa la hando ni lipi ? jamani tusifike huko mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,hap jf tusiwe watu wa kupinga kila kitu tu kwa kuwa tunataka kuipinga serikali
   
 12. mak89

  mak89 JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2012
  Messages: 974
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 80
  Eti mhariri mkuu kibonde utegemea nn hapo
   
 13. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Lakini wadau,inamaana hizo barabara bado tunaona hazina msaada kwa taifa letu?
  Sina chama,ila ni vyema tukawa wepesi kukubali kile kizuri kinachofanywa na serikali,kuwa upinzani sio kupinga kila jambo,
  swali je barabara hizo zinazojengwa huko dsm hazitakuwa na msaada kwa taifa letu? Na vipi kuhusu lile daraja la kigamboni?
  Kikawaida huwa hivi
  leo ccm ipo madarakani,kila lifanywalo tutaliona si lolote,kesho chama kingine kitakuwa madarakani na tutasema na kuona hivyo hovyo.sasa waswahili wanasema huwezi kumlidhisha kila mtu ktk hii dunuia,mfano mzuri ni ktk familia tutokazo,hatuwezi kuwaridhisha wanafamilia wote,utafanya jema lakini baadhi ya wanafamilia wataona ni baya na wengine wataona ni jema
  tuwe wepesi kukubali kwa yale tuonayo ni mema kwa taifa letu
   
 14. B

  BigMan JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  angekuwa mutabuzi ama kichaa nyaronyo kicheere ama jerry muro kwa kuwa ameonyesha nia ya kujiunga na cdm mngewaita wapiganaji makamanda,tunaelekea kusiko watanzania tubadilike,tukubali kusifia na kukosa
   
 15. B

  BigMan JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,097
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  ebu chungulia upange wa pili wa shilingi vipi kwa cdm nako vyeo vyao vikoje ? baba na mchumba wake,babu na mkwe wake,kaka na dada yake na jirani na jirani mwenzake
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Serikali inatimiza wajibu wake propaganda za kuwasifia za nini? Hata hivyo jhayo yanayofanyika ni long overdue na hayaendani na raslimali serikali hiyo hiyo inazoruhusu kutoroshwa nje.
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Tunachosema hapa hayo yanayofanyika yanalingana na kiwango cha raslimali za nchi yeey kama rais anazosimamia kutoroshwa nje ya nchi? Ni wazi kuwa kinachofanyika ni peanuts ukilingnsiha na kiwango cha raslimali za nchi anazohusika na utoroshwaji wake akiwa kama rais.
   
 18. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Mwenzio anasaka UDC huko Nyasa
   
 19. akohi

  akohi JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 761
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 60
  Binafsi napata sana shida kusikiliza vipindi vya mawingu, bora zamani enzi za akina kipanya na fina. Siku hizi ni buuuureeee kabisa
   
 20. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160

  Kuna faida gani ya kutumia raslimali kubwa kujenga barabara halafu wanasiasa wachache wa CCM kutumia maelfu ya malori yao kuvivunja kutokana na kuiua reli zilizopo hapa nchini kuuawa kimkakati? Kuhusu daraja la Kigamboni hoja hapa ni kwanini Serikali hii isimamie utoroshwaji nje wa dhahabu yetu takriabini ya kais cha Bilioni 10 kila iwiki halafu iwapore wafanyakazi mafao yao na kuzitumia kujenga daraja hilo?
   
Loading...