GEPF kufufua Kilimanjaro Machine Tools kwa bilioni 1.6

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Mfuko wa Mafao ya Kustaafu (GEPF) unatarajia kutoa sh 1.6 Bil awamu ya kwanza kwa ujenzi wa kinu cha kufua chuma katika kiwanda cha kutengeneza vipuri vya viwandani cha Kilimanjaro Machine Tools.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya GEPF, Joyce Shaidi, alisema uamuzi wa kutoa fedha hizo unaotokana na kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli la ujenzi wa viwanda.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa juzi ikiwa ni sehemu ya mkutano mkuu wa nane wa mwaka wa mfuko huo utakaofanyika kwa siku mbili leo na kesho.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji anatarajiwa kufungua mkutano huo.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom