Georgia: Waziri Mkuu ajiuzulu akipinga kukamatwa kwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Waziri Mkuu wa Georgia amejiuzulu leo kufuatia mpango wa kumkamata kiongozi mmoja mkuu wa upinzani. Giorgi Gakharia amesema kukamatwa kwa kiongozi huyo Nika Melia, huenda kukauzidisha mzozo wa kisiasa katika nchi hiyo ya zamani ya Sovieti.

Hapo jana mahakama moja ya Georgia ilitoa uamuzi wa kumuweka kizuizini Melia hata kabla kusikilizwa kwa kesi yake.

Kiongozi huyo wa upinzani huenda akapewa kifungo cha hadi miaka tisa jela iwapo atapatikana na hatia ya "kupanga machafuko" wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mwaka 2019. Ameyakanusha madai yote hayo yanayomkabili akisema yamechochewa kisiasa.

Georgia imekumbwa na mzozo wa kisiasa tangu uchaguzi wa bunge mnamo Oktoba ambao ulipingwa na upinzani uliodai kulikuwa na udanganyifu. Chama tawala cha Dream Party kilidai kushinda.


Muungwana
 
Back
Top Bottom