Georgia Mtikila: Hatujui Rais Magufuli anakotupeleka, Mtikila angekuwa hai angemfungulia mashtaka

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
19,712
Points
2,000

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
19,712 2,000
Mke wa marehemu Mchungaji Christopher Mtikila, aliyefariki dunia Oktoba 4, mwaka juzi, Georgia Mtikila, amevunja ukimya na kuzungumzia jinsi anavyoteswa na kesi tatu zilizoachwa mahakamani na mumewe.

Mtikila alifariki kwa ajali ya gari iliyotokea Kijiji cha Msolwa mkoani Pwani akiwa anatokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili katika ofisi za Chama cha Democratic (DP) zilizopo Mchikichini, Ilala Dar es salaam katikati ya wiki, mjane huyo alisema hadi sasa hafahamu hatima ya kesi hizo kutokana na kuahirishwa mara kwa mara.

"Kesi zile alizoziacha, hasa alizokuwa anashughulika kwa kuwasaidia watu, nisingeweza kuziendesha. Lakini zilizokuwa na mawakili, mimi kama msimamizi wa mirathi nimeendelea nazo na hakuna hata kesi moja ambayo imekwisha, bado zinaendeshwa na mawakili.

"Kesi zinanitesa kwa sababu yeye alivyokuwapo zilikuwa zinaendeshwa haraka, sasa hivi zinaahirishwa tu hatujui zitaisha lini. Zinanitesa, lakini namshukuru Mungu ananitia nguvu na kwa sababu kuna mawakili", alisema.

MWENENDO WA SIASA

Kuhusu utawala wa Rais Dkt. John Magufuli na mwenendo wa siasa hapa nchini Georgia alisema: "Hatujui anakotupeleka, mimi ni Mwanasiasa, rais anapoingia na kuzuia mikutano ya hadhara, akazuia wananchi kukutana na kuzungumzia mambo yao, nina wasiwasi sana na jinsi siasa itakavyokwenda kwa sababu siasa ni kuzungumza, siasa ni kutoa maoni.

" Mkizibwa maoni tena kwa lazima na aliyezungumza ni mkuu wa nchi, tafsiri yake ni sheria, ndiyo maana hatujui maisha ya siasa yatakuwaje ukizingatia Uchaguzi Mkuu ni mwaka 2020. Sielewi itakuwaje",

MIGOGORO CUF, DP

Pia alizungumzia mgogoro unaofukuta ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) ukihusisha kambi mbili za Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini na Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Georgia, alisema mgogoro pia upo ndani ya DP huku akimnyoshea Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi, kuwa chanzo.

"Sisi tuna mgogoro mkubwa sana, usione tunanyamaza, msajili anataka kutufanya kama CUF anavyoifanya. Mgogoro wa CUF tunawaonea huruma, lakini tutawasaidiaje? Hatuwezi kuwasaidia kwa kuwa vyama vyetu havina utamaduni wa kusaidiana, tumekuwa kama kuku wa kienyeji, kuku anachinjwa pale, huyu anakula mchele hapo akingojea kisu chake", alisema

Kutokana na hali hiyo, alisema kama Mchungaji Mtikila angekuwapo hai angekwenda mahakamani kulalamika suala la kuzuiwa kwa mikutano hata vikao vya ndani vya vyama vya upinzani.

Chanzo: Mtanzania
 

heavyload

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2017
Messages
840
Points
500

heavyload

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2017
840 500
Katiba mpya ndo muarobaini wa hili jinamizi si vinginevyo. Kama uhakiki wa watumishi tu unachukua miaka mitatu vipi kuhusu kushughulikia wezi. Tusipoangalia tunawachia vizazi vijavyo majanga yasiyo yao kwakuwa kila anayekuja anakuja na mipango na agenda zake. Nchi haina dira tunaimbaimba tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,381,732
Members 526,184
Posts 33,810,262
Top