George Wajackoyah: Nitakuwa Rais wa kwanza barani Afrika kuhalalisha Bangi

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,923
13,344
Wakili maarufu, George Wajackoyah, amezua gumzo hivi karibuni nchini Kenya. Hii ni baada ya kujitosa rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kugombea kiti cha urais, kwenye uchaguzi mkuu, baadaye mwakani. Alipoibuka na moja ya sera yake ya kipekee, alipozungumza na wanahabari jijini Nairobi. Wajackoyah aliahidi kwamba atahalalisha matumizi, uuzaji pamoja na upanzi wa mmea nyeti wa bangi. Iwapo wakenya watamchagua kuwa rais wao.

Aliongeza kwamba mmea huo una uwezo mkubwa mno wa kuwa kitega uchumi cha kutajika nchini, hususan kwenye sekta ya kilimo. Huku akidai kwamba waafrika walihadaiwa na mkoloni kwamba mmea huo haufai. Kwa faida ya mkoloni kwenye biashara yake ya vilevi na sigara. Ambazo alisema zina madhara chungu nzima na wala hazina hata chembechembe za manufaa yeyote, zikilinganishwa na bangi.

Wajackoyah alidai kwamba mafanikio ya matumizi ya bangi, kama tiba ya baadhi ya mangonjwa sugu ni kichocheo tosha, cha kufikia uamuzi wa kuhalalisha mmea huo. Huku akieleza pia kwamba akiwa rais atatekeleza mikakati kabambe ya kuhakikisha kwamba Kenya itaifaidi sana kiuchumi. Sanasana kwenye biashara ya kimataifa('exports') ya mmea huo.
Kura mnazo wadau? Vote for my Nigga George, genius without a doubt!
Kenya: I Will Be the First President in Africa to Legalise Marijuana, Wajackoyah Says

 
Back
Top Bottom