George Mpole amka la sivyo utapotea

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
George Mpole wewe ni kijana uliyevimba kichwa baada ya kuwa mfungaji bora msimu uliopita.

Picha lilianza mechi ya kwanza ya ligi shidi ya Simba, wewe ukajificha kwa makusudi eti hautakuwepo kwa maana eti utokee dakika za mwisho kama 'suprise' kwa Simba na bado hukufanya chochote, hata :shot on target'!

Wenzako wanasafiri kimataifa wewe unajifanya unaumwa ukaacha kwenda! Haya, kwasasa nasikia umejitoa kwenye timu eti kuna pesa unadai!

Hivi hapo Geita ni wewe peke yako tu unadai? Mbona unajifanya maarufu kabla hata ya umaarufu wenyewe?

Kwa akili zako ndogo na finyu unadhani dirisha dogo unaweza kwenda Simba au Yanga? Kwa taarifa yako hata Ihefu huwezi kwenda!

Rudi ongeza bidii kwenye timu, kama ipo ipo tu lakini siyo huku kulazimisha umaarufu, utakuja kuumbuka. Au kama una pasi ya kusafiria na viza nenda Uarabuni ukacheze ligi daraja la pili huko.
 
George Mpole wewe ni kijana uliyevimba kichwa baada ya kuwa mfungaji Bora msimu uliopita!
Picha lilianza mechi ya kwanza ya Ligi vs Simba wewe ukajificha Kwa makusudi eti hautakuwepo Kwa maana eti utokee dakika za mwisho kama sapraisi Kwa Simba na Bado hukufanya chochote hata shoti on target!

Wenzako wanasafiri kimataifa wewe unajifanya unaumwa ukaacha kwenda!
haya kwasasa najisikia umejitoa kwenye timu eti Kuna pesa unadai!
hivi hapo Geita ni wewe peke yako tu unadai?
mbona unajifanya staa kabla hata ya ustaa wenyewe?

Kwa akili zako ndogo na finyu unadhani dirisha Dogo unaweza kwenda Simba au Yanga,
Kwa taarifa Yako hata Ihefu huwezi kwenda!
Rudi ongeza bidii kwenye timu kama ipo ipo tu lakini sio huku kulazimisha ustaa utakuja kuumbuka..
Au kama una passport na viza nenda uarabuni ukacheze Ligi daraja la pili huko..
Jimama la Tabata Kimanga alilolipata limeshampotezea Dira yake ya Kucheza Soka na ndiyo ameshapotea hivyo.
 
Kuna namna mbalimbali za kudai haki, yeye kachagua mgomo na yupo Sawa. Sasa bila kulipwa atakula nini na familia yake?
 
Ni yeye peke yake anadai hapo Geita?
Kila Mtu ana Majukumu yake na Michongo yake, inawezekana wengine hawadai ila wana vyanzo vingine vya Mapato ila kwake yeye anategemea Pesa hizo hizo na familia inamtegemea pia
 
Huo ufungaji Bora wa Tff waliomzawadia unaenda kuua ka-kipaji kake kote!!. Na asikifirie kabisa kama anaweza hata pata usajiri yanga au Simba coz hizi ndizo timu zenye malimbikizo ya madeni hasa kwa walichezaji wa ndani, huo mgomo wake pekee yake unaonesha kiasi gani alivyo zuzu.
 
Kila Mtu ana Majukumu yake na Michongo yake, inawezekana wengine hawadai ila wana vyanzo vingine vya Mapato ila kwake yeye anategemea Pesa hizo hizo na familia inamtegemea pia
Kama anawadai, basi Yuko sahihi. Ila anachokosea ni njia aliyotumia kudai hiyo haki yake,maana anajiumiza yeye. Kama ingekuwa ndio effective way ya kudai chake, basi angekuwa ashapewa.

Benchi linaua sana viwango vya wachezaji. Anaumia yeye.
 
Back
Top Bottom