George Mkuchika waziri wa utawala bora janga jingine hili.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

George Mkuchika waziri wa utawala bora janga jingine hili....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bushman, May 22, 2012.

 1. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,302
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli hawa mawaziri wa tanzania sijui wanaishi miongoni mwa jamii za kitanzania au wamekuja kwa mkataba kuafanya kazi na kuondoka huyu waziri yuko mikoa ya kusini kwenye ziara zake huko,kuna kauli alinukuliwa na vyombo vya habari (tbc 8:00pm) juzi akisema;
  1. walimu wote wakuu waliofaulisha wanafunzi ambao hawajui kusoma wala kuandika katika mtihani wa darasa la saba watawajibishwa.

  nina maswali yafutayo
  1. anayetakiwa kuwajibishwa ni mwalimu mkuu au viongozi waandamizi wa wizara ya elimu na idara zake.??
  2. mkuchika anajua kuwa kuna shule zina walimu watatu tu??na wote wanafundisha masomo yanayofanana??
  3. anajua kuwa huko mashuleni siku hizi hakuna hata "chaki' za kuandikia ubaoni??je unategemea nini katika mazingira kama haya??hili nimeliona kwa macho yangu kwa sababu wazee wangu wote walimu wa shule ya msingi.
  4. anajua kwamba mitaala inabadilishwa na wizara bila kutoa mafunzo kwa walimu ambao ndio wadau wakubwa katika kufundisha???
  5. anaelewa kuwa walimu ndio tabaka ambalo limesahaulika sana katika utumishi wa umma?tofauti na kipindi cha enzi za mwalimu ambapo mwalimu,bwana shamba na bwana waganga walikuwa wanathaminiwa sana katika jamii??amefanya utafiti kujua nini chanzo cha matatizo hayo???
  6. serikali yenu imewalaghai walimu mara ngapi kuhusu madai yao??unajua kuwa walimu wamekata tamaa sana???je unategemea kupata matokeo mazuri kutoka kwa walimu waliokata tamaa??
  mimi naona uanze kuwajibika wewe kwa sababu umepewa wizara nyeti lakini unakurupuka kama vile umekuja kutumikia watanzania kwa mkataba kama expatriate baada ya hapo utarudi kwenye nchi yako uliyozaliwa.timizeni wajibu wenu ili mpate nguvu ya kuwawajibisha wasio wajibika kwa tulipo fikia sasa mnalea matatizo baadala ya kuondoa.namwomba mungu tanzania ipate/azaliwe pacha wa paul kagame (rwanda) ili tuweze kuwa na dhana ya uwajibikaji.
   
 2. M

  MSHUKU WA MANGI Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu Mkuchika ilibidi apigwe chini na wenzake kama si huruma ya JK.Hana jipya kabisa!
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,084
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  hivi kwa mfano, mitihani ya darasa la sabu nasikia ilikuwa ya kuchagua jibu sahisi, sasa kama mtu kabatatisha mwalimu mkuu anahusikaje?
   
Loading...