Geographia naijua vizuri sana!................

Terrire

Member
Jul 13, 2011
88
9
Mzee mmoja hua anapenda kujisifia sana. Siku hiyo akawa anajisifia ashatembelea zaidi ya nchi 12 Afrika.
Ikawa namna hii;
CONGO nimewahi kutembelea kipindi Pepe Kale anaanza mziki nilikuwa huko.
RWANDA nimeishi kama miaka miwili kipindi kile kuna machafuko ya makabila
SOMALIA tulikuwa tukipeleka vyakula vya msaada mara kwa mara
Mara mtu akamuuliza swali “Kwa maana hiyo Geographia unaijua vizuri sana eeh”, mzee akajibu
GEOGRAPHIA ndo usiseme maana pale nimeishi mda na nina watoto wawili huko……………………….
 
waongo kama hawa wapo sana...!

nakumbuka hata mimi wakati nilivyokua formII kuna jamaa alikua anatudanganya wakati akiwa anatusimulia movie..! sasa tukataka kumshika....! akawa anataka kuelezea mapikipiki ambayo jamaa walikua wanatoka nayo kwenye jengo flani hivi..! sasa tukamwambia kua eeeeh yale mapikipiki yalikua yanaitwa mitochondria eeeh...!? jamaa akakubali fasta akasema eeeh bwana na wewe uliyaona eeh...!? basi tulicheka kinyama..!
 
Hata huku kwetu kuna jamaa alijidai katembelea nchi nyingi sana za ulaya akaanza kututajia "aah pale Uingereza tulikaa wiki moja kisha tukapanda treni ya chini tukaenda United Kingdom tukakaa siku tatu, then tukaenda mpaka Great Britain tukapiga semina ya siku mbili baadae ndio tukamalizia na England tukarudi bongo..'
 
Wabongo ndio zetu hizi tukiwa kijiwe mtu anaazisha stori ya uongo hadi yeye mwenyewe anajishtukia.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom