Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,802
- 11,961
Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), amewatoa hofu Wananchi kuhusu hotel kubadilisha jina. Ameyasema hayo leo wakati akiongea na Wahariri wa Vyombo vya habari jijini Dar Es Salaam.
Watu wamekuwa wanapotosha kwamba hotel ikibadilisha jina basi ni njia ya kukwepa kodi, hilo si kweli na msikubali kudanganywa.
Watu wanabadilisha majina ya hotel mara nyingi ni kubadilisha brand yao. Na hausiani chochote na kodi kwani hakuna kipya kinachoongezeka wala kupungua kwenye uwekezaji huo ambacho kinagusa kodi. Na utaratibu upo wa kisheria ambao wanafuata ili kubadilisha jina.
Wengi wanatumia majina ya Hotel za huko nje mfano Serena, kempinski, hyatt nk. Mwisho wa siku unakuta wanashindwa kuelewana na wenye jina la hotel, matokeo yake wanabadilisha jina lingine eidha laweza kuwa jina la hotel lingine.
Hivyo kawaomba watu wabadili mtizamo wao pindi hotel inapo badilisha jina, hakuna Kodi inaibiwa.