Genge laundwa kumkabili Kikwete: Agenda 21?

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
802
Genge laundwa kumkabili Kikwete


- Lahofia mabadiliko serikalini

- Yeye ajiandaa kuwakabili


Na Saed Kubenea

GENGE la watuhumiwa wa ufisadi nchini linajiandaa kukabiliana na utawala wa Rais Jakaya Kikwete ili kuudhoofisha kabisa, MwanaHALISI limeelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, genge hili sasa linaunda mtandao wa nchi nzima ili "kulegeza nguvu za Kikwete."

Hadi sasa wanaotuhumiwa kuwa kwenye genge, tayari wamekutana mjini Morogoro kwa kikao cha siku moja. Kikao cha pili kimefanyika jijini Dar es Salaam mwezi uliopita.

Vikao vyote viwili vimehudhuriwa na baadhi ya makada na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi wa zamani serikalini na waandishi wa habari walioitwa kama "waalikwa maalum" ili wasaidie katika kujenga kile walichoita "mkakati usioshindwa."

Taarifa za kuwepo genge hilo na majukumu yake zimekuja wakati kuna taarifa nyingine kutoka ndani ya serikali kwamba Rais Kikwete amejiandaa kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa.

Rafiki wa karibu mno wa mmoja wa watuhumiwa wa ufisadi waliomo serikalini alilidokeza MwanaHALISI kwamba watuhumiwa wamejiapiza kumdhoofisha Kikwete kabla hajawaumbua zaidi.

Viongozi wa genge hilo hawajafahamika bali kuna fununu kwamba limebuniwa na litaongozwa na waliokuwa marafiki wa karibu sana na Kikwete wakati wa mchakato wa kutafuta urais ambao wanajihisi wameenguliwa au kudhoofishwa kisiasa.

"Mambo mengi yanayojitokeza, wameyafanya kwa pamoja au anajua kuwa waliyafanya; kwa hiyo wanasikitika kuona anakaa kimya bila ya kuwatetea au kuwakemea wanaowatishia au kuwaumbua mbele ya wananchi," kimeeleza chanzo cha gazeti hili.

Hata hivyo, taarifa za kuwepo genge hilo zinaonekana kuwa siyo habari kwa utawala wa Kikwete. Ofisa mmoja serikalini amekiri, "Hata rais anajua hayo; usidhani amelala tu. Huyu ni mkuu wa nchi bwana," ameeleza.

Akizungumza kwa kujiamini, ofisa huyo wa ngazi ya juu amesema: "Tunafahamu kinachoendelea. Tuko makini. Nakuhakikishia hawatafanikiwa kudhoofisha utawala."

Ofisa huyo akizungumza kwa sharti la kutotajwa, amesema: "Subiri. Utaona mabadiliko makubwa yatakayotokea katika kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa."

Mtoa habari huyo amesema serikali ina taarifa za kutosha juu ya wanaotaka kuleta vurumai serikalini na hatua waliyofikia katika maandalizi yao.

Amesema genge hili lina nia ya kupaka matope baadhi ya viongozi serikalini, kuwadhoofisha na kuhakikisha kwamba hawatakubalika kwa umma kuchukua nafasi za juu kama uwaziri pale itakapolazimu kufanywa mabadiliko.

Taarifa zaidi zinasema waliolengwa mbali na Kikwete ni Spika wa Bunge, Samwel Sitta, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Dk. Harisson Mwakyembe.

Wengine ni Profesa Mark Mwandosya ambaye ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, na Mbunge Simanjiro, Christopher ole Sendeka, Naibu Spika Anne Makinda, Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii na mfanyabiashara mmoja mashuhuri nchini.

Mtoa habari hizi amesisitiza: "Rais ana taarifa zote. Yuko makini. Amejiandaa kukabiliana na lolote na kamwe hatarudi nyuma."

Kuna taarifa kwamba baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi waliokwishaathirika kwa maamuzi ya Bunge, wana mkakati wa kuhakikisha wanarudi kwenye nafasi zao serikalini na kwamba watafanya kila liwezekanalo kufanikisha hilo.

MwanaHALISI liliwasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, kutaka kupata usahihi wa taarifa hizi alisema, "Sijui kama kuna kitu hicho. Nadhani huo ni uzushi wa mjini wa kawaida usioisha."

Taarifa ambazo gazeti hili limepata zinasema Rais Kikwete ana mpango wa kufumua uongozi kuanzia baraza la mawaziri hadi ngazi ya chini anakofanya uteuzi.

Hatua ya rais kutoteua waziri mpya wa Wizara ya Miundombinu tangu 20 Aprili alipojiuzulu Andrew Chenge, kumewaweka mawaziri matumbo moto na kutoa nafasi kwa wachunguzi wa mambo ya kisiasa kuona mabadiliko hayo kuwa suala linalowezekana.

Tangu kutokea mfumko wa madai ya ufisadi kwa baadhi ya viongozi wa serikali ya CCM, mawaziri wanne wameshajiuzulu.

Hawa ni aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri waliokuwa katika Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi. Chenge alijiuzulu wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo, kuna orodha ndefu ya mawaziri na maofisa wa serikali wanaotuhumiwa kula mlungula kutokana na ununuzi wa rada na ambao kwa sasa wanachunguzwa na shirika la uchunguzi wa ufisadi la Uingereza (SFO) na serikali ya Tanzania.

Imefahamika kuwa kutokana na uteuzi wa mawaziri kuwakumba wale ambao baadaye wanapatikana na kashfa, rais ameanzisha utaratibu mpya wa kupata wateule wake.

"Sasa kila mtarajiwa sharti achunguzwe kwanza na chombo maalum kabla ya kukabidhiwa madaraka ili kumwondolea rais aibu ya kujirudia kila mara," ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya serikali.

Tayari rais amefanya mabadiliko mara nne katika Baraza la Mawaziri tangu achukue madaraka ya kuongoza nchi karibu miaka miwili na nusu sasa.

Mara ya kwanza alifanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kubadilisha baadhi ya mawaziri wakiwemo Karamagi kutoka Biashara na Viwanda kwenda Nishati na Madini na Dk. Msabaha kwenda Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wakati huo pia Chenge aliyekuwa Afrika Mashariki alipelekwa Miundombinu kuchukua nafasi ya Basil Mramba aliyekwenda Biashara na Viwanda.

Mara ya pili mabadiliko yalitokana na kifo cha Juma Akukweti aliyekuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu aliyeshughulikia masuala ya Bunge.

Mara ya tatu mabadiliko madogo yalifanywa kuziba nafasi ya Asha-Rose Migiro aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye aliteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) kuwa msaidizi wake.

Rais alifanya mabadiliko ya nne alipovunja baraza zima la mawaziri na kuliunda upya Februari mwaka huu. Alimrejesha Chenge kwenye wizara yake ya awali akipuuza kelele za umma na vyombo vya habari za kudai "hakustahili."

Source: MwanaHALISI
 
Kama yaliyowekwa hapa yatafanyika kweli basi nitamuona Jk kama mtu mwenye akili kweli. na kweli atakuwa ametekeleza majukumu yake ktk kumukomboa mtanzania.

Lakini yangu macho, maana mimi kutokuwa na imani na Jk ilianza mara tu baada ya mabadiliko ya kwanza ya baraza la mawaziri baada ya kufanya yale yalev tuliyoyazoea.

Tunasubiri mabadiliko hayo.

Tanzania ili tuendelee inatakiwa tuachane na siasa za ubinafsi. CCM/TANU kuna kipengele kimoja kinasema nitasema kweli daima FITINA kwangu mwiko. Nafikiri kuna wengi wameisha vunja kipengere hiki.

Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa sana ya uongozi kuanzia ngazi za kata mpaka taifa. Hata CCM hili kiwe chama kinahitaji mabadiliko makubwa sana kuanzia ngazi za chini, vinginevyo siasa zinazofanyika sasa sio siasa. nafikiri watanzania wanahitajio chama chenye kuelekeza watu kwenye maendeleo. Siyo Chama chenye kuelekeza watu kwenye Mabaya. Ni kazi ya chama tawala kuhakikisha kinaweka misingi ya kuachana na mabaya na kujenga tanzania yenye mwelekeo wa maendeleo.


Kwa sasa hivi ni itakuwa vigumu kwa watanzania wenye Utaalamu mbali mbali kukaa kwenye environment ya watu kila kukicha ni WIZI ufisadi ndio topic na mambo yasiyokuwa ya maendeleo.
 
Lakini hizi habari zina ukweli ama ndio hadithi zinazotafuta mbinu ya kutuondoa nguvu sisi tunaopiga vita uwajibikaji wa kiongozi wetu.

Isije kuwa kila tunayoandika hapa yakaonekana kuwa ni kundi la hao Mafisadi kwani kila siku Kikwete amekuwa kichwa cha hoja zetu..hawa wansiasa wana mbinu nyingi sana.

Kibaya zaidi ni pale Kikwete mwenyewe anapokuwa kimya akijaribu kuwalinda mafisadi bila kufahafahamu kwamba Wadanganyika siku zote ni wanafiki wakubwa...watacheka na wewe usoni pale wanapohitaji kitu lakini wengi wao yameshika kutu ktk roho zao.

Nina hakina wapo wengi wanasubiri kuanguka kwa Kikwete na bahati mbaya hata sisi tumejiunga na kundi hilo kutokana na hizo pamba alizojiwekea masikioni..Lakini siku atakapoweza kujitenga na kundi hilo hapo tena mkuu swala la kumlinda rais wetu ni swala la kitaifa na hao kundi la agenda 21 itabidi watafute nchi ya kukimbilia...na kama Marekani waemavyo tutawafuata huko huko..
 
Kupambana na ufisadi ni vita. Na katika vita adui yako akigundua kwamba wewe ni dhaifu basi anapata nguvu ya kupambana nawe. JK kishaonyesha udhaifu mkubwa wa kupambana na ufisadi, sasa mafisadi wamegundua hilo kwamba jamaa anayumba na hana credibility miongoni mwa Watanzania wengi hivyo wameamua kumgeuzia kibao ili wazidi kuharibu credibility yake ambayo imeshatetereka kwa kiasi kikubwa
 
Acha tuone maana inasemekana kuwa masuke na mtama hufanana sana awali ,ila mtama ukiwashakuwa(komaa) ni rahisi kutenganisha mtama na masuke.So time will tell.Maana hapa naona kama brainwash education.
 
Rais hajaamua kuenea ktk kiti chake alichopewa na wananchi ndo maana tunasikia haya magenge.Yeye asikae nyuma ya kamera maana hataonekana.Ajaribu kukaa mbele ya Kamera atamke kitu kwa mjibu wa taratibu,kanuni na sheria zinazoendesha nchi hii kama hakitakuwa?
Lakini kama atendelea sana kukaa nyuma ya kamera amekwisha kabisa
 
...ukipigana na mtu na kila akikupiga sehemu flani mahususi una flinch,atapiga hapohapo wakati wote mpaka akushinde.Lakini kama ni mpiganaji jasiri,utajikaza na kutoonyesha maumivu hata kama yapo.Huo ndio mtihani wa JK
 
Kampeni za chinichini zaimarika CCM

2008-05-08 10:34:23
Na Mashaka Mgeta


Kampeni za chini kwa chini, zimeibuka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zikiratibiwa na wanachama wake wanaotaka kugombea ubunge mwaka 2010.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Bw. John Chiligati, ameowanya wanachama wanaofanya kampeni hizo na kuahidi kuwashughulikia.

Hivi karibuni, gazeti moja la kila wiki, lilidai katika makala yake ya uchunguzi kwamba, ingawa hiki ni kipindi cha kwanza cha Rais Jakaya Kikwete, yupo mwanachama mmoja wa chama hicho aliyeutaka urais mwaka 2005, naye ameanza kampenzi za chinichini kutaka kuingia ikulu.

Akizungumzia kuhusu kampeni za chini chini zilizoanza, Bw. Chiligati, alisema wanachama watakaobainika kuhusika na kampeni hizo, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni na maadili ya chama hicho.

Habari kutoka ndani ya CCM, zilidai kuwapo makundi ya wanachama, walioanza kujiimarisha majimboni, ili kuhakikisha wanateuliwa kugombea ubunge mwaka 2010, kupitia tiketi ya chama hicho kinachoaminika kwamba bado ni ngazi nzuri ya kutafutia ubunge.

Orodha ya wanachama wa CCM wanaodaiwa kuhusika katika mpango huo, inawahusu waliokuwa wabunge kwa kipindi kilichoishia mwaka 2005, Mawaziri na Naibu Mawaziri.

``Hali katika CCM hivi sasa si shwari, watu wenye uchu wa kuwa wabunge wapo majimboni wakitoa misaada na kujinadi kwa wajumbe wa vikao vya uteuzi, ili wateuliwe mwaka 2010,`` aliiambia Nipashe mbunge mmoja.

Mbunge huyo aliyewahi kuwa Waziri, alisema miongoni mwa kauli zinazotolewa na watu wanaojipitisha majimboni hivi sasa, ni `kuwaponda`? wabunge waliopo, kwamba hawajafanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005.

Kutoka mkoani Mara, inadaiwa kuwa Naibu Waziri mmoja, anashindana kwa karibu na mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato (TRA), anayetaka kuwania ubunge katika moja ya majimbo ya mkoani humo.

Kwa mujibu wa habari hizo, mfanyakazi wa TRA anatumia kigezo cha jinsia kama ukosefu wa sifa unaomfanya Naibu Waziri (majina yao tunayo) asiungwe mkono.

Pia Naibu Waziri anatumia kigezo cha elimu na uzoefu wa uongozi, kama hoja inayompa uwezo wa kuliwakilisha jimbo hilo bungeni.

``Hawa watu wanashindana sana, lakini mpaka sasa hawajaweka azma yao kugombea ubunge kwa kuwa muda wa kuanza rasmi kampeni haujafika,`` kilisema chanzo chetu cha habari.

Aidha, mkoani Mbeya inadaiwa kuwa mwana-CCM mmoja (jina tunalo) aliyewahi kuwa mbunge, anapita kwenye jimbo moja mkoani humo, akijitangaza kutaka kurejea katika kile anachokiita kuwa `jimbo lake⿮

Taarifa hizo zinadai kuwa mwana-CCM huyo anampinga mbunge aliyepo sasa, na ambaye alimuwezesha kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000.

Aidha, inadaiwa kuwapo ushindani ulioibua hali ya makundi ya wanachama wanaowaunga mkono wenzao wanaotaka kugombea ubunge kwenye majimbo mbalimbali nchini.

Kutokana na hali hiyo, taarifa zinadai kuwa miongoni mwa mkakati unaotumiwa na washindani hao, ni kujijengea safu ya uongozi utakaoshiriki katika uchaguzi wa serikali za vitongoji, vijiji na mitaa utakaofanyika mwakani.

Miongoni mwa wanaotaka kuwania ubunge, walishiriki kufanikisha makundi ya watu wanaowaunga mkono, kushinda katika uchaguzi wa CCM uliopita.

``Kwa sasa wenzetu wanajipanga kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mtaa, ili kujiwekea mazingira bora zaidi ya kushinda ikiwa watateuliwa na CCM,`` alisema mmoja wa chanzo chetu cha habari.

Uchunguzi wa Nipashe, ulibaini kuwa watu wanaoendesha kampeni za chini chini ndani ya CCM, wanashiriki katika kutoa misaada kwa chama hicho na jumuiya zake.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Bw. Chiligati, alisema kufanya kampeni kabla ya mwaka 2010, ni ukiukwaji wa kanuni na maadili ya CCM.

``Hawa watu wanaofanya kampeni, wanatumia muda gani kukitumikia chama na wananchi??Alihoji na kucheka.

Bw. Chiligati, alisema wahusika wa kampeni hizo wakijulikana, watakuwa wamejiondolea sifa za kuwania nafasi ya kuteuliwa na CCM kuwania ubunge.

``Hata kama watawatumia watu kuelezea azma yao, chama kipo macho, tutawapata tu,`` alidai.

Bw. Chiligati, alielezea kusikitishwa na hatua hiyo, kwa vile majimbo yaliyopo yana wabunge hadi ifikapo Uchaguzi Mkuu ujao.

Aidha, Bw. Chiligati, ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alitetea hatua ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kutumia magari ya serikali kwa shughuli zao majimboni.

Madai ya kuanza kampeni za chini kwa chini ndani ya CCM, yameibuka ikiwa ni takribani miaka miwili, kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu ujao.

SOURCE: Nipashe
 
Wengine ni Profesa Mark Mwandosya ambaye ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, na Mbunge Simanjiro, Christopher ole Sendeka, Naibu Spika Anne Makinda, Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii na mfanyabiashara mmoja mashuhuri nchini.

Huyu mfanyabiashara lazima ni Mengi tu,naona kawapania sana hawa
 
Hawa jamaa mm naamini wanaweza wakashinda kabisa kwani wanafedha wanaunda mtandao we fikiria kama MAFISADI LOWASA na CHENGE wapokelewa kwa mbwembwe kubwa sana kwao huko na kuonekana watakatifu baasi wameunda mtandao mkubwa sana ambao JK hawezi kuusambalatisha kwani kesha onyesha udhaifu mkubwa sana.
 
Genge laundwa kumkabili Kikwete


Lahofia mabadiliko serikalini

Yeye ajiandaa kuwakabili


Na Saed Kubenea

Kuna taarifa kwamba baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi waliokwishaathirika kwa maamuzi ya Bunge, wana mkakati wa kuhakikisha wanarudi kwenye nafasi zao serikalini na kwamba watafanya kila liwezekanalo kufanikisha hilo.
Source: MwanaHALISI

Walioathirika na maamuzi ya Bunge ni Lowasa, karamagi na Msabaha. Kwa hivi bwana Kubenea unataka kutuambia unazo taarifa kwamba hawa wabunge wanapanga mikakati ya kurudi kwenye nafasi zao???How is this possible on earth???
 
Mimi naendelea kuwasikitikia sana wananchi wenzangu wanaoendelea kufikiri na kuamini kwamba JK sio sehemu ya tatizo. The only hope is that people will realise the true colours of JK before it is too late!
 
Yaai amekuja na kazi ya kubadilisha mawaziri tu ,miaka inakatika muda wake asifikiri unazidi kuwpo hapo kwenye kiti cha Uraisi bali unakwenda kwa kasi na nguvu mpya ,maana kila siku zinapopita WaTanzania wanajuta kuchagua handsomeboy ,yaani ni mtu wa milunzi tu utafikiri mpiga filimbi wa melini.Huyu jamaa yaani Muungwana ukimuona katika ziara zake anapotembelea tembelea kwa raha zake basi utajua kama ni mtu asie na wasi wasi kabisa ,tembea zake mkono mmoja mfukoni na akipiga mirunzi mdomoni akiimba nyimbo za kwao.
Tulipata Raisi Mlokole Nyerere akatupeleka kwenye vijiji vya ujamaa tukaliwa na Simba ,akaingia Mwinyi mzee wa taarabu yeye ikawa rukhsa kila kitu we fanya tu mradi huvunji sheria maana unaweza sheria usizifuate lakini kwa wakati huo huo huzivunji ,mara kaingia Mzee wa Togwa Mkapa biashara mpaka Ikulu na nyie mlioko nje huko kazi kwenu kama mtateka benki au mtapeana mikopo mtajiju..sasa kaingia huyu Ustaazi eti anapokuwepo chupa ya ulevi isionekane machoni pake wala hotelini huko anakofikia basi mambu ya ulevi yawekwe kusini kama yeye yupo Kaskazini na akienda Kaskazini yapelekwe mashariki inakuwa vioja si vidogo anasafiri akirudi anabadilisha mawaziri kazi ni hiyo na hafukuzi mtu ulichopata ndio chako anabahatisha mwengine , inaonekana atamaliza muda wake jamaa kibao wataukwaa Uwaziri yaani Uraisi wake nafasi za uwaziri nje nje !!!
 
yaani ukiangalia jinsi hii nchi inavyokwenda ni kama vile unaangalia tamthilia.
coz hao wooote waliotimuliwa kwa ufisadi ndo marafiki wakubwa wa kikwete, so ni wazi kuwa vile alivyofanya nikuwafumba midomo wabongo kisha ye na washikaji zake wanaendelea kula raha...mi nakuunga mkono kitila mkumbo kuwa fisadi namba moja ni JK.
 
Kufanya hivyo ni UHAINI wanatakiwa wakamatwe na kutiwa kizuizini. Tusipofanya hivyo Tanzania inakwenda kubaya. Usalama wa taifa wako wapi siku hizi jamani?????
 
Kale ka mzimu ka ccm kulindana kako mbioni kuisha na hapo mchezo utakapokuwa mtamu. Kitendo cha Rais kuwa na uhakika wa kukaa madarakani mika 10 bila wasiwasi ufe.
 
Hilo ni Genge La wanyang'anyi ambalo ni lazima Muungwana ataliweka kizuizini,na nadhani kuna haja ya kufufua thread yangu kuhusu uchaguzi wa UVCCM,huko ndipo anguko lingine la tatu la Lowassa litakapoanzia.

anataka kuweka mtu wake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom