Genge la walaghai, matapeli na wanyang'anyi wanatesa wananchi hapa Sahara jijini Mwanza

BrAsMaRiLiSaShElMa

Senior Member
Sep 23, 2016
131
250
Kwako OCD NYAMAGANA,
C.C. RPC MWANZA;

Bila kupoteza muda napenda nieleze juu ya uovu unaofanyika hapa eneo la SAHARA, mkabala na Posta Pamba Road.

Katika eneo hili kuna pilika nyingi za kibiashara, ambapo watu wengi kutoka sehemu mbalimbali hufika hapa ili kujipatia mahitaji yao mbalimbali.

Penye wengi pana mengi; wapo watu wanaofanya biashara zao halali na watoa huduma mbalimbali; lakini pia wapo watu waovu ambao wanawaibia watu wengine fedha na mali zao kwa ulaghai na utapeli na hata kwa kuwanyang'anya kibabe.

Miongoni mwa hawa watu waovu, lipo genge la watu ambalo linaweka banda kama ofisi kwa ajili ya kufanya uhalifu.

Watu hawa wamejenga hema au banda ambamo wameweka vitu vya kudanganyia watu kama TV, Redio, Generator, Sub Woofer n.k; huku wakiwashawishi wapitanjia wacheze kamari kwa kuweka fedha, ili eti waweze kujipatia vitu hivyo!

Watu hao wako kundi kubwa; wapo wakinamama, wapo vijana na watu wa makamo. Hawa wote hufanya kazi kwa pamoja huku wengine wakijifanya nao kuwa wateja, na hata kujifanya wameshinda zawadi au fedha kutoka kwa waendesha mchezo huo, kumbe ni wenzao.

Hufanya haya yote ili kuwashawishi wapitanjia waone kwamba kumbe kweli inawezekana mtu kunufaika na kamari ile, hivyo mtu hujitosa kuweka fedha zake ili ajipatie moja ya vifaa hivyo au azalishe fedha yake, lakini mwisho wake huwa ni kilio!!

Watu hawa ni hatari; wakikuona unamtahadharisha mtu asikubali kucheza kamari hiyo, basi watakusonga, kukupiga na hata kukupora mali yako na hutapata msaada maana watu wanawaogopa.

Haya yanafanyika wakati mkabala na banda lao ng'ambo ya barabara kuna askari polisi wenye silaha wanachunga benki ya posta; na mbele kidogo kabla ya kufika keep left ya Nyerere Road kuna kituo cha polisi Pamba Road.

Afande OCD Nyamagana, ina maana kweli wewe hujawahi kupata taarifa juu ya hawa wachezesha kamari ambao wanachezesha hadharani barabarani kutwa nzima siku 7 kwa wiki? Au unataka tuamini maneno yao kwamba huwa wanapeleka mgao sehemu sehemu?

Sipendi kuamini maneno yao hayo, lakini sielewi kwa nini watu hawa waendelee kuibia watu hadharani tena bila hofu wakati wewe upo Mjini na maofisa wako wengi wenye mbinu, weledi, vifaa na uwezo wa kisheria; kwa nini jambo kama hilo halikomeshwi?

Katika makabila kadhaa ya Tanzania na baadhi ya nchi jirani MULIRO maana yake ni MOTO; tunataka hicho kibanda kiwake moto kiteketee kabisa, kisiwepo tena hapo SAHARA; kinafedhehesha dola.
 

Trimmer

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,645
2,000
Ajabu ni kwamba hutangaza na kuonyesha kibali kutoka mamlaka husika (hapa siwezi ku confirm ni mamlaka gani)
Ni kama vile huu mchezo una "baraka" zote toka "Himayani"
 

MoneyHeist4

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
1,510
2,000
Bila kusahau maeneo ya stendi mpya ya nygezi (Nyabulogoya) ilikohamia ukiwa unaingia tu unawakuta hapo barabarani na hema lao.

Huwa najiuliza sana inamaana serikali huwa haioni huu wizi.

Ukijifanya kumwambia mtu asicheze huo mchezo wanakukata jicho la hatari unaamua tu utoke. View attachment 1676144
View attachment 1676145
 

MoneyHeist4

JF-Expert Member
Jul 10, 2017
1,510
2,000
IMG_2717.jpg

IMG_2720.jpg
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
3,774
2,000
Maadam wanalipa kakodi kidogo serikali haijali kuhusu wananchi wanaotapeliwa.
Juzi kuna majamaa niliwakuta Kariakoo Gerezani, eti mmoja ananisemesha kuwa ni mchezo mzuri ukiwa na bahati. Akatoa buku akijifanya hawako pamoja, ile anapewa tiketi tu nikamwonyesha mshiko ila nikamwambia ni heri nikanunue mbwa kuliko kamari ya mbongo
 

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,736
2,000
Hata Arusha karibu na Stand ya mkoa opposite ya Sheikh Amir Abeid Stadium wamepiga kambi
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
9,282
2,000
Ao jamaa wapo kitambo sana,kuna kipindi walikua maeneo ya mwaloni karibu na geti la Nyeunge.
Ao wapo kitambo sana,miaka ya nyuma nikaja tena kuwakuta pale Ilala Boma.
Awajamaa ni matapeli,kikubwa ni watu kuacha tamaa,tamaa zinawaponza watu kutaka mali ama vitu kwa rahisi.
 

Ngwakwiii

Member
Dec 6, 2019
50
125
Kwa huo mchezo wa kamari ni katibu mikoa yote Tanzania upo ila ni ulaghai mtupu huwa nashangaa vyombo vya ulinzi jwa nn hawavifuatiliii
Sio watu wote waelewa wa kujua kwamba wale ni wezi maana huwa wanakuwa wengi na wanakuwa maeneo ya wazi kabisa naamini ni wakati wa mh simbachawene ataliona hili
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom