Generali Ojukwu Ni Kwanini?

Na mwandishi kama anaogopa kusoma madocuments makubwa ya lugha za kisomi za maprofessa na mshauri asome novel iliyoandikwa kwa lugha nyepesi na mwandishi wa kinaigeria anayoitwa Elechi Amadi jina la kitabu ni sunset in Biafra.wameeleze mkasa wa biafra kwa lugha ya kawaida.
 
William,
Nimesema soma hicho kitabu. Pia kuna kitabu kingine ameandika Godfrey Mwakikagile, "Nyerere and Africa: End of an Era". Kuna hoja za kujadilia humo kuhusu vita ya Nigeria. Huwezi kufikia hitimisho kwamba sera zetu wakati wa Mwalimu zilikuwa wrong bila kuwa na full knowledge of what you are talking about. That is what makes us great thinkers here. And yet still, hapa hapa JF kwenye archives zake kuna mjadala mrefu kuhusu vita vya Nigeria na kwa nini Tanzania iliunga mkono Biafra. Sasa unaanzisha thread ambayo umeshafikia hitimisho kwamba Tanzania tulifanya makosa kuiunga mkono Biafra bila kuwa na data sahihi na relevant. No research no speak.
Mkuu thanks kwanza kwa ilimu uliotoa.....pili kuna thread it was hot namshauri william asome kwanza.....
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/90742-why-did-nyerere-support-biafra.html

archieve za jf ni hazina jamani kuna thread nyingine mnazotaka kuanzisha au maswali mengine yana majibu humu humu....
 
Tanzania ilivotuma jeshi kwenda kuikomboa Seychelles, na mpaka Seychelles iko jinsi ilivyo kwa sababu yale mapinduzi yalizimwa na jeshi letu, pia ni wrong policy?

Hapa ndio CCM wanapopotezana na wananchi. Wanatafuta point kwa lolote baya linalotokea sasa hivi kuwa ni kosa la history, kama vile sasa hivi nchi inatawaliwa na watoto. Huyo Mwalimu unayetaka kumlaumu kwa kila kitu, majority ya wananchi wa kawaida hawatakuelewa, hata wale waliozaliwa baada ya yeye kutoka madarakani. Hio inaleta picha kwa wananchi kuwa hata solutions za matatizo yanatokea sasa hivi hamna, mwenye nazo hizo solutions ni Mwalimu, ambaye hayupo tena.

Nenda leo Zanzibar kawaambie kuwa haya matatizo ya Uamsho yanatokana na Tanzania kui support Biafra 1967! Wrong policies hata kama zilikuwepo, ndio zinatakiwa kui shape nchi na kuwa na mwelekeo mzuri kwa kurekebishwa na watawala wanaofuata, sio kukaa na kusema kila saa tuna matatizo sasa hivi kwa sababu ya zamani. Mfufueni basi Mwalimu aje kuwarekebishia, then mumwache apumzke kwa amani.

Only in Tanzania.
 
Siasa wakati mwengine huwa kama mchezo wa kamali. Unaweza kushinda ukaonekana shujaa au ukashindwa na kuonekana dhaifu. Katika swala la Biafra, Tanzania ilichokifanya ni maamuzi ambayo iliamini ni sahihi. Kwa vile maamuzi hayo hayakuungwa mkono na nchi zenye influence na siasa za Dunia, hayakufanikiwa. Hata hivyo, ingetokea kuwa Biafra ikafanikiwa kuwa Taifa huru, Tanzania ingeonekana shujaa.

Kitu ambacho mimi siungi mkono kuhusu siasa za Tanzania za miaka ya 60 ni swala la kujihusisha mno na Uhuru na ukombozi wa nchi nyingine. That was a major mistake of the era.Nchi iliyopata Uhuru inapaswa kuendelea na harakati za Uhuru wa kiuchumi na maendeleo. Katika historia ya Tanzania hakuna maandishi ya jinsi Tanzania ilivyosaidiwa na mataifa mengine kujikomboa, sasa kama hivyo ndivyo, kwanini tuliamini kuwa ili wengine wawe huru ni lazima sisi tutumie resources zetu kuwakomboa??? Tumetumia resources kibao kuwakomboa Afrika Kusini, mwisho wa siku wanatucheka tu!!! Tumepeleka majeshi Biafra kwa gharama kubwa, mwisho wa siku tumeloose. Iwapo jitihada hizo tungeziweka kwenye kuhakikisha Tanzania inakuwa namba moja katika uzalishaji wa pamba, kahawa na karafuu tungekuwa mbali sana hivi sasa. Katika historia ya Bara lililoendelea kuliko yote, Ulaya, hakuna tabia hiyo ya nchi moja kwenda kuikomboa nyingine unless kama ilitaka kuitawala. Sisi hatukutaka kutawala nchi yoyote lakini tumetumia resources zetu kuwasaidia watu ambao wangeweza kuwa Huru wangekuwa tayari. That, I believe, was a grand mistake. sasa, baada ya kufanya makosa hayo ya miaka ya 60, tunaenda wapi? Kwa sababu makosa yameshafanyika, tuangalie tunakoelekea.
 
William kaka, najaribu kuelewa hasa msimamo wako katika hili ni upi.. Hasa katika mapungufu ya policies na misimamo mingi ya Taifa letu kwa wakati huo.. Nani hasa alikosea.. Ni Nyerere mwenyewe kama kiongozi au mfumo wa chama na serikali yake kwa wakati huo?

Pamoja na yote, nashukuru kwa kuleta hii thread, mie sikuwepo wakati huo na ningependa sana kujua historia na wapi tulikosea. Kwaiyo mie ni msomaji katika hii thread nikiwa na nia ya kujifunza zaidi.
 
Kwa usahihi yule alikuwa ni Kanali Ojukwu ambaye alikuwa amesoma na kumzidi hata mtawala wake Jenerali Yakubu Gowon. Wakati wa Ukoloni wa mwingereza , mkoloni alitumia utawala usio wa moja kwa moja kuwatawala waafrika kwa kuwatumia machifu na viongozi wa kikabila ni Sir Donald Cameron aliyeanzisha mfumo huu.

Kama tujuavyo nchi ya Nigeria imegawanywa na mto Niger ambao uko katika "Y-SHAPE" Kaskazini mwa nchi hiyo kuna kabila la Hausa, Kusini magharibi mwa nchi kuna kabila la wa -Yoruba na Kusini mashariki kuna kabila la wa Igbo. Katika kipindi cha kabla ya mkoloni Afrika Magharibi walikuwa na vi-nchi vilivyokuwa vikijulikana kama "South Sudanic states" mfano wake ni " Dahomey" na hii kitu inayojulikana kama "SOKOTO CALIPHATE" ya akina UTHMAN DAN FODIO. Maeneo haya dini ya Uislam ilikuwa imeshamiri na kuota mizizi kwa kiasi kikubwa na wakati wakoloni wanafanya mkutano wao wa Berlin wa mwaka 1884 kuigawa Afrika kwa kiasi kikubwa eneo la kaskazini mwa Nigeria lilikuwa likikaliwa na Waislam wengi ambao hawakupenda kusoma shule za kikoloni zilizoeneza ukristo. Ni katika makabila ya Kusini mwa Nigeria ambako Ukristo ulishamiri kwa wingi na kupelekea watu wake kupata elimu na kuajiriwa kama makarani, waalimu, maafisa wakati wa ukoloni.

Wakati Nigeria ikipata Uhuru, mkoloni aliiacha misingi ile ile ambapo kwa asilimia kubwa watu wa kusini ndio waliopata nafasi za ajira pamoja na maisha mazuri upande wa kaskazini na kuwafanywa wao kwa mabwana na wale Wa-Hausa kuwa watwana ambao wakifanya kazi za kutumwa na zile ambazo hazikuwa na heshima. Ikumbukwe eneo hilo ni la wakazi waislamu. Hali hii iliamsha chuki na hisia dhidi ya wale watu wa kusini ambapo wengi walikuwa wakipigwa na kuchomewa nyumba zao na wengine kuuawa. Wakati huo Kanali Ojukwu alikuwa na madaraka makubwa katika nchi akisaidiana na Jenerali Gowon. Ojukwu alikuwa ni mtu wa Kusini. Hali hii ikampa hisia Ojukwu kutokana na serikali yake kutolisemea jambo hilo na kuamua kuwahamisha watu wote walio kuwa kaskazini kwenda kusini na kuanzisha Jamhuri ya watu wa "BIAFRA".

O.A.U kama tujuavyo lilikuwa ni umoja wa nchi za kiafrika unaongozwa kinafiki na ulishindwa kulisemea jambo hilo kwa kigezo cha kutokuingilia siasa za ndani ya nchi "sovereignity" na kupelekea watu wengi kuuawa na vita hivi vya Biafra. Ni nchi za Tanzania, Zambia na Ivory Coast zilizoweza kujitokeza wazi na kuitambua jamhuri ya watu wa Biafra. Ojukwu alitumia zaidi vyombo vya habari vya nje na kwa kiasi kikubwa alitumia zaidi Propaganda wakati wa-Nigeria wenyewe walitumia njia ambayo kwa kizungu wanasema ni "DRY THE POND TO GET THE FISH" Kwa kuharibu miundo mbinu kama barabara, mawasiliano na vitu vingine ilipelekewa watu wengi kufa kwa njaa kwa kukosa vyakula na mahitaji. Matokeo yake Ojukwu alikimbia nchi ya jirani na huo ndio ukawa mwisho wa vita vya Biafra. Kiukweli ilikuwa inasikitisha sana jinsi watoto walivyokuwa wakifa kwa njaa tena pasipo hatia.

Kwa upande wa Zanzibar,ni lazima tukubali kwamba Zanzibar ni nchi ambayo imepata uhuru wake kwa kumwaga damu. Ninasema wazi kwamba walimwaga damu kwa sababu watu wengi waliuawa siku ile ya tarehe 12/1/1964. Na ushahidi wa makaburi ya hailaiki upo. Hii damu bado inawasumbua na kuwatesa na nadhani inawawasha. Ukijaribu kuangalia wanaoanzisha choko choko hizi si hao kikundi cha UAMSHO. Bali hao UAMSHO ni "PROXY" ya wanasiasa ambao wanamahusiano ha HIZBU. Kwa sababu zao na wanazozijua wao wanadai utawala wa Ki-sultan ulikuwa bora zaidi ya muungano na ni heri Zanzibar ijitenge. Jambo wasilolijua ni kwamba ile damu ya mwaka 64 bado inawawasha na kuwasumbua. Watauana halafu baadaye wataanza kusema tukae meza ya mazungumzo tuongee. Kwa hiyo hapa hakuna cha UAMSHO wala nini hawa wafadhili wao na wanaowalinda ni wanasiasa na we need tu fish 'em now before its too late.
 
Mleta mada umegusa pazuri sana.

Sakata la Zanzibar, iliyoungana tu na Tanganyika linakuwa mwao watu kutaka kujitenga na muungano. Biafra iliyokuwa part and parcel ya Nigeria, si kwa kuungana, walipotaka kujitoa (secession) Nyerere aliwaunga mkono kwa hali na mali. Nakumbuka makopo ya kuchangisha pesa za Biafra tukilazimishwa mashuleni kuyabeba na kwenda kufanya umatonya, nasema kulazimishwa kwa kuwa hakuna aliyeweza kukataa. Tukipita kuomba omba mitaani kuwaombea Biafra kwa kushinikizwa na Nyerere.

Ilikuwa ni udini mtupu wa Nyerere na hakuna zaidi.

Nyerere alikuwa ni kanisa kwanza, Tanzania baadae. Mnafikiri kwanini anapigiwa debe na wakristo wenzie ili apewe utakatifu?

Lakini Mwenyeezi Mungu ni mkubwa, hakuna alichofanya chochote kikawa na mafanikio si siku hizo si baadae, kwa kuwa alichokisema ni kingine na aliyonayo moyoni ni mengine. Mungu hatazami matamshi yetu, hutazama nia zetu.
 
- Kila ninapoangalia tulikotokea hili Taifa, ninapatwa wasi wasi sana kwamba hatukufika hapa tulipo kwa makosa, tumefanya makosa mengi sana nyuma in terms of policies mpaka leo hii kurekebisha inakuwa ni almost impossible, ingawa watawala wa sasa wanajitahidi sana.

- Eti ni kwa nini Tanzania tuliunga mkono Waasi wa Nigeria waliokuwa wanaongozwa na General Ojukwu, kwenye kiu yao ya kujitenga na Nigeria Federation? Ninakumbuka tukiwa wadogo Shuleni, tulivyokuwa tunaimbishwa nyimbo za kumsifu Ojukwu, why? I mean ni policies ngapi huko nyuma we were wrong maana inaonekana ni nyingi sana that ni vigumu sana sasa kurekebisha njia!

- JE have we ever apologize to the Nigerians kwa makosa yetu ya kuuunga mkono uasi wa Ojukwu, dhidi ya serikali halali ya nchi hiyo?

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!


William J. Malecela.

Kwa nini tuapologize kwa Nigerians wakati unasema hujui kwa nini tuliwaunga mkono waasi in the first place? Nadhani muhimu kwanza kupata majibu ya swali hili ndipo tutajua kama kuna haja ya ku-apologize au la.
 
Tanzania ilivotuma jeshi kwenda kuikomboa Seychelles, na mpaka Seychelles iko jinsi ilivyo kwa sababu yale mapinduzi yalizimwa na jeshi letu, pia ni wrong policy?

Hapa ndio CCM wanapopotezana na wananchi. Wanatafuta point kwa lolote baya linalotokea sasa hivi kuwa ni kosa la history, kama vile sasa hivi nchi inatawaliwa na watoto. Huyo Mwalimu unayetaka kumlaumu kwa kila kitu, majority ya wananchi wa kawaida hawatakuelewa, hata wale waliozaliwa baada ya yeye kutoka madarakani. Hio inaleta picha kwa wananchi kuwa hata solutions za matatizo yanatokea sasa hivi hamna, mwenye nazo hizo solutions ni Mwalimu, ambaye hayupo tena.

Nenda leo Zanzibar kawaambie kuwa haya matatizo ya Uamsho yanatokana na Tanzania kui support Biafra 1967! Wrong policies hata kama zilikuwepo, ndio zinatakiwa kui shape nchi na kuwa na mwelekeo mzuri kwa kurekebishwa na watawala wanaofuata, sio kukaa na kusema kila saa tuna matatizo sasa hivi kwa sababu ya zamani. Mfufueni basi Mwalimu aje kuwarekebishia, then mumwache apumzke kwa amani.

Only in Tanzania.

Kama watu wanafuatilia vizuri mambo, CCM wamemgeuza Mwl Nyerere kuwa kinga. Kwa mfano CCM wakiambiwa hawana tena uwezo kuongoza nchi wanatakiwa waondoke wao wanajibu - Mwl Nyerere alisema bila CCM imara nchi itayumba. Lakini ukiwauliza kwa nini hii nchi inayumba wanasema Mwl alikuwa na sera mbovu sana!

Ndio maana nasuburi kwa hamu kubwa maelezo toka kwa William kwa nini policies za miaka ya 1960s zinatutesa sasa 2012? Na kwa nini CCM hawajaziondoa hizo policies wanazoona ni tatizo? Kama waliweza kufuta Azimio la Arusha (tena Mwl akiwa bado hai) wanashindwa nini kufuta hizo policies zingine wanazosema ni kero?
 
Wiliam atuambie kwa nini asijiulize wakati huu wa utawala wa kKiwete tumepeleka jeshi kupigana Comoro kumndoa Kanali Bakari, kiongozi wa visiwa vya Anzuani tena bila support ya Bunge la Wananchi. Juzi juzi former director wa TISS mzee Kitine kajuza kuwa Comoro walitoa fedha Serikalini kwa ajili ya kikombozi waziri katia ndani na wewe ukapiga chapuo kuwa Kitine anawivu wa kike dhidi ya waziri unayedai ni swahiba wako.Kama unaakili timamu Tafakari ukipata mwanga tupatie mtazamo wako na siyo hisia hisia za ovyo.
 
W.J.Malecela pole kwa weledi duni kiasi cha kushusha mapigo ya moyo wangu.Katika thread zako ikiwemo hii yafuatayo nina baini kama hivi.Elimu yako hasa ya sera na uchambuzi ni ndogo sana,Mambo mengine ni muhimu kupata feedback kwa mzee cygwesima na kupata conclusion na kama unataka support toka kwenye jopo la great thinkers unakuja na mtazamo dhahiri badala ya kuyumba yumba.Pia ni kwamba pengine ili jina la Malecela unalitumia vibaya pengine ni mtoto wa shamba boy kiasi kwamba una direct contact za kuongea na kupata ufafanuzi kwa mzee huyo ambaye alibobea katika tasnia ya international relation wakati wa mwalimu.Na pia nashangaa kuabudu utawala wa sasa kwamba unafanya vizuri kuliko enzi ya mwalimu kwa lipi ?au umetumwa na mzee cygwesima kumchokonoa mwalimu kwa sababu hajawahi kujadiliwa kama presidintial candidate baada ya mwalimu ampige ban?.Na mwalimu wakati wa uhai wake alieleza wazi kuwa wakati wa uongozi wake kulikuwa na matatizo mengi na sehemu nyingine walifanya vizuri na pengine walifanya vibaya,Tatizo la uongozi wa sasa ambao Wiliam anapigaya debe wanachukua mabaya wanaacha mazuri.

- Hayo maneno makundu yameniacha sina mbavu! ha! ha! ha!, maana unakubali halafu unakataa! ha! ha! Great Thinker bana! ha! ha! ha! unasema nikaamulize baba, halafu tena unauliza kama ni baba huyo huyo aliyenituma, yaani sina mbavu!! ha! ha! ha!

William.
 
Ningetaka kusikia toka kwa William ni kwa vipi policies za huko nyuma zinatutesa sasa, na ugumu wa kuzibadilisha unakuwa wapi?

- Wewe ni msomi, so unapaswa kuelewa effect za binadam waliozoea kuishi kwenye failed policies, akiondoak kiongozi wa zile poilicies itawachua muda mrefu sana kuanza kujiamini, maana tatizo kubwa la kuzoea kuishi kwenye failed policies ni unapoteza kujiamini!

William.
 
Nasikitika sana pale ambapo JF inageuzwa kuwa kijiwe cha ubishi usio na tija.Tena hasa pale premium member anapokuwa ndiye sababu ya tabia hii.JF hasa jukwaa la siasa ni mahali pa hoja na kuelimishana yale tusiyoyajua kuhusu nchi yetu.Mtu unaweka mjadala mpana kama huu huku ukiwa reluctant kupokea lolote na kubishia kila kitu bila kujustify kwa hoja,unashangaza.Umeulizwa swali,umejibiwa.Umepewa mpaka vitabu usome, hutaki kwa hoja dhaifu kwamba haviko objective!Umeletewa government statement concerning the same issu unaigore na kuendeleza porojo zilezile za "tumefanya madudu mengi ndiyo maana tupo hapa tulipo".Inawezekana yapo madudu mengine lakini at least hili unaelimishwa hapa kuwa halikuwa dudu,si ukubali kuelimika kaka.Ukubali kuwa kuna vitu vinahitaji thorough research kabla ya kutaka kuvicriticize.Kama unapewa hoja with supporting documents na unazipinga basi tupe za kwako.Kama unapewa majina ya vitabu vya kusoma na unasema havipo objective(kabla hata hujavisoma)basi tupe vitabu ambavyo vipo objective na vinavyosapoti hoja yako(ambayo mpaka sasa haijulikani).Kinyume na hapo utakuwa ni ubishi usio na mwisho na JF itageuzwa kuwa kilinge cha ubishi.

- Sawa sawa Great Thinker!! yaani ninachoka kweli!!


William.
 
- Kila ninapoangalia tulikotokea hili Taifa, ninapatwa wasi wasi sana kwamba hatukufika hapa tulipo kwa makosa, tumefanya makosa mengi sana nyuma in terms of policies mpaka leo hii kurekebisha inakuwa ni almost impossible, ingawa watawala wa sasa wanajitahidi sana.

- Eti ni kwa nini Tanzania tuliunga mkono Waasi wa Nigeria waliokuwa wanaongozwa na General Ojukwu, kwenye kiu yao ya kujitenga na Nigeria Federation? Ninakumbuka tukiwa wadogo Shuleni, tulivyokuwa tunaimbishwa nyimbo za kumsifu Ojukwu, why? I mean ni policies ngapi huko nyuma we were wrong maana inaonekana ni nyingi sana that ni vigumu sana sasa kurekebisha njia!

- JE have we ever apologize to the Nigerians kwa makosa yetu ya kuuunga mkono uasi wa Ojukwu, dhidi ya serikali halali ya nchi hiyo?

- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!


William J. Malecela.

Huna haja ya kutuuliza sisi hebu sogea hatua chache tu mwuulize John Malecela kwani yeye wakati huo alikuwa mmojawapo wa Viongozi wa TZ
 
- Wewe ni msomi, so unapaswa kuelewa effect za binadam waliozoea kuishi kwenye failed policies, akiondoak kiongozi wa zile poilicies itawachua muda mrefu sana kuanza kujiamini, maana tatizo kubwa la kuzoea kuishi kwenye failed policies ni unapoteza kujiamini!

William.

kwani baba yako ameondoka?
 
Kama watu wanafuatilia vizuri mambo, CCM wamemgeuza Mwl Nyerere kuwa kinga. Kwa mfano CCM wakiambiwa hawana tena uwezo kuongoza nchi wanatakiwa waondoke wao wanajibu - Mwl Nyerere alisema bila CCM imara nchi itayumba. Lakini ukiwauliza kwa nini hii nchi inayumba wanasema Mwl alikuwa na sera mbovu sana!

Ndio maana nasuburi kwa hamu kubwa maelezo toka kwa William kwa nini policies za miaka ya 1960s zinatutesa sasa 2012? Na kwa nini CCM hawajaziondoa hizo policies wanazoona ni tatizo? Kama waliweza kufuta Azimio la Arusha (tena Mwl akiwa bado hai) wanashindwa nini kufuta hizo policies zingine wanazosema ni kero?

- Zinatutesa kwa sababu tumezoea kuishi kwenye failed policies, imetuathiri sana kisaikolojia hatuamini kwamba watwala wa sasa wanaweza kuanzisha sound policies, tukipatwa na matatizo tu kidogo kitaifa tunakuw wepesi kudai afadhali Mwalimu, sasa wengine tunashangaa mbona hawa Viongozi wengi tulionao wameanzia na Mwalimu, sasa iweje wawe na matatizo kuongoza vizuri kama utawala wa MWalimu ulikuwa perfect?

- Ndio tunakuja kuuliza haya maswali, na in the process tunajifunza kwamba apologists wa Mwalimu kuna one thing very starnge kwao, kuulizwa maswali serious au kukososlewa, kwa sababu haikuwa style yao, na cha ajabu wengi wao sasa ni supporter wa Chadema na huko wamepeleka ile ile tabia yao ya kutotaka kukosolewa,

- Can you imagine sasa hivi litokee taifa moja Duniani na kuanza kuwasaidia wakorofi huko Zanzibar na wakatoa statement kama yetu iliyowekwa ya kwa nini tunasaidia Biafra? I mean with your clear conscious una-support vipi a state kujitenga na Federation huku mataifa yoye ya Dunia yanayokubalika kwa sound policies wana-support Serikali ya Federation?

- To me hizi zilikuwa failed policies na tatizo ni nyingi sana in our past, na nina wasi wasi ndio maana mpaka leo tuna tatizo sana na kujiamini kuanzisha new sound policies, halafu the worst hatutaki kujadili kabisa makosa ya zamani!!

William.
 
Huna haja ya kutuuliza sisi hebu sogea hatua chache tu mwuulize John Malecela kwani yeye wakati huo alikuwa mmojawapo wa Viongozi wa TZ

- Can you imagine tukiaanza kuwaambia wachangiaji hapa wakaulize baba zao, ina maana tunahitaji kufunga JF, basi! ha! ha! ha!, yaani hizi ndio siasa ngumu sana za bongo, a Great Thinker anakurupuka kamuulize baba yako na huyu ni Great Thinker, unajua inasikitisha sana! ha! ha! ha!


William.
 
Back
Top Bottom