General Tyre yafungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

General Tyre yafungwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jan 19, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,670
  Trophy Points: 280
  Na Saed Kubenea
  MABILIONI ya shilingi za walipa kodi, ambayo Edward Lowassa alishinikiza yalipwe kwa kampuni ya kutengeneza matairi ya General Tyre (GT), yameteketea.

  Taarifa kutoka kiwandani, mkoani Arusha zinasema kiwanda kimefungwa na haijulikani kitapata wapi na lini mtaji mwingine wa kukifufua.
  Lowassa, kabla ya kujiuzulu nafasi ya waziri mkuu, alishinikiza wizara ya fedha na mipango, chini ya Zakia Meghji, kutoa Sh. 10 bilioni kwa General Tyre ili “kulinda kiwanda hiki” kisifilisike.

  Hivi sasa suala hili liko mezani kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye General Tyre inaomba “akubali” kuwa fedha zilizotolewa zilitumika vizuri, kinyume cha taarifa ya maodita waliopitia hesabu za kampuni hiyo.

  General Tyre inaomba pia serikali iongeze fedha nyingine, juu ya mabilioni ambayo matumizi yake hadi sasa bado ni utata mtupu.
  Kwa mujibu wa barua ya Katibu wa Lowassa wakati huo, B. Olekuyan kwa Katibu wa Meghji, Kumb. Na. PM/P/I/567/40 na iliyobeba kichwa cha maneno, “General Tyre East Africa LTD Arusha,”
  Lowassa aliagiza kama ifuatavyo:
  “Tuliishaliamulia suala hili kwamba wapewe government guarantee kulinda kiwanda hiki, mkopo wa awali na ajira za Watanzania. Kama WF (waziri wa fedha) ana maoni tofauti alete kwenye kikao. Vinginevyo atekeleze kabla ya tarehe 15/7/2007.”
  Katika barua hiyo, ambayo katibu wa Lowassa alikuwa anapeleka pia kwa waziri wa viwanda biashara na masoko, wakati huo Basi Mramba, anaelekeza nakala yake ipelekwe kwa mawaziri wote wanaohusika ili wajue msimamo wa waziri mkuu.

  Taarifa zinasema Mramba na Lowassa waliafikiana serikali itoa fedha kwa GT, kwa mujibu wa barua ya 28 Juni 2007 iliyotoka kwa Mramba kwenda kwa Meghji.
  Naye Mramba anajenga hoja ya kutolewa kwa fedha hizo haraka na bila masharti. Anaonya kwamba kuchelewa kutekeleza agizo la Lowassa kutasababisha kiwanda kufungwa.

  “Ushauri wangu kwako (Meghji) ni kwamba ujitahidi kuweka dhamana kwa ajili ya fedha hizo za NSSF haraka iwezekanavyo. Kama fedha zikikosekana, kiwanda hicho chaweza kufungwa,” inasema barua hiyo ya Mramba kwa Meghji.

  Hata hivyo, pamoja na kutolewa kwa mabilioni hayo ya shilingi, kiwanda hicho kimefungwa mwaka jana.
  Aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kiwanda hicho, William Shelukindo, mbunge wa Bumbuli (CCM), amethibitishia gazeti hili kuwa kiwanda kimefungwa pamoja na mabilioni ya shilingi yaliyomwagwa humo.
  Hata hivyo mabilioni hayo ya shilingi yameghubikwa na utata. Nyaraka ambazo gazeti hili limepata zinaonyesha kuwa siyo fedha zote zilizopelekwa kiwandani Arusha.

  Nyaraka zinaonyesha kuwa Sh. 1 bilioni zililipwa kwa kampuni ya ukaguzi ya DAI Consulting kutoka nchini Afrika Kusini. Kampuni ya DAI ilipewa fedha hizo na NSSF kama gharama za ushauri kwa GT.
  Lakini GT inalalamika, katika barua yake kwa Pinda, kuwa malipo ya Sh. 1 bilioni zilizotolewa kwa DAI Consulting ni fedha nyingi ikilinganishwa na kazi iliyofanyika.

  Meneja Mkuu wa GT, Deven Lohani, raia wa Nepal, katika barua yake ya 17 Agosti 2009 kwa Waziri Mkuu Pinda, anaorodhesha malalamiko kuhusu usahihi wa matumizi ya mabilioni hayo.

  Hata hivyo, kampuni ya matairi inasema haikuwa na njia nyingine ya kupinga malipo hayo kwa kuwa hiyo ilikuwa sehemu ya mkataba wa kupewa fedha hizo na NSSF. Kampuni ya DAI iliteuliwa na NSSF, inasema GT.
  “…Ni muhimu kufahamu kwamba kampuni ya DAI Consulting ilipendekezwa kwetu na NSSF. Katika kipindi hicho GT ilikuwa na matatizo makubwa ya kifedha na ililazimika kukubali sharti hilo,” inasema sehemu ya barua ya GT kwenda kwa Pinda.

  Meneja Lohani ameeleza kuwa tatizo kubwa lilikuwa ni kiasi hicho kutolewa kwa mafungu-mafungu na si kwa jumla kama ilivyokuwa ikitarajiwa.
  Shellukindo, hata hivyo, aliliambia MwanaHALISI kuwa kwa kadri anavyofahamu, nyingi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya kuifufua GT, zilitumika kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali yaliyokuwa yakiikabili kampuni hiyo.

  “Siwezi kusema kwa hakika ni kiasi gani kilitolewa na serikali katika kuifufua GT. Nilicho na uhakika nacho ni kuwa fedha nyingi zilitumika kulipa madeni ya kampuni,” alisema Shellukindo.
  Kwa kauli ya Shellukindo, Sh. 10 bilioni zilizotolewa na NSSF kwa udhamini wa serikali hazikutumika kufanya kazi iliyokusudiwa.
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,053
  Likes Received: 3,961
  Trophy Points: 280
  kama kawa walaji ni wengi na Kikwete amelala
   
 3. M

  Mundu JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kama kawaida yake, mzee wa vimemo EL, hapa pia amependekeza 10bn zitoke kwa kasi ya ajabu! Huyuuuuuuuu...
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kubenea inabidi aanze kuandika makala nzito kama hiyo kisomi zaidi zaidi na si kimipasho. Kutokana na facts alizonazo angeweza kuandika kitu kizuri kweli. Halafu ni muhimu kutambua watu na heshima zao badala ya kuwataja kiswahili swahili. Lowassa ni Mbunge na hata kama mtu hataki kumuita Mheshimiwa (sidhani kama kuna sababu ya kufanya hivyo) ni vizuri kumuita "Bw. Lowassa" n.k Hii ni katika suala la kuonesha weledi. Vile vile kina Bw. Mramba, n.k
   
 5. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  M.M.M, well said.... jamani hii GT tumeshaiongelea lakini facts na namna hii mambo ilivyowekwa ni kitu ambacho kwa kweli sio ada......

  In this I rest my case!!!
   
 6. M

  Mindi JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  Mimi sikubaliani na hoja kwamba Kubenea anatakiwa kuandika "kisomi" zaidi. Nini hasa maana ya kuandika "Kisomi"? Lengo kuu la mwandishi yeyote ni kuwakilisha ujumbe wake kwa namna anayoona inafaa zaidi. kuna vitendea kazi vingi anavyoweza kuvichagua na kuvitumia ili kutekeleza hilo. ameamua kutumia mtindo huo anaotumia, ambao mimi sioni tatizo kabisa. inaweza akawa pia ana "protest" na matumizi ya hayo maneno "Mheshimiwa" kwa ujumla wake, na HASA kwa watu ambao wamefanya kila jitihada kuunajisi uheshimiwa wa kila mtanzania. mwingine angeweza kabisa kutumia mtindo wa kejeli: "Mheshimiwa Lowasa" na bado akajenga hoja zinazomhusisha na kashafa mbalimbali ambazo haziendani na uheshimiwa huo. huyu naye atakuwa anatumia mtindo wake kuwasilisha ujumbe wake. hii habari ya kusema "kisomi" ni moja ya kasumba ambazo tunahitaji kuzipiga vita. weledi ni kuchagua katika kile alichoandika Kubenea, msingi wa ujumbe wake, na kuutolea maoni au kuufanyia kazi. sidhani ni kumtendea haki kuangalia tu style aliyotumia na kusema siyo ya "kisomi". ni sawa na kumtazama mtoa mada amevaa nguo aina gani na kufanya ndiyo ishu kubwa, na kuweka pembeni ujumbe anaowasilisha. Tumuache Kubenea aandike vile alivyochagua yeye kuwasilisha ujumbe wake
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks MMM

  Tatizo letu kubwa ni namna tunadeliver message... suala la general tyre ni very serious lakini ukiliweka kimitaa basi litaishia hivyohivyo... nadhani hapo tatizo ni edtorial tu, angetafuta mtu awe anamuwekea sawa habari zake

  lakini ni habari ya kusikitisha sana
   
 8. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Nilishawahi kufanya field pale miaka ya 2004-2005,kipindi kile hakukuwa na production,na kiwanda kilikuwa kinaelekea kufa.nakumbuka continental walikuwa wanahold share 25% na zilizobaki ni serikali,Na huyo CEO wa pale alikuwa mjerumani kama sikosei,alikuwa na rekodi pamoja na sifa ya kufufua viwanda vilivyokufa na vinavyoelekea kufa ila kwa TZ nadhani alishindwa.
   
Loading...