Salaam wanaJambo wenzangu. Nilitokea kupita mitaa ya Arusha siku chache zilizopita na kwa mshangao wangu mkubwa nikakuta kwamba kiwanda cha General Tyre (Njiro Area) kimefungwa.... Nilifanikiwa kuulizia juu juu (habari za mitaani) nikaambiwa kwamba kiwanda kimefungwa sababu wameshindwa kulipia bili za umeme na wamekatiwa umeme.
WanaJambo wenzangu, General Tyre ya miaka ile (wakati kila gari lilikuwa linavaa chapa jenerali) leo tunaambiwa kimeshindwa kazi sababu ya kushindwa lipia umeme??? Mimi nadhani mojawapo kati ya haya yametokea:
1. Ulaji kama ilivyo katika makampuni yetu makubwa!
2. Upinzani wa kibiashara kutoka katika makampuni kama Fireston (Kenya), Yana (TZ) na ya kiChina kumelisababisha kampuni letu kubwa kushindwa pambana!
3. Ni mbinu ya kulifanya shirika lionekane halina faida ili lisukumwe kwa bei ya kutupa!
Kulikoni General Tyre? Wenye data hebu tuambieni jamani....