General Tyre: Is it a slow death to a once an East Africa Giant??

Ngongo,
Ingekuwa vizuri kama ungeweza kutumia uzoefu wako uandike makala "What happened to our indigenous industries," kwa sababu suluhu waliyotumia akina Mwinyi na Mkapa, ya kubinafsisha kila kitu kiholela, ni ya madhara makubwa kwa Tanzania as a nation kulinganishwa na malalamiko kuwa viwanda vilikuwa havi-perform, therefore bora kubinafsisha kuliko kuviacha kuwa mzigo kwa taifa. Lingekuwa somo zuri sana kwa Watanzania wanaotafuta njia mbadala ya ubinafsishaji kiholela kama solution and the only way to development.
 
Heshima kwako Juan Manuel,

Mkuu suala la General Tyre limeshajadiliwa kwa kirefu sana hapa jamvini kama sijakosea thread ilianzishwa na Morani 75 mwaka 2008.Binafsi nilitoa ufafanuzi usiokuwa na mashaka kwasababu niliwahi kufanyakazi pale idara ya Accounts.

Labda nikupatie nondo kwa ufupi sana kama utahitaji maelezo marefu na mapana tafuta hiyo thread ya Morani 75.

General Tyre (EA) Ltd ilianzishwa miaka 70s na Mwl JK Nyerere kufuatia ziara alioifanya nchini Marekani.Kiwanda kilikuwa kijengwe Dar lakini Mwl alikuwa na sera ya kuwekeza viwanda mikoa mbali mbali ya Tanzania bahati nzuri kiwanda kikajengwa Arusha.Marekani walijenga Tanzania kwakuwa walikuwa wanaigia kwenye teknolojia mpya ya tairi ilivyo mitambo ya zamani ililetwa Tanzania.

Serekali ya Tanzania ilikuwa na hisa ya asilimia 76 na General Tyre Amerika asilimia 24.General Tyre marekani walikuwa na wajibu wa kuhakikisha wanaleta technology hivyo Chief Executive Officer,Finance Manager na Factory manager ilikuwa ni lazima watoke Marekani,Tanzania ilikuwa na nafasi moja tu ngazi ya management nayi ni Human Resource Manager.Mwenyekiti wa Board ya wakurugenzi na wajumbe nadhani saba walikuwa watanzania.

General Tyre Amerika ilikumbwa na matatizo ya kifedha kwenye miaka ya 80s ililazimika kuuza viwanda vyake vyote duniani kwa continental ya ujerumani General Tyre Tanzania nayo haikusalimika ikaangukia mikononi mwa Continetal Ujerumani.

Continental ilimleta Chief Executive Officer wake Muhindi [Nepal] mwenye uraia wa marekani Bwana Devendrah Lohani bila kuuma uma maneno kaburi la General Tyre likawa limechimbwa.Lohani aliikuta General Tyre katika hali nzuri [Stock,Cash flow,Debtors & Assets] kwa kushirikiana na mwenyekiti wa bodi Bwana Shelukindo na baadhi ya managers wazalendo Assets ziliuzwa hovyo fedha zilizopatikana badala ya kusaidia kampuni zikawafaidisha zaidi manager hasa Lohani.Hali ya General Tyre kufikia mwaka 2004 ikawa mbaya kiasi cha kushindwa kulipa mishahara wafanyakazi wake na madeni ya creditors yakawa yanazidi kila kukicha.

Mwaka 2005 CEO D Lohani kwa ushirikiano na Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba walifanikisha mpango wa mkopo wa us 10 milioni [Tsh 14.5 bilioni]kutoka NSSF kwaajili ya kumodernise kiwanda [ununuzi wa mashine za kisasa] na nusu ya fedha kulipa madeni ya benk zilizokuwa zikiidai General Tyre.Fedha zilipopatikana badala ya kununua mitambo mipya na ya kisasa zikaliwa mitambo ya zamani ikapakwa rangi.Muda wa kurejesha mkopo ulipofika General Tyre haikuwa na uwezo wa kurejesha hata senti moja mbaya zaidi haikuwa na sifa tena za kupata mkopo mwingine kutoka bank yoyote.

Asante sana mkuu kwa kunifahamisha,madudu ya nchi hii yanakera sana,unaweza ukaamua kuwa hata suicide bomber ili kuwamariza mafisadi,thanks.
 
"General Tyre imekufa, tusiwalaumu wakenya wala waganda, Viongozi wetu wamekosa uzalendo, kwa nchi kama Korea ya Kusini wakati wa uongozi wa Lee Park, viongozi kama Mary Nagu walikuwa wananyongwa au kupigwa risasi mbele ya raisi. Huku kwetu Mary Nagu anazidi kupanda chati na kukaa meza moja na raisi. Sijui labda kitafufuka baada ya SIRILI kupewa wizara hiyo tena, japo walikuwa pamoja na NAGU mwizi wa kura Hanang?
 
TISS is protecting those who are prosecuting Tanzania it is a shame-Go to Loliondo those the murderers of Tanzania (OBC) are protected by our own intelligence paid by our money. What a shame. JUAN it is not GENERAL TYRE ALONE-SERENGETI IS DYING AS A RESULT OF UNPROTECTED HUNTING IN LOLIONDO HUNTING BLOCK UNDER OBC CONCESSION WHO ARE PROTECTED NOT ONLY BY TISS BUT ALSO................... ANGALIA SIMALIZWE HAPA LABDA ANANISIKIA
 
"General Tyre imekufa, tusiwalaumu wakenya wala waganda, Viongozi wetu wamekosa uzalendo, kwa nchi kama Korea ya Kusini wakati wa uongozi wa Lee Park, viongozi kama Mary Nagu walikuwa wananyongwa au kupigwa risasi mbele ya raisi. Huku kwetu Mary Nagu anazidi kupanda chati na kukaa meza moja na raisi. Sijui labda kitafufuka baada ya SIRILI kupewa wizara hiyo tena, japo walikuwa pamoja na NAGU mwizi wa kura Hanang?
 
TISS is protecting those who are prosecuting Tanzania it is a shame-Go to Loliondo those the murderers of Tanzania (OBC) are protected by our own intelligence paid by our money. What a shame. JUAN it is not GENERAL TYRE ALONE-SERENGETI IS DYING AS A RESULT OF UNPROTECTED HUNTING IN LOLIONDO HUNTING BLOCK UNDER OBC CONCESSION WHO ARE PROTECTED NOT ONLY BY TISS BUT ALSO................... ANGALIA SIMALIZWE HAPA LABDA ANANISIKIA

KwenyeRED hapo FAFANUA kama zipo detaiils zozote.... you r a great thinker so you need to be specific bro, maana hii hujisaidii peke yako bali na wengine tuliopo hapa, kwa hiyo elezea kwa kina.
Kwenye BLUE hapo........... FICHA UPUMBAVU WAKO HAPA..... LAKINI USIFICHE HEKIMA.... kama kuna mtu mtaje unless otherwise UNAFICHA UPUMBAVU WAKO.... kama sio, basi TAJA sijui unamuogopa nani??? Hau huna ushahidi wa unachozungumza???
 
What i know about General tyre ni kwamba yule CEO mkenya alitumwa na YANA ile kampuni ya matairi ya kenya ili aje kuihujumu General Tyre na YANA waweze kuchukua soko la matairi. Siamini kwamba TISS hawakulijua hili bali nadhani uzalendo ni zero. Nawasilisha.
 
Alafu pabaya ni kwamba wengi mpaka leo hawajalipwa their just deserves. Hii nchi na serikali sometimes inasikitisha!!! yani kujivunia kuwa mbongo kwa kweli sometimes ni aibu tu.:puke:
 
Wapo wadau wa ndani ya bunge ambao naamini ni wahudhuriaji wazuri wa hapa jamvini!Nawaomba wapeleke hoja binafsi bungeni ili kunusuru hujuma!
NAOMBA KUWASILISHA
 
Ni ngumu kuamini waziri aliyehusika anaitwa panga zee lenye makali...
 
Msumari wa mwisho wapigiliwa jeneza la General Tyre

  • Ni kilio na kusaga meno kwa wafanyakazi 317
  • Serikali yakatisha rasmi ajira zao

MWAKA 2003 mmoja wa wafanyakazi vijana wa kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre East Africa Ltd cha Arusha alifichua tuhuma za ufisadi mkubwa uliokuwa ukifanywa na menejimenti ya kiwanda hicho kwa kuwaeleza baadhi ya wafanyakazi wenzake.

Mfanyakazi huyo hakuishia kueleza wenzake tu, lakini pia alichukua hatua za kuvujisha habari hizo katika vyombo kadhaa vya habari; lengo likiwa ni kuiamsha bodi ya wakurugenzi na serikali ambayo ndiyo yenye hisa nyingi katika kampuni hiyo kuhusu ufisadi huo.

Ufisadi huo uliokuwa unatishia ustawi na uhai wa kiwanda hicho ulikuwa unafanywa na meneja wake, Deven Lohan - raia wa Nepal kwa kushirikiana na wakuu wa idara mbalimbali ambao ni wazawa.

Vyombo kadhaa viliripoti habari za ufisadi katika kiwanda hicho lakini kwa mwamko kidogo wa serikali yetu; hakuna hatua za maana zilizochukuliwa huku Wizara ya Viwanda na Biashara, ambayo wakati huo ilikuwa chini ya Waziri Basil Mramba (Awamu ya Tatu), ikikalia mada hayo bila kuyachunguza.

Hata hivyo, pamoja na kuonyesha uzalendo wake, mfanyakazi huyo hakupata kuungwa mkono na wenzake katika kufichua ufisadi huo, na badala yake baadhi walimchongea kwa wakubwa ambao nao walichukua mara moja hatua za kumfukuza kazi.

Wafanyakazi hao walimwona mwenzao kama mtu msumbufu na vijana wa sasa ambao wanakosa nidhamu katika sehemu za kazi wenye tabia za kujaribu kuhoji kila jambo. Hata hivyo, jambo ambalo wafanyakazi hao hawakulijua ni kwamba ufisadi huo ungekuja kuwa "gharika" katika maIisha yao ya baadaye.

Baada ya kuachishwa kazi, mfanyakazi huyo alipata kazi katika moja ya makampuni ya simu za mkononi mkoani Arusha, na hadi leo bado anaendelea kufanya kazi na kampuni hiyo.

Lakini miaka mitano (mwaka 2007) baadaye, ufisadi huo mkubwa ulisababisha kiwanda hicho kusitisha uzalishaji na wafanyakazi wakawa wanalipwa mishahara bila kuzalisha chochote kwa miezi sita hadi mwaka 2008 kiwanda kilipofungwa kabisa.

Kiwanda hicho kilifungwa baada ya kushindwa kuagiza mali ghafi ya kutengeneza matairi, kukatiwa umeme na maji na wafanyakazi walipelekwa likizo isiyokuwa na malipo.

Tuhuma za ufisadi zilizokuwa zimeibuliwa kuhusu meneja huyo ni kutumia fedha za mkopo wa Shilingi bilioni 10 zilizotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa matumizi mengine badala ya kufufua kiwanda hicho kwa kuongeza uzalishaji.

Baada ya kiwanda kupata fedha hizo huku kikidhaminiwa na serikali, menejimenti ilipa kiasi cha fedha kwa madeni waliyokuwa wanadaiwa lakini kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 3.5 zinaelezwa kutumika bila vielelezo vyovyote.

Imeelezwa kuwa meneja huyo alitumia fedha nyingi kwa matumizi binafsi yakiwemo ya kuwaleta ndugu zake kutoka Nepal na mmoja wa wana wa mfalme wa nchi hiyo kutembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro, Serengeti na Manyara kwa gharama za kiwanda hicho!

Aidha, kiasi kingine cha fedha kilitumika kwa sherehe za kidini zilizofanywa na meneja huyo katika mikoa ya Tanga na Dar es Salaam.

Meneja huyo kabla ya kuondoka nchini na kurudi kwao pia aliuza nyumba nne za kampuni zilizokuwa katika eneo la Corridor katika manispaa ya Arusha kwa bei ya kutupa; huku moja akijiuzia mwenyewe kwa kwa kiasi cha Shilingi milioni 100.

Wakati Meneja huyo akifanya vitendo hivyo, ambavyo kwa ujumla vilionekana kama hujuma, wakuu wa idara nao hawakuwa nyuma katika "udokozi"; kwani inaelezwa kuwa kila moja katika idara yake alifuja kiasi alichoweza wakitumia mwanya wa udhaifu wa menejimenti.

Baadhi wanadaiwa kuiba vipuri mbalimbali vya mashine za kuzalisha matairi na wakati mwingine wakinunua vipuri feki ambavyo vilishindwa kufikia viwangi vinavyotakiwa.

Kufuatia mlolongo huo wa matukio ya ufisadi uliochukua zaidi ya miaka mitano sasa, wafanyakazi hao wapatao 317 wamekumbwa na hali ya hofu, mashaka na wasiwasi baada ya serikali kukatisha ghafla mikataba yao ya ajira kuanzia wiki iliyopita; huku wakiwa hawajalipwa mishahara kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Uamuzi huo wa kusitisha ajira za wafanyakazi hao ambao umekuja ghafla na bila kutarajiwa ulitangazwa wiki iliyopita na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk.Shaban Mwijaki wakati alipofanya mkutano na wafanyakazi hao.

Wafanyakazi hao wamepewa notisi ya kulipwa mshahara wa mwezi mmoja pamoja na mafao yao yatakayolipwa na serikali ambayo ndiyo yenye hisa nyingi katika kiwanda hicho.

Serikali inamiliki hisa karibu asilimia 80 za kiwanda hicho wakati kiasi cha hisa kilichobakia kinamilikiwa na kampuni ya Continental ya nchini Marekani.

Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyakazi, mafao ya serikali kwa mujibu wa sheria ni kidogo sana, na kuna uwezekano hakuna mfanyakazi atakayelipwa zaidi ya shilingi milioni 2 bila kujali muda ambao mfanyakazi husika amefanya kazi.

"Kuna waliofanya kazi miaka 17 wanaambullia Shilingi 700,000 na wengine milioni 1.2….sasa hapo utaona ni kwa kiwango gani wafanyakazi wanapata hofu ya maisha watakaporudi mitaani", alisema mmojawao mwishoni mwa wiki.

"Kwa kweli wafanyakazi wote wamepata hofu hasa wengi ambao tuna umri mkubwa ambao si rahisi kupata ajira serikalini na hata makampuni binafsi tunaweza kumudu gharama za maisha wakati hatujalipwa mafao ya maana", aliongeza mfanyakazi huyo.

Wafanyakazi hao wanadai kuwa wao hawahusiki na ubadhirifu huo na hatua zilizochukuliwa na serikali ni sawa na kuwapa adhabu kwa makosa ambayo hawakutenda.

Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi (TUICO), tawi la kiwanda hicho, Lukio Tulule alikataa kutoa ufafanuzi kuhusu utaratibu na sheria inayotumiwa na serikali kulipa mafao kwa wafanyakazi hao kwa madai kuwa jambo hilo limemfanya achanganyikiwe.

"Ndugu yangu, sielewi chochote naomba uniache tu suala hilo limenichanganya sana….nipigie simu Jumatatu nitakuwa nimepitia nyaraka zilizopo na nitajua utaratibu uliotumika kulipa mafao yetu", alisema.

Akizungumzia hatua ya kukatisha ajira za wafanyakazi hao, Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa serikali imechukua uamuzi huo kutokana na ukweli kuwa kwa sasa kiwanda hicho hakiwezi tena kuzalisha matairi hadi hapo serikali itakapopata mbia mwingine.

"Kutokana na kiwanda kuwa na madeni makubwa na ufisadi uliofanywa na menejimenti, serikali imeona ni vyema kiwanda hiki kikafungwa kwanza na wafanyakazi kulipwa mafao yao wakati tukijipanga upya kutafuta hatua za kuchukua", alisema.

Kufungwa kwa kiwanda hicho kunahitimisha kuwepo kwa viwanda vya umma katika mkoa wa Arusha vilivyokuwa vimeanzishwa katika miaka ya 70 na 80 na ambavyo karibu vyote vilikuwa vimebinafsishwa wakati wa serikali ya awamu ya tatu kwa wawekezaji mbalimbali, lakini vingine vikiwa vimetelekezwa na kubakia magofu.

Viwanda hivyo, ambavyo viliufanya mkoa wa Arusha kuwa ni mkoa wa pili kwa kuwa na uchumi mzuri baada ya Dar es Salaam, ni pamoja na kiwanda cha bia, kiwanda cha madawa ya binadamu cha TPA, kiwanda cha kusindika nafaka cha NMC, Baby Food, kiwanda cha nguo cha Kiltex, kiwanda cha sabuni cha EMCO na kiwanda cha mbao cha Fibreboard.


Source: Raiamwema.


Hii habari kwa kiasi kikubwa imejaa uzushi.

Kijana anayezungumziwa kwamba alifichua ufisadi uliokuwa ukifanywa na managemant ya GT kwa kuwaeleza wafanyakazi wenzake na baade vyomba vya habari si za kweli hata kidogo tena zimejaa ubabaishaji na uvivu wa hali ya juu kwa mwandishi wa habari hii. Gazeti la Raiamwema linapaswa kuwaomba radhi wasomaji wake kwa kuandika habari pasipo kufanya utafiti wa kutosha.

Kwa sisi tuliowahi kufanyakazi GT uliposoma hii habari tulijua moja kwa moja kijana anayezungumziwa anaitwa Antony Mhandiki.

Kilichomwonda A Mhandiki si kwasababa alifichua ufisadi uliokuwa ukifanywa na managemant ya General Tyre bali kugombea ulaji baina yake yeye na L Mgoyo [Purchasing Manager]

Bwana A Mhandiki alikuwa Ag Marketing Manager kuanzia mwaka 2004 mpaka alipoondolewa mwaka 2007. Kama mkuu wa division ya masoko Bwana Mhandiki alihusika na uhagizaji wa vifaa vya promotion [t-shirt, kofia,key holder na vifaa vya michezo] kupitia idara ya ununuzi [Purchasing]. Kampuni ya Zizou ilipata tender ya kuleta vifaa vyote vyenye thamani ya zaidi ya tsh 250 milioni,ugomvi wa Bwana Mhandiki na Bwana Mgoyo ulisababishwa na kutokugawana kwa usawa 10% na mgawo wa fedha za vifaa ambavyo kampuni ya Zizou hawakuweza kusupply.

Bwana Leonard Mgoyo alitumia vyema fursa iliyokuwepo wakati huo, vyombo vya habari hasa gazeti la RAI na baadaye Mwahalisi yalikuwa yakitoa habari za ufisadi uliokuwa ukifanywa na Bwana D Lohani.

Bwana L Mgoyo kwa uchungu wa kunyimwa ulaji alikwenda kujengea hoja kuu mbili kwa manaja mkuu aliyeanza kulemewa na kashfa za ufisadi.

[1] Kwakuwa Bwana A Mhandiki aliwahi kufanyakazi katika gazeti la Daily news ni rahisi kwake kujuana na wanahabari na kuwa yeye anahusika na uvujaji wa habari zilizokuwa zikihihusisha General Tyre na ufisadi.

[2] Gazeti la RAI wakati huo lilikuwa na wanahabari wengi wahaya/wanaotoka mkoa mmoja na Bwana A Mhandiki.

Hoja hizi mbili zilisababisha Bwana A Mhandiki kuachishwa kazi General Tyre, ingawa manaja mkuu alikuja kukiri baadae alifanya kosa kubwa kumwachisha A Mhandiki kazi kwasababu bado habari za ufisadi ziliendelea kutoka kwenye vyombo vya habari.

Najua waandishi wa habari wa gazeti la Raiamwema wanatembelea sana hapa jamvini itakuwa jambo la maana kama mtaweza kuirekebisha habari mliyoitoa bila kuifanyia utafiti wa kutosha. Tuliokuwa tunazitoa habari za ufisadi tuko bado hatujafa tena tunafahamiana sana. A Mhandiki alikuwa ni sehemu ya viongozi waliosababisha General Tyre ikafikia hapo ilipo.

Naomba kuwasilisha.

Wewe ndo huyo "whistleblower?" Uliefukuzwa kazi?
 
Kiwanda cha General Tyre kimeshindwa kuzalisha matairi kwasababu ya ufisadi wa wanasiasa wenye tamaa ya kutaka kumiliki kila kitu kwa gharama yoyote.Nimesoma post za wenzangu ambao wamejitaidi kueleza kwa undani jinsi GTEA ilivyotafunwa na viongozi wetu wasiokuwa na huruma kwa nchi yao.

Binafsi mimi ni mfanyakazi wa General Tyre [EA] Ltd, kwahiyo ninachoandika si kitu cha kusikia au kuambiwa bali ni mambo ambayo nimeyashuhudia yakitendeka. Tulijitahidi kupiga kelele kwa kadri ya uwezo wetu lakini hakuna waliotaka kusikiliza kilio chetu mpaka kiwanda kilipofungwa au kusimamisha uzalishaji kabisa.

Kwanza nakubaliana kwa 100% na ndugu Kabonde kwamba mashine za General Tyre ni za zamani sana,kiasi kwamba hata ajira kwa wafanyakazi wa kiwandani walitakiwa kuwa na kilo zisizopungua 70 kgs,kigezo cha elimu kilikuwa akizingatiwi sana kama uzito.

General Tyre ilianza kuyumba mara mfumo wa uendeshaji ulipobadilishwa,mfumo wa zamani ulikuwa hivi, General Manager [Chief executive officer], Sales & Marketing Manager, Chief Financial Officer, Factory Manager wote walikuwa wanatoka Marekani, Human Resouce Manager alikuwa mtanzania na wote walikuwa wanaingia kwenye mikutano ya Bodi. Mfumo mpya uliwaengua managers wote kutoka Marekani isipokuwa General Manager [Chief executive officer] pekee. Tatizo kubwa ni kwamba manages wa kitanzania walikuwa si wajumbe wa bodi na mamlaka ya nidhamu ilihamishiwa chini ya General Manager. Sijui kama wa JF mmenielewa au mmeshagundua sanaa iliyofanyika.

Mfumo mpya ulimpa madaraka makubwa kupita kiasi General Manager afanye kila analotaka kufanya bila kuhojiwa na Managers wa kitanzania, mfumo huu pengine ungeweza kufanyakazi kama bodi ya wakurugenzi ingeamua kufanyakazi yake ipasavyo lakini bodi nayo ikaungana na General Manager kuiba mali ya umma.

Naomba kutafautiana na ndugu Kabonde pale anaposema General Tyre iliacha kufanya ukaguzi wa kila mwaka [annual audit] kuanzia mwaka 2005. Mwaka 2005 ukaguzi ulifanyika na kampuni ya Ernst & Young kama kawaida lakini ripoti haikutolewa. Kuna sababu kuu mbili zilizopelekea ripoti ya wakaguzi Ernst & Young kufichwa nazo ni:

1) Mwaka 2005 wakaguzi nje {external auditors} walitakiwa na NBAA kukagua kwa kufuata viwango vya kimataifa. Kabla ya maagizo ya NBAA wakaguzi walikagua Balance Sheet peke yake. Ukaguzi wa mwaka 2005 uliofanywa na vijana wa Ernest & Young ulikuwa wa kutisha kwa mafisadi

{A} walikagua Trading, Profit & Loss a/c {B} Account zote zilizokuwa na figures kuanzia 1milioni.

Kwa wataalamu wa fani ya uhasibu watanielewa haraka kwamba Trading,Profit & Loss a/c matumizi {expenses} zinaonekana bila shida, Devendra alidhani kuna baadhi ya wafanyakazi wa department ya Account walimchongea kwa wakaguzi kumbe utaratibu ulikuwa umebadilika.

2) General Manager Devendra Lohani Mhindi wa Nepal mwenye uraia wa Marekani hakuwahi kukaguliwa kwa kiwango hiki.

Bahati mbaya kwake mwaka 2005 alikuwa ame-lobby akapata mkopo wa tsh 12.3bilioni kutoka NSSF kwa njia za ajabu ajabu. Ernst & Young walipomaliza ukaguzi walitoa Draft kwa General Manager kama taratibu za ukaguzi zinavyotaka ili management iweze kuipitia na kuangalia kama kuna hoja ambazo zimekosewa zisahihishwe kabla ya kupelekwa kwenye bodi ya wakurugenzi.

Hoja za wakaguzi zilikuwa nzito kwa fisadi Devendra,hasa matumizi yake binafsi ambayo Ernst & Young walisema wazi ni makubwa kupindukia, $ 1 million Consultation fee ya Debt Advisory International nazo zilimkaba koo Devendra, gharama za kumkrimu mfalme Gyanendra Shah wa Nepal na ujumbe wake nazo zilikosa majibu kutoka kwa Devendra Lohani.

Kila kitu kinawezekana Tanzania bwana Devendra hakurudisha ripoti kwa wakaguzi na bodi ya wakurugenzi chini ya mwenyekiti W Shelukindo nayo haikuhangaika kuiulizia na huo ndiyo ukawa ni mwanzo na mwisho wa kufanyika kwa ukaguzi General Tyre. Mara nyingi najiuliza bodi ya wakurugenzi ya General Tyre ilikaa bila kuona financial report kwa miaka mitano sijui walikuwa wanajadili nini zaidi ya kugawana posho za vikao na kumwacha bwana Devendra akitutambia kwamba yeye yuko mbele ya serekali yetu tukufu kwa miaka kumi zaidi!

Inabidi nipumzike kidogo mambo ya GTEA ni mengi mno ni bahati mbaya ufisadi wa Devendra haukupewa umihimu unaostahi labda kwasababu General Tyre iko mikoani pengine ingekuwa Dar tungeisikia kama tulivyoisikia EPA, Radar nk
Mambo yanatisha historia ya GT kuanguka kwake kunatisha.
 
Back
Top Bottom